Mambo matano yanayothibitisha kuwa viumbe wa kale au Neanderthals walikuwa sawa na wanadamu

Iliyochapishwa

Viumbe wa kale au Neanderthals walielezwa kama viumbe wajinga na wakatili, waliokuwa wanaishi kwenye mapango, waliopitwa na wakati na waliokaribiana na sokwe kuliko wanadamu

"Haswa walikuwa ni viumbe wenye akili sawa na binadamu. Hawakuwa kama nyani. Sio vizuri kuwa dunia kutumia neno Neanderthal kama matusi wakati huu," kulingana na makavazi ya historia nchini Uingereza.

Watu hawa waliotoweka miaka elfu arobaini iliyopita na waliokuja kutambuliwa kuwa walio katika familia ya wanadamu miaka 160 tu iliyopita, Neanderthals wamedharauliwa na sayansi kwa miongo kadhaa.

Miaka ya hivi karibuni hata hivyo, utafiti umeonyesha kuwepo mambo magumu zaidi kuhusu ndugu zetu hawa.

Hii ni mifano ya ugunduzi unaoonyesha kuwa viumbe hawa waliotoweka walikuwa wameendelea kuliko vile tunafikiri.

Viumbe wa kale au Neanderthals walielezwa kama viumbe wajinga na wakatili, waliokuwa wanaishi kwenye mapango, waliopitwa na wakati na waliokaribiana na sokwe kuliko wanadamu.

1. Mababu zetu walikutana au kuishi nao.

Wanadamu katika karne ya 19 na 20 huenda walifikiri kuwa Neanderthals walikuwa tofauti sana na binadamu wanaofahamika kama Homo sapiens, lakini badhi ya wanadamu wa zamani hawakufiria hivyo.

Neanderthals na wanadamu sio waliishi pamoja katika mabara ya Ulayana Asia lakiani pia walifanya mapenzi na kuzaa watoto pamoja.

Kulinga na utafiti wa kijenetiki kwa mabaki ya Neanderthals, Homo Sapiens mara kwa mara walifanya mapenzi na Neanderthals kwa maelfu ya maiaka. Kwa hivyo leo hii kuna watu walio na karibu asilimia 2 ya DNA ya Neanderthals.

Ikiwa haijulikani haswa ni kwa nini, baada ya kuwepo kwa miaka 350,000, sababu iliyochangia Neanderthals walitoweka.

Baadhi ya sababu zinazotajwa ni pamoja na kuwa hawakuzaana kwa haraka, kuwa wanadamu wa sasa walichukua walichokuwa wanategemea kuishi na kisha kuwaambukiza magonjwa mapya.

Wengine hudai kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yalichangia kutoweka kwao.

2. Waliweza kuwinda na kuua kutoka mbali

Kulinga na utafiti uliofanya na chuo cha London na kuchapihshwa mwaka 2019, Neanderthals walitengeneza silaha zilizokuwa na uwezo wa kuua kutoka mbali.

Katika kufikia uamuzi huu, watafiti walitumia mikuki ya miti iliyofukuliwa eneo la Schöningen, nchini Ujerumani miaka ya 1990. Mikuki hii ilikadiriwa kuwa yenye miaka 300,000.

Watafiti walifanyia majaribio uwezo wa silaha hizi ambapo walirusha mikuki wakijaribu kulenga shabaha na kugonga maeneo kutoka umbali tofauti.

Mikuki hiyo kwa ufasaha iligonga maeneo yaliyolengwa umbali wa mita 20.

Annemieke Milks, mtafiti aliyeongoza utafiri huo aliimbia BBC kuwa ugunduzi huo kwa mara nyingine ulibainisha akili ya Neanderthals.

3. Neanderthals waliwazika wafu

Moja ya maeneo maarufu zaidi walimokuwa wanaishi Neanderthals ni lile la Old man of La Chapelle-aux-Saints, lililogunduliwa mwaka 1908 ambalo lilikuwa na mabaki ya mtu mwenye ulemavu kwenye uti wa mgongo.

Wendani wa kiumbe huyi walimchimbia kaburi na kumlinda kutoka kwa wanyama, kulingana na utafiti kutoka eno hilo uliochapishwa mwaka 2014.

Lakini huu sio mfano tu wa maziko ya Neanderthal.

Kwenye pango huko Teshik-Tash nchini Uzbekistan, mtoto wa Neanderthal alipatikana amezikwa na kuzungukwa na mifupa ya mbuzi, huku eneo la Regourdou nchini Ufaransa, mifupa ilikuwa imewekwa kando ya mwili.

4. Huenda waliwatunza wazee

Wataalamu pia wanadai kuwa Neanderthals walikuwa wenye huruma kuliko ilvyodhaniwa.

Mwaka 1957 wanaakiolojia walipata mabaki ya Neanderthal yaliyokuwa na majeraha kadhaa katika pango la Shanidar nchini Iraq.

Kulingana na utafiti uliofanywa mwaka 2017 na mwananthropolojia Erik Trinkaus kutoka chuo cha Washington huko Saint-Louis na Sébastien Villottekutok kutoka kituo cha ufaransa cha utafiti wa sayansi ni kua kiumbe huyu alikuwa kisiwi.

Na licha ya ulemavu huu, aliishi hadi miaka 40.

Kulingana na wananthropolojia, ni kuwa hangeweza kuishi hadi umri huo bila msaada kutoka kwa watu wengine.

Mtu mwingine mzee kutoka eneo la La Chapelle-aux-Saints pia naye anaonekana kutunzwa na wandani wake.

Kulingana na watafiti waliochunguza eneo hilo, majeraha yake na ukosefu wa meno na umri wake mkubwa, unaonyesha alikuwa anatunzwa na jamii waliomsaidia kuishi kwa kila njia.

5. Kulikuwa pia na wasanii

Miaka 42,000 iliyopita, Neanderthals walikuwa na uwezo wa kungenza vito kutoka kwa meno ya wanyama na pembe za ndovu.

Utafiti uliochapishwa kwenye nakala ya sayansi mwaka 2018 unadai kuwa hata walichora kwenye mapango nchini Uhispania miaka 20,000 iliyopita kabla ya wanadamu wa sasa kuwasili Ulaya.

"Kulingana na maoni tangu michoro hii inafunga mjadala kuhusu Neanderthals," alisema João Zilhão, mtafiti kutoka kundi la watafiti la chuo cha Barcelona waliogundua michoro hiyo.

"Hawakuwa tofauti au hawakuwa na akili ndogo. Wao ni aina fulani ya binadamu ambao kwa sasa hawapo kabla.