Kuondolewa marufuku kwa wasichana wa shule wanaopata mimba kwaibua hisia mseto Tanzania

v
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Hatua ya Serikali ya Tanzania kuondoa marufuku ya wanafunzi wanaopata ujauzito kurejea masomoni, imepokelewa kwa mtazamo tofauti kwa wale waliokuwa wanaonekana kuunga mkoano na wale waliokuwa wanapinga. Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alipozungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika miaka 60 ya uhuru wa Taifa hilo.

Mbali na wanafunzi waliopata mimba, wanafunzi wengine waliokatiza masomo ya kwa sababu mbalimbali nao wataruhusiwa kurejea katika mfumo huo rasmi.

Rebecca Gyumi, Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wasichana Tanzania, Msichana Initiative, ameiambia BBC kwamba hatua hiyo ya serikali wameipokea vizuri ila bado kuna wasiwasi kidogo

'tumepokea kwa furaha sana , na niseme tu tunatumaini waraka ambao mheshimiwa waziri amehaidi atautoa, utakaoelezea utekelezaji wa tamko lake, itaweza kutupa picha ya namna ambayo serikali imejipanga kutekeleza hili', alisema Gyumi na kuongeza kuwa inapaswa kuwekewa sheria hili tamko la waziri na waraka wake uwe na nguvu za kisheria.

'tuaamini ni hatua nzuri na zaidi tunatumaini serikali itaweza kuhusisha mchakato ule wa sera na kuweka sheria, ambapo hili tamko pamoja na waraka utaweza kuchukuliwa katika sheria', alisema Gyumi.

Kwenye mtando wake wa twitter Chausiku yeye amepongeza tu hatua hiyo ya serikali ya Tanzania.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Mtu anayejiita fundi mitambo alitaka serikali ya Tanzania kuwaangalia na wale wanaowapa mimba wasichana hao, ili kulea vyema mtoto anayezaliwa.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Mwingine anayeitwa dhul-qarnain, ambaye alichangia kwenye ukurasa rasmi wa wizara ya elimu Tanzania, akionyesha kuwazodoa wale ambao waliunga mkono hatua ya kufukuzwa mabinti waaopata imba mashuleni na sasa wanapongeza tena hatua ya kuondolewa kwa marufuku hiyo.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Mwanaharakati Fatma Karume, naye hakuwa nyuma akijibu chapisho la aliyewahi kuwa waziri wakati wa utawala wa hayati Magufuli, Faustine Ndugulile baada ya mbunge huyo wa Kigamboni kuchapisho kuelezea hatua ya serikali kuruhusu wanafunzi waliopata mimba kurejea shuleni. Fatma akionyesha kama jitihada zaidi zilihitajika.

Ruka X ujumbe, 4
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 4

Shirika la utafiti la Twaweza Tanzania, liliwahi kufanya utafiti kubaini wanaotaka wanafunzi wanaopata mimba kurejea shuleni, wakati ule kaba ya katazo kuondolewa. Mmoja wa maafisa waandamizi wa shirika hilo, Anastazia Rugaba, aliiambia BBC kwamba, ni jambo jema.

'naungana na watanzania wengine zaidi ya asilimia 70% ambao katika tafiti zetu walipendekeza kwmaba watoto wa kike wapewe nafasi ya kurudi masomoni pindi wanapokuwa wajawazito, kwa hiyo wakishajifugua warejee shule', alisema.

Upo wasiwasi kwamba, hatua hii ya serikali huenda ikachochea wasichana wengi kujiingiza kwenye ngono za mapema na ndoa za utotoni, Rugaba anapingana na hilo, 'Ushuhuda wa wenzetu waliopitisha sera hii kama vile Zanzibar, Kenya, Zambia, Botswana hata Uganda, tangu wamepitisha sera hii matatizo ya ujauzito yamepungua sana kwenye mashule,' alisema.

C

Chanzo cha picha, Getty Images

Juni 2017 Hayati Magufuli alipiga marufuku wanafunzi wanaopata mimba mashuleni kuendelea na masomo ya shule ya msingi na sekondari akisema ndani ya utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shuleni.

Akazitaka taasisi zinazotetea utaratibu wa wanafunzi waliopata mimba kurudi shuleni, kufungua shule zao za wazazi lakini si kuilazimisha Serikali kufanya hivyo.

Kauli ya Magufuli ikazua mijadala na upinzani kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu nchini na nje ya nchi hiyo, wakiona hatua hiyo ni kumnyika haki ya kupata elimu mtoto wa kike.

Shirika la Human Rights Watch lilisema mwezi uliopita kwamba marufuku hiyo ya serikali ya Tanzania kwa wanafunzi waliopata mimba imewanyima maelfu ya wasichana haki ya kupata elimu.

Baadhi ya wasichana walioathirika kwa kuondolewa shule wakiwa wajawazito wameiambia BBC kwamba ni hatua ya furaha. Ngayo, ni jina la kubuni alipita kwenye changamoto hiyo alipoolewa akiwa na umri mdogo wa miaka 13 na kuacha shule ingawa alifaulu kwenda kidato cha kwanza.

Ngayo amefurahi kwa hatua aliyoifikia baada ya kupata elimu na kuweza kutimiza ndoto zake.