Video feki zinazosambaa mtandaoni kuhusu maandamano Marekani

Man uses his phone to record events ahead of him. Burning cars in the background.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Kifo cha mmarekani mweusi George Floyd wa mjini Minneapolis aliyekabwa na polisi na kusambabisha maandamano kote nchini Marekani na hata mataifa mengine duniani yamesababisha video za uongo.

Katika maandamano hayo kuna video na picha za kutengeneza ambazo zimeenea katika mitandao ya kijamii.Lakini baadhi ya hizi picha si za kweli au haziwasilishi ukweli wa ghasia ambazo zinaendelea kama wanavyosema.

Kitengo cha BBC cha kuchunguza ukweli wa taarifa , kimebaini kuwa video ambazo zimekuwa zikisambaa mtandaoni kwa kudai kuwa ni uhalisia wakati si kweli.Na hiki ndicho tulikibaini katika mitandao ya kijamii na vyema taarifa ipi ya kuiamini na taarifa zipi za kutoziamini.

Video inayoonyesha matofali ilichunguzwa

Tetesi zinazosambaa mitandaoni kuhusu matofali kupangwa katika maandamano za kweli.

Video kadhaa inaonyesha kuwa kuna matofali ambayo yanadaiwa kuwekwa na polisi au serikali imeagaliwa na mamilioni ya watu.

Montage of screenshots about misleading "brick" videos

Chanzo cha picha, Getty Images

Taarifa nyingine ya uzushi inayolaumu Antifa - kikundi cha mlengo wa rais Trump kushutumiwa kuhamasisha ghasia.

Hata hivyo hakuna ushahidi mpaka sasa kuonyesha kuwa kuna waandamaji ambao wametumwa kufanya ghasia hizo .

Video nyingi na picha tunazoziona hazionyeshi eneo husika, ni kawaida kwa matofali kuwa karibu na jengo linalojengwa.

Video hiyo ya matofali, utafiti umebaini kuwa ni namna ya kuwatoa watu kuona maandamano yanayoendelea, Polisi wa San Francisco aliandika katika kurasa yake ya Twitter kuwa matofali yale yalikuwepo kwa ajili ya ujenzi na tayari wamewasiliana na mhandisi kuyaondoa.

Polisi mmoja wa idara ya Boston alipinga taarifa hizo feki kuhusu video ambayo inamuonyesha afisa wa polisi akitoa matofali kwenye gari.

Maoni ambayo yameandikwa katika mitandao ya kijamii yanaeleza kuwa polisi wanatoa matofali kwenye magari ili kutumia kwa ajili ya kuomba radhi dhidi ya waandamanaji.

Hata hivyo Chuo kikuu cha Boston katika idara ya polisi kimeandika kwenye ukurasa wa tweeter kuwa polisi walikuwa wanayakusanya matofali yale kwasababu yalikuwa yameharibika na walitaka kuyarudisha katika kituo.

Video nyingine kutoka Fayetteville, North Carolina ambayo iliangaliwa na mamilioni ya watu inaonyesha matofali yamepangwa karibu na waandamanaji na mwanaume mmoja anasema hakuna ujenzi hapa.

Tumechunguza picha hizo za Mei 24, na kubaini kuwa zilikuwepo muda mrefu kabla ya maandamano kuanza.

Instagram posts showing images of bricks in Hong Kong - labelled "misleading"

Picha nyingine za zamani za maandamano katika maeneo mengine kama ya mwaka jana ya Hong Kong zimekuwa zikitumika.

Video za zamani

Utafiti umeona picha ambazo ni za kweli lakini zilipigwa zamani na matukio hayo ni ya zamani, hazina uhusiano na maandamano haya ya sasa licha ya kwamba zimekuwa zikitumika kuelezea hayo.

Miongoni mwa video za kweli kabisa za kukatwa kwa watu weusi ambazo zimesamaa hivi karibuni. Video hiyo inayoonyesha polisi wamemkamata na kumuachia huru baada ya kuona kitambulisho chake.

Screenshot of video showing two white policemen arresting a black man. The Twitter post above it says: "FBI Agent of South Sudan heritage ... being Racially Profiled ... See What happened after his arrest & what they did after they found out who he his ..."

Maelezo ya picha hiyo yanasema mtu huyo ni mfanyakazi wa shirika la kijasusi FBI na imeangaliwa na watu zaidi ya milioni 4 kwenye Tweeter. Madai hayo yameandikwa pia kwenye mtandao wa Facebook na Instagram na kuangaliwa na watu wengi zaidi.

