Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita Afghanistan: Watu wenye silaha wavamia harusi kuzuia muziki usipigwe
Wanaume wenye silaha ambao walijitambulisha kama Wataliban wameivamia harusi mashariki mwa Afghanistan na kutaka muziki usipigwe.
Wapiganaji hao waliuwa watu wawili na wengine 10 kujeruhiwa, maofisa wameeleza.
Msemaji wa Taliban amesema wapiganaji wawili kati ya watatu wamekamatwa lakini wamekanusha kuwa walijifanya wanatekeleza harakati za kiislamu.
Muziki ulipigwa marufuku wakati Taliban ilipoongoza mwaka 1996 mpaka mwaka 2001.
Mamlaka mpya ya Talban hayajapitisha marufuku hiyo .
Shuhuda ameiambia BBC kuwa kulikuwa na ndoa za pamoja za wapenzi wanne katika wilaya ya Surkh Rod, jimbo la Nangarhar siku ya Ijumaa.
Walipata ruhusa kutoka viongozi wa eneo hilo wa Taliban kucheza muziki katika eneo hilo ambalo lilikuwa linatumika na wanawake pekee.
Lakini majira ya usiku, wapiganaji walivamia usiku na kujaribu kuteketeza spika.
Wageni walipopinga , ndipo walipoamua kuwamiminia risasi.
Msemaji wa Taliban ,Zabihullah amesema kesi hiyo bado inafanyiwa uchunguzi.
Kundi la wanamgambo wa kiislamu-IS ambao wanapingwa na Taliban, pia wanalaumiwa eneo lingine huko Nangarhar kwa tukio kama hilo kwa siku za nyuma.
Afghanistan iliangukiwa utawala wa Taliban mwezi Augosti baada ya Marekani kuondoa majeshi yao katika nchi hiyo.
Wakati wa utawala wa awali, walikuwa wakiekeleza sheria kali za kiislamu lakini sasa kuna mabadiliko kidogo na hata wanataka kutambuliwa kimataifa.
Tangu Taliban irudi madarakani, utawala huo umekuwa ukishutumiwa kufanya mauaji ya mwanamuziki na wanamuziki wengi wamekimbia Afghanistan tayari.