Virusi vya corona: Dawa bandia zashehena Afrika Magharibi

Iliyochapishwa

Uuzaji wa dawa bandia ni biashara inayoendelea kushamiri Afrika Magharibi, huku taasisi za sheria zikijitahidi kukabiliana na magenge ya uhalifu ya kigeni yenye kuhusishwa na biashara hiyo, ameandika Emma Hooper.

Ni nadra sana nchini Nigeria kuwa na mazungumzo kuhusu tatizo la dawa bandia bila kutaja janga lililosababishwa na dawa ya watoto ya kunywa ya 'My Pikin.'

Mwaka 2009, watoto 84 waliuawa kwa dawa iliyosemekana kutibu matatizo ya meno iliyokuwa imechanganywa na diethylene glycol, kiyeyusho kinachotengenezwa viwandani na hupatikana ndani ya kimiminika au maji maji yanayotumiwa kupunguza mgando.

Wafanyakazi wawili wa kampuni hiyo waliotengeneza dawa hiyo ya kunywa walipatikana na hatia.

'Dawa mbaya'

Bado utengenezaji au uuzaji dawa bandia unaendelea sana Nigeria.

"Suala hilo ni miongoni mwa yaliyokuwa gumzo," Dkt Alero Roberts amesema, na kuongeza: "Tumekuwa na matatizo kadhaa."

Dkt. Roberts, mhariri mwandamizi katika chuo cha hospitali cha Lago, ana bahati kwasababu hospitali hiyo ina mfumo mzuri wa uagizaji dawa na haina tatizo la dawa bandia, ingawa wanakutana na wagonjwa ambao wametumia dawa bandia.

Ana hofia kwamba usambaaji wa dawa bandia huenda ukaongezeka nchini Nigeria kwasababu ya athari ya ugonjwa wa Covid-19.

"Aidha, kuna uwezekano mkubwa wa upungufu wa dawa za saratani, ," Dkt. Roberts amesema.

Maduka ya kuuza dawa hospitalini yakiwa na upugufu, wagonjwa watanunua dawa kwengineko hata kutoka maduka ambayo hayajaidhinishwa na mamlaka.

Na hawaitaji kwenda mbali, nje tu ya dirisha la hospitali yake, Dkt Roberts anaona wauzaji wa vitu viwili 'dawa na majeneza'.

Wachuuzi wa dawa ni jambo la kawaida Afrika Magharibi - ambapo nchi nyingi eneo hilo, uuzaji wa dawa ni kibiashara zaidi kuliko taaluma.

Ukosefu wa usimamizi wa mamlaka ni moja ya sababu eneo hilo lina shuhudia uhalifu mwingi katika biashara ya uuzaji wa dawa bandia. Na Afrika Magharibi hii ni biashara kubwa.

Siku za hivi karibuni, wahalifu wamefanya Idara ya Haki Miliki katika kitengo cha huduma kwa wateja kinachosimamiwa na Mohammed Babandede, kuwa na shughuli nyingi wakati ambapo janga la corona limetengeneza mwanya wa biashara ya dawa bandia kuongezeka.

"Inaogopesha sana," anasema, na kuongeza kwamba kwa kipindi cha wiki moja, zaidi ya dawa milioni 30 bandia zimekamatwa.

Anaelezea kwamba mamlaka nchini India imetoa kikosi chao cha ujasusi kwa meli iliyokuwa inaelekea bandari ya kisiwa cha Tin Can mjini Lagos, mji mkuu wa manunuzi.

Mitandao yenye nguvu

Shehena hiyo ilijumuisha dawa nyingi tu bandia za dexamethasone - dawa inayoaminika kutibu dalili kali za ugonjwa wa Covid-19.

Wiki hiyo hiyo, idara hiyo ilikamta dawa bandia za tramadol, 920,000 katika bandari ya Lagos ambazo baadhi yao zilikuwa zimetoka India mji wa Mumbai.

Kuna uwezekano mkubwa dawa hizo zilikuwa zinapelekwa katika masoko ya kaskazini wa Nigeria ambako matumizi mabaya ya dawa ni jambo la kawaida.

Bwana Mohammed amesema kwamba kukamatwa kwa washukiwa halikuwa jambo rahisi kwasababu mara nyingi shehena hizo huwa zimesafirishwa kwa anwani bandia zilikotoka na zinakoelekea - hiyo inamaanisha kwamba mamlaka haiwezi kutambua chanzo chake.

Nchini Nigeria ambapo watu wamekatwa, mara nyingi mitandao hiyo huwa na nguvu kiasi kwamba ni nadra sana wahusika kushitakiwa - mawakili wazuri ndio wanaosimamia kesi hizo wakitafuta washukiwa kuachiliwa kwa dhamana au wakitafuta namna kesi hizo zinavyoweza kuahirishwa kwa miaka mingi.

