Kwanini China inaweza kushinda mashindano mapya ya kujihami kwa silaha duniani?

Image of Chinese soldiers
Iliyochapishwa

China inajenga jeshi lake kwa haraka.

Hatua ilizopiga katika teknolojia ya makombora, zana ya nuklia na mifumo ya intelijensia vimezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa waangalizi wengi wa nchi za magharibi, wanaoamini kuwa kuna mabadiliko makubwa katika usawa wa kimataifa wa nguvu za kijeshi.

Rais Xi Jinping ameamrisha jeshi la China kujiboresha ifikapo mwaka 2015. Anasema wanastahili kufikia kiwango cha jeshi la kimataifa lililo na uwezo wa kupigana na kushinda vita ifikapo mwaka 2049.

Bajeti kubwa

China imekosolewa na baadhi ya wataalamu wa kimataifa kwa kukosa uwazi kuhusu ni kiwango gani pesa inatumia kwa ulinzi.

China huchapisha data rasmi za matumizi yake lakini nchi za magharibi zinakadiria kuwa bajeti china kwa jeshi lake ni kubwa zaidi.

Inaaminika kuwa kwa sasa china inatumia fedha nyingi zaidi kwa jeshi lake kuliko nchi yoyote ile isipokuwa Marekani.

m
Presentational white space

Bajeti ya jeshi la China, imepita ukuaji wa ujumla wa uchumi wake kwa karibu muongo mmoja kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa masuala ya kimatafa mjiini Washington.

Kuongeza zana za nuklia

Mwezi Novemba idara ya ulinzi nchini Marekani ilitabiri kuwa China ilikuwa na mpango wa kuongeza mara nne zaidi zana zake za nuklia ifikapo mwishoni ma muongo wa sasa.

China inalenga kumiliki takriban silaha 1,000 zinazoweza kubebwa na makombora ifikapo mwaka 2030.

Vyombo vya habari nchini China vilitaja madai haya kuwa uvumi na wenye upendeleo.

Lakini wataalamu kutoka taasisi ya utafiti kuhusu silaha huko Stockholm wanaochapisha data za kila mwaka kuhusu zana za nuklia, wanasema China imekuwa ikiongeza zana zake miaka ya hivi karibuni.

China bado ina kasoro ikilinganiswa na silaha 5,550 za marekani zinazoweza kupachikwa kwa makombora, lakini ongezeko lake la zana za nuklia ni moja ya tisho kubwa kwa ubabe wa jeshi wa nchi za magharibi.

Makombora ya Hypersonic

m

Makombora ya Hypersonic husafiri kwa kasi mara tano zaidi kuliko sauti

Hayana kasi kubwa kuliko yale ya masafa marefu au ICBM, lakini ni vigumu sana kuyatambua yakiwa angani na hayawezi kuzuiwa na baadhi ya mifumo ya ulinzi wa makombora.

"China wanaelewa kuwa bado wako nyuma, kwa hivyo wanataka kuwapita wengine," kulingana na Dr zeno Leoni kutoka chuo cha Kings huko London.

"Kuunda silaha za hypersonic ni moja ya njia wanayotumia kufanya hivyo."

China imekana kufanyia majaribio makombora ya hypersonic, lakini wataalamu wa nchi za magharibi wanaamini kuwa majaribio mawili ya makombora yaliyofanywa mwezi Julai ni ishara kuwa jeshi lake liko njiani kupata silaha hizo.

Presentational white space

Dr Leoni anasema hata kama makombora ya hypersonic hayataleta mabadiliko makubwa, yanaweza kufanya sehemu muhimu kuwa katika hatari ya kushambuliwa.

"Makombora ya hypersonic kwa mfano yataleta changamoto kubwa katika kulinda meli za kubeba ndege za kivita," anasema.

Lakini pia anasema kuwa tisho kutoka kwa makombora ya hypesonic ya China huenda limechochewa na baadhi ya maafisa wa nchi za magharibi, wenye lengo la kushinikiza kuongezwa bajeti kwa teknolojia ya zana za jeshi.

Mifumo ya intelijensia

m

China ina mikakati ya kuunda zana zinazotumia intelijensia kwa mujibu wa idara ya ulinzi nchini Marekani.

Taasi ya masuala ya sayansi ya jeshi nchini China imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa hili linafanyika kwa kushirikisha teknolojia ya sekta za kibinafsi na ya mashirika ya serikali

Ripoti zinazema kuwa huenda China tayari inatumia mifumo ya intelijensia kwenye roboti za jeshi na mifumo ya kuelekezwa ya makombora na pia ndege zisizokuwa na rubani na vyombo vya majini visivyo na nahodha.

Tayari China imeendesha oparesheni kubwa za mitandaoni nchi za ng'ambo kwa mujibu wa utafiti wa hivi majuzi kutoka kwa wataalamu.

Mwezi Julai, Uingereza, Marekani na EU waliilaumu China kwa udukuzi wa mitandao uliolenga mitambo ya Microsoft.

Jeshi kubwa zaidi la wanamaji duniani Lakini lisolo na nguvu kuliko yote.

China imeipita marekani na kuwa na jeshi kubwa zaidi la wanamaji duniani lakini wataalamu wanasema kuwa idadi ya meli ndio huamua ubabe wa jeshi la wanamaji.

m

Kwa sasa Marekania inangoza kwa ubabe wa jeshi la wanamaji ikiwa na meli 11 za kubeba ndege za jeshi huku China ikiwa na mbili, na nyambizi nyingi zaidi zinazotumia nishati ya nuklia, na pia meli zingine kubwa za vita.

Lakini China inatarajiwa kupanua zaidi jeshi lake la wanamaji.

Kanali wa zamani wa jeshi la China Zhou Bo, anaamini kuwa ni muhimu sana kwa China kuboresha jeshi lake la wanamaji ili kukabiliana na vitisho vilivyo baharini.

Anasema tatizo kubwa linaloikumba China ni uchokozi wa Marekani katika maji ya China.

Jeshi la Marekani linatabiri kuwa kati ya mwaka 2020 na 2040 idadi ya meli zote za jeshi la wanamaji wa China zitaongezeka kwa karibu asilimia 40.

Wakati ujao usiotabirika

China inahama kutoka kipindi cha kutotumia makabiliano hadi kile cha vitisho zaidi?

Hadi sasa mfumo wa China ni ule wa kushinda bila vita, anasema Dr Leoni, Lakini anaongeza kuwa inaweza kubadilisha mikakati hii siku za usoni.

"Kuwa na jeshi la wanamaji la kisasa italeta mabadiliko."

Lakini kanali Zhou anasema kuwa hofu ya nchi za magharabi haina msingi.

"China haina mpango wa kuwa polisi wa dunia kama Marekani," anasema. Hata kama China siku moja itakuwa na nguvu zaidi itadumisha sera zake.