Jerry Rawlings: Ni kwanini kiongozi huyo wa zamani aligawanya maoni nchini Ghana

Jerry Rawlings

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jerry Rawlings alikuwa mtoto wa mkulima na mama Mghana
Iliyochapishwa

Jerry Rawlings alinyakua mamlaka mara mbili nchini Ghana lakini akayarejesha nchini chini ya udhibiti wa demokrasia .

Baada ya jaribio la kwanza la mapinduzi alihukumiwa kifo lakini alikwepa kuipindua serikali ya nchi ya kijeshi.

Miaka miwili baadaye Rawlings alimuondoa madarakani kiongozi wa nchi aliyechaguliwa kidemokrasia halafu baadaye alifanikiwa kugombea mwenyewe katika uchaguzi.

Awali Rawlings ambaye ni mjamaa, alianzisha mageuzi ya soko huria na kuifanya nchi yake kuwa muhusika mkuu katika ujumbe wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa .

Je Jerry Rawlings ni nani?

Jerry John Rawlings alizaliwa Accra Juni 22 mwaka 1947, mtoto wa kiume wa Mkulima Mskochi na mama Mghana.

Alisomea katika shule ya sekondari ya Achimota ambako alifanya vizuri katika uwanja wa mashindano ya farasi na alielezewa na wanafunzi wenzake kama mzungumzaji asiyeogopa kutoa mawazo yake na mwenye uasi.

Mwaka 1968 alijiunga na shule ya mafunzo ya kijeshi ya Teshie, karibu na mji mkuu Accra, na baadaye alipelekwa katika shule ya uendeshaji wa ndege.

Akiwa na cheo cha Luteni wa pili, alipata mbawa na kujiunga na kikosi cha wasomi - Fourth Squadron cha ndege za jet za wapiganaji chenye makao yake mjini Accra.

Gerry Rawlings addresses supporters in 1982

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Akihutubia vikosi vya la baraza jeshiu katika mkutano karibu na Accra

Wakati Rawlings alipopandishwa cheo kuwa Luteni wa ndege 1978, alikuwa tayari ameanza siasa.

Ghana, nchi ambayo ilikuwa ya kwanza Afrika kupata uhuru wake kutoka kwa Uingereza, ilikuwa inakabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula, hasara na mkwamo wa uchumi .

Rawlings alielekeza hasira zake kwa kile alichokiona kama ukosefu wa nidhamu, ufisadi na matumizi mabaya ya utawala wa kijeshi.

Wakati marufuku ya vyama vya kisiasa ilipoondolewa mwaka 1979, Rawlings alipata umaarufu mkubwa kama mtu mkosoaji maarufu wa serikali , aliitolea wito ifanye juhudi zaidi kuwasaidia masikini.

Akisukumwa na uungaji mkono huu, Rawlings alifanya jaribio lake la mapinduzi la Mei 1979. Halikufanikiwa na akakamatwa na kuhukumiwa kifo .

Jaji aliuawa

Alifanikiwa kutoroka jela kwa kusaidiwa na maafisa wa ngazi ya chini na vyeo vingine na kumpindua kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, Jenerali Fred Akuffo.

Rawlings alichukua utawala wa serikali kama kiongozi wa Baraza la kijeshi la mapinduzi (AFRC), na kusababisha kuandikwa kwa kichwa cha habari katika gazeti la Uingereza kitakachokumbukwa : " Chotara Mskochi na mchezaji wa mchezo wa farasi aichukua Ghana".

AFRC lilikua limeapa kuwawajibisha viongozi wa zamani, na Akuffo na viongozi wengine wa kijeshi walinyongwa.

mabango mwaka 1996

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alishinda kwa wingi wa kura katika chaguzi mbili za urais

Rawlings alianzisha kile alichokiita zoezi la utunzaji wa nyumba '' housekeeping exercise" kuiondoa Ghana katika kile AFRC walichokielewa kuwa ni vitendo vya ufisadi wa utawala wa kijeshi.