Adebayo Alonge anafahamu fika jinsi makundi haya yalivyo hatari. Yeye wenyewe akiwa mwathiriwa wa dawa bandia, Bwana Alonge alinunua dawa ya salbutamol mwaka 2003 kutoka duka la kuuza dawa huko Ibadan kusini magharibi.

Dawa hizo zilikuwa zimebandikwa vibandiko vyenye majina bandia na zilikuwa zimechanganya na dawa aina ya diazepam inayotumika kwa matumizi kadhaa kama vile kupoteza fahamu kabla ya mgonjwa kufanyiwa oparesheni, ambayo ilimsababishia yeye kupoteza fahamu kabisa kwa wiki tatu.

Kile alichopitia kilimfanya kuanzisha kampuni ya RxAll, ambayo inatumia teknolojia kubaini ubora wa dawa aliyopendekezewa mgonjwa.

Mwaka jana alianza kupokea vitisho vya kuuawa kwa kazi yake anayofanya.

"Hatutaacha kufanya tunachofanya - nilishawahi kufa tayari, na hivyo basi siogopi kufa tena," alisema.

Katika maghala madogo madogo yaliyopo sehemu mbalimbali za miji ya nchi za Afrika Magharibi, kuna watu waliojificha humo ambao biashara yao ni kufungasha tena dawa.

Pia huenda ikawa miongoni mwa shuhuli zao ni kubadilisha tarehe sahihi ya bidhaa kuharibika au kutengeneza bidhaa kuanzia mwanzo licha ya kwamba mhusika hana taalamu stahiki.

Wakati mwingine, maghala hayo huvamiwa na mamlaka na bidhaa kuharibiwa lakini mitandao iliyopo ya makundi hayo na jinsi wanavyoendesha shughuli zao, inaaanisha haitachukua muda mrefu kuanza tena shughuli zao kwengineko.

Shehena za dawa bandia hubandika vibandiko vya 'msaada wa kibinadamu'

Mbinu zinazotumiwa na wanahalifu zinazidi kuchanganya.

"Wanaendelea kuwa na busara katika ubunifu wao, ukizuia njia moja wanayotumia, bila shaka watatafuta njia mbadala. Hii ndio sababu hili limekuwa tatizo kubwa Afrika Magharibi na Nigeria kwa ujumla," jambo linalompa wasiwasi Bwana Mohammed.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Dawa za Kulevya na Uhalifu na Mashirika baina ya serikali Duniani limetenga idara maalum kusaidia majimbo ya eneo kukabiliana mitandao ya uhalifu.

Bob Van den Berghe, mtaalamu wa sheria ambaye ambaye yuko kwenye idara hiyo, amesema kwamba kilogramu 81 za dawa katika shehena lililoandikwa jina la 'makasha ya misaada ya kibinadamu' ilinaswa katika bandari ya Afrika Magharibi mapema mwaka huu.

Shehena hiyo ilikuwa inatoka Ufaransa lakini maafisa wamebaini dawa bandia katika makontena yanayotoka nchi mbalimbali ikiwemo Brazil na Uswizi, amesema.

Idara hiyo iliripoti kwamba kiwango kikubwa cha dawa zilizonaswa ilikuwa katika bandari za mji wa Lomé huko Togo na Cotonou huko Benin.

Kontena ambazo hupita uchunguzi wa bandarini kufunguliwa na kusambazwa kwa kiwango kidogo kidogo katika nchi za Burkina Faso, Ghana, Ivory Coast, na maeneo mengine ya mashariki mwa Nigeria, utafiti umeonesha.

Suala la uhai au kifo

"Tunaimarisha oparesheni yetu, tukiangazia zaidi maeneo ya mpakani kukabiliana na uhalifu huu," Bwana Van den Berghe amesema.

Huku vifo 116,000 vikikadiriwa kutokea kila mwaka ambavyo chanzo chake ni dawa bandia za ugonjwa wa malaria katika eneo la jangwa la Sahara pekee, oparesheni hizi huenda ikawa suala la uhai au kifo.

Hata hivyo, wataalamu wanaonya kwamba ikiwa vita hivi dhidi ya dawa bandia ni vipate ushindi, juhudi zaidi zinastahili kufanywa kuhakikisha huduma bora ya afya inapatikana kwa wote.

"Bila shaka mapungufu ya mifumo ya afya kulikojitokeza baada ya kutokea kwa ugonjwa wa Covid-19, kutafanya serikali kuweka kipaumbele kuhakikisha kila raia anapata dawa salama na kwa gharama nafuu", amesema Dkt Gernot Klantschnig, mhariri mwandamizi katika somo la Uhalifu wa Kimataifa chuo kikuu cha Bristol Uingereza.