Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vazi ambalo hutangazwa kuwasili kwake katika mitindo
Mpiga picha wa NigeriaOye Diran amepiga picha za mitindo ya mavazi ya jamii ya Yoruba .
Jinsi mitindo hii inavyokuja na kuondoka, Oye Diran anaonyesha picha za zamani za familia, Alikuwa anavutiwa na maonyesho ya mitindo ya mavazi ya wanawake wa Yoruba kutoka Magharibi mwa Afrika katika miaka ya 1960s, 1970s na 1980s.
Picha ya mama yake na dada zake wakiwa wamevalia mavazi ya kuvutia kwa rangi .
Mavazi hayo ya asili asili ni sketi ya kufunga, kitambaa cha kichwa cha kufunga na blauzi kubwa ambayo ni maarufu kwa wanawake wa Yoruba nchini Nigeria.
Diran, ambaye asili yake ni Yoruba, ni mpiga picha wa nchini Nigeria anayeishi New York, amegundua kuwa mtindo wa uvaaji wa mavazi yaayofahamika kama 'iro na buba' yamekuwa yakibadilika kila mara , licha ya kwamba umaarufu wa vazi hilo bado upo.
Amekuwa akivutiwa na mavazi hayo na wakati anaangalia mtandaoni kutafuta nguo za aina hiyo alisikitishwa na kile alichokiona.
"Nilichokuta katika mtandao ni nguo hizo za asili zilkiwa zimeboreshwa kisasa zaidi na sio kile ambacho nilikuwa nakihitaji," aliiambia BBC.
Hivyo akachukua kamera na kutengenez picha kadhaa za mavazi hayo na kuziita ' A Ti De' (Tumewasili).
Wayoruba ni kabila la pili kwa ukubwa nchini Nigeria ambalo linafahamika kwa kupenda sherehe za shamrashamra nyingi na sherehe za kila wakati - sherehe za kitu chochote kutoka kwa mtoto mpya mpaka kufugua nyuma mpya huwa kuna mkusanyiko mkubwa wa marafiki na familia wakiwa na wameandaa chakula na vinywaji pamoja na kufungulia muziki.
Kitu kinachovutia zaidi katika mikusanyiko hii haswa kwenye harusi ni rangi za nguo ambazo wageni wamevaa.
Kwa wanawake huwa wanavaa vazi la iro na buba , vazi ambalo miaka ya nyuma walikuwa wanavalia katika shughuli maalumu.
Lakini enzi hizo zimepita muda mrefu sasa na mavazi hayo yamechukuliwa na vazi la e aso-ebi, wakati wageni wa sherehe wanapovaa, huwa zina muonekeano wa sare kwa wote.
Hii ni ishara ya namna gani mambo yamebadilika, vazi la aso-ebi halihifadhiwi tena kwenye sanduku kusubiri shughuli maalum kuvaliwa, sasa hivi vazi hilo sio muhimu tena kusubiri siku maalum bali linavaliwa tu kipindi mtu atakapojisikia.
"Mitindo ya Yoruba imekuwa ikibadilika kwa miongo kadhaa lakini muonekano wake huwa ni uleule ," Diran aliiambia BBC.
"Nahisi kama tumeanza kuona mitindo mipya ya mavazi haya kuanzia miaka ya 2000s mpaka leo hii.
"Kwa mfano, mwaka 1960s urefu wa nguo ya iro ilikuwa chini ya magoti.
Lakini leo hii urefu wa vazi la iro linaweza kuwa mbali kutokea kwenye miguu.Tunaona mitindo ya mavazi mingine duniani yanabadili mitindo ya Yoruba ," alisema.
Diran, ambaye ni mchoraji na mpiga picha wa mitindo alizaliwa nchini Nigeria katika mji wa kibiashara wa Lagos, na mama yake alikuwa msanii wa picha na baba yake alikuwa daktari wa wanyama na mfanyabiashara.
"Mama yangu alikuwa na studio ya kuchora picha, nilivyokuwa mdogo nilikuwa naona kazi zake, alikuwa anachanganya kazi za picha, kuchora, kupaka rangi na kupiga picha.
"Nimekuwa nikiwa navutiwa na sanaa."
Anapenda kuweka picha za asilia na zenye rangi za kung'aa.
"Katika picha zake alikuwa anajaribu kuwasilisha urembo, nguvu na mtazamo ," alisema.
Mitindo ya Yoruba ambayo imepata umaarufu mkubwa ni blausi kuwa na mikono mikubwa na shingo ya duara.
Wamekuwa wakitumia kitambaa aina ya chiffon mpaka organza na kwa sasa mavazi hayo yamekuwa yakivaliwa kiasili yamekuwa yakifungwa kabisa.
"Vazi la Ti Deni ni vazi linalotaka kuonyesha kujiamini," alisema.
"Lilikuwa linatangazwa siku linapowasili mara nyingi ."
Kwa watu wanaopenda sherehe, maneno hayo yamezungumzwa katika nguo zao za yoruba.
All images subject to copyright