Majaji wa ngazi ya juu kadhaa na maafisa wa jeshi waliuawa katika kipindi hicho.

Lakini, mbali na kung'ang'ania katika madaraka mapya aliyoyapata, Rawlings aliitisha uchaguzi katika kipindi cha miezi minne ya mapinduzi yake.

Chama kipya kilichopendwa cha People's National Party, kilichoongozwa na Hilla Limann, kiliingia madarakani.

Ukali

Hatahivyo , Limann aliangaliwa na wengi kama mtu tu anayetumiwa na Rawlings na kushindwa kwake kufanya mageuzi ya uchumi wa Ghana haraka kulimfanya aondoke madarakani.

Kutokana na kuongezeka kwa madeni ya kigeni na mfumuko wa bei kwa 140%, kutoridhika kwa umma kuligeuka kuwa machafuko.

Na tarehe 31 Disembar 1981, Rawlings aliingilia kati kwa mara ya pili, akafanya mapinduzi yaliyoileta serikali mpya, Baraza la Provisional National Defence Council (PNDC), likaingia madarakani.

PNDC, kikiongozwa na Rawlings kilitaka kuibadili Ghana kuwa taifa lenye utawala wa Kimarxist.

Malkia Elizabeth na Jerry Rawlings wakati malkia hyo alipotembelea Ghana 1999

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia Elizabeth na Jerry Rawlings wakati malkia hyo alipotembelea Ghana 1999

Ilianzisha mabaraza ya wafanyakazi kwa ajili ya kusimamia viwanda vya nchi, kamati za ulinzi za wafanyakazi zikaibuka katika kila jamii, na Rawlings akageukia kwa muungano wa Usovieti kuomba msaada.

Lakini miaka miwili tu katika jaribio lake ndani ya ujamaa, Ghana iliuacha.

Labda kwa kuhisi kwamba Muungano wa Usovieti ulikuwa karibu kuvunjika , Rawlings alichukua hatua za kukumbatia soko huria.

Alishusha thamani ya sarafu, akaacha kuwaajiri wafanyakazi katika makampuni ya serikali na kutaifisha viwanda vya Ghana, ikiliwa ni pamoja na mashamba yake muhimu ya kahawa na kakao.

Ushindi wa wa kishindo.

Lakini, ingawa mabadiliko haya yalizifurahisha nchi za magharibi pamoja na Mfuko wa fedha duniani(IMF), makali yaliyoambatana na mageuzi hayo yalisababisha machafuko ndani ya nchi.

Kati ya mwaka 1983 na 1987, Rawlings alinusurika majaribio manne dhidi yake. Kamata kamata ya serikali, ambapo viongozi wa upinzani walikamatwa na kufungwa, ililalamikiwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kote duniani.

Hali ilikuwa mbaya hata zaidi wakati Waghana milioni walipofukuzwa kutoka nchi jirani ya Nigeria.

Lakini, kufikia miaka ya mapema ya 1990, mageuzi yake yalikuwa yameiongoza nchi kuelekea katika uchumi imara na mwaka 1992, Rawlings akashinda uchaguzi wa rais wa Ghana.

Jerry Rawlings na aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi 1987

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jerry Rawlings na aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi 1987

Ushindi wake wa kishindo, akiwa na asilimia 58% ya kura, uliaminiwa kuwa ulikuwa ni wa haki na Jumuiya ya Madola na Umoja wa Afrika.

Na kutokana hasa na nchi kuwa na uthabiti mpya wa kiuchumi , alichaguliwa tena katika ushindi mwingine wa kishindo mwaka 1996.

Aliinua sura ya Ghana kimataifa kwa kuchangia wanajeshi wengi katika vikosi vya Umoja wa Mataifa na walinda amani, hususan katika mataifa ya Liberia, Sierra Leone, Lebanon na Iraq.