Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Uganda 2021: Madai ya uongo kuhusu Joe Biden na wengine
- Author, Peter Mwai
- Nafasi, BBC Reality Check
- Iliyochapishwa
Wakati uchaguzi wa Uganda ukitarajiwa kufanyika Januari ,kumekuwa na taarifa ghushi kadhaa ambazo zimekuwa zikishirikishwa na watu wakati wa kampeni ambao umekuwa na ghasia.
Rais Yoweri Museveni, ambaye yupo madarakani tangu mwaka 1986, anakabiliana na wagombea wengine 11 , kati yao akiwemo mwanamuziki anayefahamika kama Bobi Wine.
Baadhi ya taarifa ambazo si za kweli zilizozagaa wakati wa kampeni zimekuwa katika ujumbe mfupi na video:
Joe Biden haungi mkono upinzani
Kwa mfano video ambayo imetumwa sana katika mitandao ya kijamii ikimuonesha rais mteule wa Marekani Joe Biden akitaka Bobi Wine (Robert Kyagulanyi) kuachiwa huru.
Baadhi walidai kuwa bwana Biden alikuwa anamsaidia Bobi Wine katika uchaguzi .
Mwanaume mwenye mvi akizungumza kwenye video anasema: "Wote tunajali uhuru wa dini zetu, tunasimama kwa pamoja na tuataka demokrasia nchini Uganda."
Lakini mwanaume umme huyo si Joe Biden, na video hiyo ya zamani ina miaka miwili mtandao.
Ni kundi la waganda katika maeneo mbalimbali duniani waliandamana mwaka 2018 wakati Bobi Wine aliposhikiliwa.
Tukio hilo lilikuwa mjini Boston, na mwanaume anayeongea anaitwa Nick Carter, mwanasiasa wa Democratic aliyekuwa anawania serikali ya eneo hilo.
Anasikika akizungumza kwa dakika tatu akiwa anatafuta kuungwa mkono na watu wa eneo lake.
Kikosi cha habari cha Biden kilisema: "Rais mteule hajaandika kitu chochote kwenye tweeter kuhusiana na suala hilo au uchaguzi wa Uganda.
Tweeter ambayo Biden aliandika kuhusu Ugunda ilikuwa ya mwaka 2019, kuhusu wapenzi wa jinsia moja.
Na hata Barack Obama hajajihusisha na chochote
Mwezi uliopita rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alidaiwa kuonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na #FreeBobiWine,
Lakini hakuna rekodi kuwa Obama aliandika mtandaoni siku hiyo licha ya uwepo wa screenshot inayoonesha kumuunga mkono Bobi wine na watu wapatao milioni walitweet tweet yake.
Vilevile ujumbe huo una makosa ya kisarufi katika neno la "iPhone" huwa linaanza na herufi kubwa.
Na hakuna tiki ya bluu bali nyeupe.
Alama ya tiki ya bluu inaainisha kuwa ni mtu maarufu, hivyo ujumbe huo ni wa kutengeneza tu.
Je Bobi Wine alikataa kuzungumzia masuala yake ya kisiasa?
Kuna madai kwenye mitandao ya kijamii yanayodai kuwa Bobi Wine alikwepa kuzungumzia kuwa alikuwa mbunge katika mahojiano ya kwenye redio.
"Muongozaji, sina mda wa kutosha hapa kwenye radio, niulize swali lingine," ndio jibu alitoa Bobi Wine.
Lakini kuna masuala kadhaa si ya kweli .
Picha ya radio iliyowekwa hapo ni ya kaskazini mwa Uganda 89.8 FM .
Wanasema alifanya mahojiano Kabale kusini magharibi mwa Uganda, huko kuna radio tofauti ambayo ni 100.4 Hills FM.
Ni kweli Bobi Wine alikuwa akihojiwa redioni Desemba 16, lakini alijadili suala la yeye kuwa mbunge na mambo aliyoyafanya.
"Ndio , aliulizwa swali hilo kuhusu ubunge na alijibu pia kuhusu mradi mwingine anauendesha," meneja wa radio Nick Kanyesigye alisema.
Na maofisa kutoka chama cha Bobi Wine' walithibitisha hilo BBC,na kuongeza kuwa na alimwambia mtangazaji aulize swali lingine na hicho kilikuwa kipindi pekee alikifanya Desemba 16.
Huu si mfano wa karatasi ya kupigia kura itakavyofanana
Mfano wa muonekano wa karatasi ya kupigia kura utakavyoonekana ikiwa na majina ya wagombea urais na alama za vyama vyao inasambaa katika mtandao ya kijamii.
Lakini tume ya uchaguzi imekanusha kutoa karatasi ya aina hiyo.
"Tume ya uchaguzi Uganda bado haijachapisha karatasi za uchaguzi wa urais kwa mwaka 2021. "alisema kamishina.
Karatasi hizo si za kweli na hata huwa hawatumii majina yao halisi ,picha au alama ya chama au mgombea.