Sababu ya makundi ya Waislamu kupinga sare mpya ya shule India

Iliyochapishwa

Mzozo umezuka kwenye jimbo la Kerala kusini mwa India baada ya shule ya serikali kuwaruhusu wanafunzi wasichana kuvaa suruali.

Manafunzi Sringi CK alisubiri akiwa kwenye kituo cha usafiri akisubiri kuabiri basi kwenda shuleni akiwa amevaa sare yake mpya, alipata pongezi kutoka kwa mwanamke ambaye hakumfahamu hatua iliyofanya ajiskie vizuri.

"Mwanadada mmoja aliniambia nilikuwa nadhifu sana na kwa kweli nilifarijika sana," msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 wa darasa la 11 katika shule ya serikali ya wasichana kwenye mji wa Balussery aliiambia BBC.

Lakini Sringi alpoiwasili lango la shule, alikumbana na waandamanaji waliokuwa wamezuiwa na polisi ambao walikuwa wakilalamika kuwa wasichaana hawastahili kuvaa suruali na shati kama wavulana

Kabla ya mabadiliko hayo wanafunzi wa kike walivaa kanzu ndefu za kitamaduni, suruali zilozolegea na koti za kufika kiunoni.

Mwalimu mkuu Indu R aliiambia BBC kuwa mwaka uliopita wasichana ambao kwa sasa wako darasa la 12 walipendekeza kuruhusiwa kuvaa sare sawa na za wavulana.

Alisema aliona uzito kwenye pendekezo hilo kwa kuwa "wengi wa wanafunzi wetu wanavaa jeans na koti kama wasichana wengine popote pale duniani na koti la kufika kiunoni halikuwa bora kwa hali ya hewa nyenye unyevunyevu ya Kerala.

"Kwa hivyo tulijadili suala hili na walimu kisha tukaita mkutano wa walimu na wazazi. Wengi walikubali kwa hivyo tukaamua kubadilisha," Bi Indu alisema.

"Lakini ni wasichana wachache wamebadilisha," aliongeza.

Bi Indu alituma picha kwa BBC za kundi la wanafunzi wakiwa na sare zao mpya, wakipiga selfi wakicheka na kuruka kwa furaha.

Sringi ambaye ni kati ya kundi hilo anasema anapenda sare yake mpya kwa sababu inafanya ahisi vizuri na haizuii viungo vyake.

Mabadiliko hayo ya sare yanaungwa mkono na serikali ya Kerala. "Sare za shule na mfumo mzima wa shule unastahili kubadilika na nyakati. Waziri wa elimu V Sivankutty aliiambia BBC. "Tuna matumaini kuwa shule zaidi zitajiunga na mpango huu kuwafahamisha wanafunzi wasichana kuhusu ubaguzi wa jinsia mapema."

Lakini sare hiyo mpya haijakubaliwa na makundi ya waislamu yenye kudumisha tamaduni yanayosema kuwa watoto wao wanalazimishwa kuvaa sare hizo mpya.

"Uamuzi ulifanywa bila ya kuita mkutano mkuu wa walimu na wazazi na sasa wasichana wetu wanalazimishwa kuvaa suruali na shati kama wavulana. Pia ni mzigo mkubwa kwa familia maskini," alisema Mujahid Balussery mwanachana wa kamati ya kiislamu ya kupinga sare za jinsia moja.

Matamshi kama hayo kutoka makundi wa waislamu wiki iliyopita yamekosolewa vikali kutoka kwa watu wengine jimbo la Kerala na kote nchini India, huku wakosoaji wakisema ni juhudi kutoka makundi ya orthodox kuwawekea vikwazo wasichana.

Kerala linatajwa kuwa jimbo lenye wasomi wengi zaidi nchini India likitajwa kufikia asilimia 100 kwa masomo.

Wasichana wanachukua asilimia 48.96 ya wanafunzi wote walio shuleni na wengi husoma hadi viuo vikuu.

Mwalimu mkuu Indu, anasema mzozo kuhusu sare mapya ni jambo la kushangaza kwa kuwa wasichana wa kike kwenye shule nyingi za kibinafsi jimbo la Kerala wanavaa suruali, na shule moja ya serikali imebadilisha kwenda sare za jinsia moja kwa watoto wadogo mwaka 2018.

"Tangu kuzaliwa, tunatofautisha kati ya wasichana na wavulana- tunawanunulia midoli tofauti, wavulana wanapata bunduki na gari huku wasichana wakipata wanasesere, wavulana huvalishwa nguo za bluu huku wasichana wakivalishwa nguo za rangi ya waridi na wanapokua, viatu vyao na nguo pia huwa tofauti.

Lakini nafikiri ikiwa wasichana wanajiskia vizuri na kuwa na ujasiri wanapovaa suruali na shati, basi wanastahili kuruhusiwa kuvaa vile. Nahisi watoto wote wanastahili kupewa uhuru ulio sawa na fursa sawa."