Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
EPL: Man City walazwa na Aston Villa, United waishinda Chelsea huku Liverpool wakiilaza Sheffield United
Kombora lililopanguliwa na Leon Bailey liliwapa Aston Villa ushindi uliostahili dhidi ya Manchester City huku wageni hao wakiendelea kusajili matokeo mabaya.
Villa walikuwa bora kwa muda wote dhidi ya mabingwa hao, ambao sasa wamecheza mechi nne za Premier League bila kushinda kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka saba.
City kwa mara nyingine tena walikosa ushawishi wa Rodri aliyefungiwa, baada ya kupoteza michezo yao mitano iliyopita, mchezo bora wa Villa ulithibitisha hatua kubwa zilizopigwa na klabu hiyo chini ya usimamizi wa Unai Emery.
Villa hawakuogopa kusonga mbele tangu mwanzo, huku kipa wa City Ederson akiokoa mara mbili mapema kutoka kwa Pau Torres na Bailey, huku kipa Emi Martinez akimnyima Erling Haaland magoli mawili ya wazi .
City walikosa utulivu na walikabiliwa na misukosuko wakati fulani, na ushindi wa Villa ulikuja dakika 16 kabla ya mpira kumalizika wakati kombora la Bailey kutoka pembeni mwa eneo lilipomgusa Ruben Dias na kumpita Ederson aliyekuwa hoi.
Man United wailaza Chelsea 2-1
Kwa mara ya pili msimu huu, Scott McTominay alifunga mabao mawili Old Trafford na kuipatia timu yake ya Manchester United ushindi mnono huku akipunguza shinikizo kwa meneja Erik ten Hag.
Juhudi za hivi punde za kiungo huyo wa kati wa Scotland dhidi ya Chelsea hazikuwa za kusisimua kama zile mbili alizofunga dakika za majeruhi na kuwashinda Brentford mwezi Oktoba.
Lakini ulikuwa usiku ambapo United walipoteza nafasi za kutosha - ikiwa ni pamoja na mkwaju wa penalti wa Bruno Fernandes
Juhudi za kwanza za McTominay zilizaa bao la kawaida kutoka kwa maguu 12 huku shambulio la kichwa lililozuiwa na Harry Maguire likimgonga
Kisha, baada ya Cole Palmer kusawazisha kabla ya kipindi cha mapumziko, McTominay alivamia lango la Chelseana kufunga krosi ya Alejandro Garnacho dakika 21 kabla ya mchezo kumalizika.
Alipaswa kuwa na hat-trick yake ya kwanza kwa juhudi zake baada ya kupewa pasi na Antony lakini akapiga juu.
Mwishowe, haikujalisha, kwani United ilinusurika shinikizo la mwisho la Chelsea, akiwemo mchezaji wa akiba Armando Broja ambaye kichwa chake kiligonga mwamba wa goli .
Liverpool yavunja matumaini ya Sheffield United
Liverpool iliharibu ugeni wa Chris Wilder wa Bramall Lane na kusalia nyuma ya kwenye visigino vya vinara wa Ligi ya Premia Arsenal.
Wilder, ambaye aliiongoza Sheffield United kupandishwa daraja mara mbili katika utawala wa miaka mitano kabla ya kuondoka kwa njia isiyo ya kawaida mnamo 2021, alipokea hisia kali kutoka kwa waaminifu wa Blades aliporejea dimbani.
Hata hivyo, Virgil van Dijk alifunga mpira wa kona iliopigwa na Trent Alexander-Arnold na kuzima matumaini ya mashabiki wa Bramall lane licha ya Sheffield United kudai kwamba alikuwa amechezea visivyo Anel Ahmedhodzic
Kulikuwa pia na utata kuhusu bao la pili la The Reds katika dakika za lala salama huku Darwin Nunez akidaiwa kumfanyia Jayden Bogle kabla ya mchezaji Dominik Szoboszlai kufunga.
Liverpool, ambao wameshindwa mara moja pekee kwenye ligi msimu huu wakati wachezaji wao tisa walipopoteza dakika za lala salama dhidi ya Tottenham, wako pointi mbili nyuma ya Arsenal ambayo ipo kileleni.
The Blades, kwa upande wake, wanasalia mkiani,