Majibu ya Rochester Minnesota kutoka idara ya polisiy amefafanua kuwa mwanaume huyo sio mpelelezi wa FBI. Na tukio hilo lilitokea mwezi Juni mwaka jana, ambapo kwa bahati mbaya alikamatwa kwa kudhaniwa mtu mwingine anayetafutwa.

Video ya kwanza kuwekwa mwaka jana haikueleza kuwa mtu huyo ni wakala wa FBI.

Video inayoonyesha tukio la mwaka jana

Video ya kijana aliyekuwa ananyanyaswa na afisa polisi wakati anakamatwa iliangaliwa na wa watu zaidi ya milioni 10 kwa siku kadhaa zilizopita.

Screenshot of a Tweet showing a video from April of a boy being arrested. The Tweet is misleading and says it involves a girl and does not indicate that the incident happened before the current wave of protests

Tukio hilo lilitokea mwezi Aprili - huko Rancho Cordova, katika mji wa Northern California.

Haiko wazi taarifa hii ilikuwa ilishirikishwa tena aidi ya mara 100,000 . Na vilevile mhanga ametajwa kuwa msichana wakati ni mvulana.

Maandamano ya sasa, kuna video ya waandamanaji inayotoa madai unyanyasaji wa polisi katika kukamata watu weusi kikatili.

Video kutoka Marekani inaonyesha polisi wakirusha mabomu ya machozi kwa waandamanaji na wandishi wa habari inaonekana wanaonekana kuwa na hasira.

Ni mwaka tofauti na nchi siyo ya kweli

Video inayoonyesha polisi wa Marekani wakiwasha moto iliyowekwa Mei 28, sio ya kweli.

Screenshot of a Tweet falsely claiming that the video shows a US police precinct on fire. We labelled it "old video".

Video hii sio ya zamani tu bali tukio hilo lilitokea nyingine.Mlipuko huu wa moto ni kutoka mji wa China.

Sasa kwa nini watu wanashirikisha video za zamani?

"Video kama hii inaweza kuchochea hisia za hasira kwa watu na kusababisha ghasia zaidi na mgawanyiko," alisema Marianna Spring, BBC mwandishi wa mitandao ya kijamii na mtaalamu wa taarifa za uzushi.

Unaweza pia kusoma:

Nadharia za uongo

Madai kuhusu aliye nyuma ya maandamano yamechapishwa mtandaoni.

Baadhi wanadai kuwa madai hayo ni ya uongo.

Kwanza video hiyo kusambaa kuhusu George Soros.

Baadhi ya washawishi na tajiri mkubwa wa Marekani amefadhili vurugu hizi za maandamano.

Wafuasiw QAnon - kuhusu nadharia ya uongo kuwa taifa lina siri kubwa kati ya polisi na Donald Trump - madai hayo yametajwa pia.

Taarifa nyingine mtandaoni zimekuwa zikidai kuwa bwana Soros amelipa watu kuandamana.

Screenshot of a meme about George Soros

Bwana Soros, katika taasisi yake ya jamii ya 'Open Society' imetoa ufadhili kuunga mkono makundi ya kijamii kuendeleza harakati hizo duniani.

Taasisi yake ilijibu tuhuma za mwisho zilizoandikwa kwenye tweeter hivi karibuni na kusema "Bwana Soros na taasisi yake inapinga vurugu zinazoendelea na hawawezi kulipa watu kufanya maandamano".

Tetesi kuhusu mataifa ya kigeni

Madai ya mtandaoni yanayodai kuwa Urusi inahusika kwa kuibuka kwa maandamano hayo.

Taarifa zilizoandikwa na maelfu ya watu zikidai kuwa Urusi imehusika kwa kifo cha George Floyd - ikiwa ni sehemu ya operesheni za kijeshi. Hakuna ushaidi wa kuthibitisha madai hayo.

Screenshot of Tweet claiming Russia is behind the US protests. Labelled "no evidence"

Maandamano haya sio mpango wa Urusi wala taifa lingine lolote - sio vyombo vya habari vya taifa au akaunti feki za mitandao - zinahusika na uzushi huu unaoshtua mtandaoni.

Utafiti kuhusu Urusi kuhusika katika uchaguzi wa rais wa Marekani kwa mwaka 2016 uliobaini kuwa Urusi ilihusika kufanya kampeni za uongo na kuweka kampeni za uongo za makundi ya wana harakati wa Marekanui na kuhusisha harakati za 'Black Lives Matter'.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Kifo cha Floyd: Wamarekani weusi wasema 'hawako salama'
Presentational grey line