Virusi vya Corona: Maeneo mapya yapata maambukizi, huku idadi ya visa ikipanda Kenya

Iliyochapishwa

Watu 25 zaidi wamepatikana vna virusi vya corona, na kulifanya taifa la Kenya kuwa na jumla ya visa vya maambukizi 912, Kulingana na taarifa iliyotolewa na Katibu tawala wa waziri wa Afya Rashid Aman Jumatatu.

23 kati yao ni wanaume, huku waili wakiwa ni wanawake. Umri wao ni kati ya miaka 22 na miaka 50

23 kati ya visa vipya vya maambukizi ya Covid-19 ni raia wa Kenya, huku 2 wakiwa ni raia wa Wasomali.

kaunti za Taita Taveta, Garissa na Meru ni maeneo ya hivi karibuni kurekodi visa vyake vya kwanza vya virusi vya corona. Taveta ina wagonjwa 2, Garissa 2 na Meru 1.

Dkt Aman amesema kuwa sampuni 44,851 ndizo zilizokwishapimwa hadi sasa.

Mpango unaolengwa kwa sasa ni kuwapima watu wengi.''Tumepokea vifaa vya kupima ndio maana tumeongeza shughuli ya upimaji'', amesema.

Madereva wa malori

Dkt Aman amesema kwamba madereva wa malori 53 tayari wamepimwa virusi vya corona na kupatikana na maambukizi kwenye mipaka ya Kenya na Tanzania, ambapo 51 kati yao walikua ni raia wa Tanzania na 2 raia wa Burundi.

Wote walirejeshwa nchi kwao.

Dkt Aman amesema kuwa mipango sasa inaendelea ya kuweka maabara katika mpaka wa Namanga ili kuharakisha upimaji na kutoa matokeo.

" Vituo vya mpaka ni muhimu. Tuna uwezo wa kupima katika mpaka wa Uganda. Tatizo lipo kwenye mpaka wetu na Tanzania na kupata majibu ya vipimo inachukua muda'', amesema.

Kenya ilifunga mipaka na majirani zake

Wiki iliyopita Kenya ilitangaza kufunga mpaka kwa muda wa siku 30 mipaka yake ya kimataifa kwenda Tanzania na Somalia Jumamosi Mei 16.Katika hotuba yake kwa taifa Rais Uhuru Kenyatta alisema hatua hiyo inajumuisha udhibiti usafiri wa watu kutoka mataifa hayo kuingia nchini Kenya.

Hatahivyo usafirishaji wa mizigo unaendelea kati ya Kenya na mataifa hayo mawili.

Na kwa upande wa Somalia masharti ni hayo hayo, mizigo peke yake ndio itaruhusiwa.

Aidha madereva watakaoingia nchini Kenya kuleta mizigo watatakiwa kupima corona kwanza.

Kenya ilimeongeza tena muda wa marufuku ya kutoka nje kwa muda wa siku 21.

Hatua za kudhibiti matembezi pia zimeendelea kuimarishwa Kenya

Rais Kenyatta alirefusha zaidi kipindi cha kudhibiti matembezi ya watu ili kudhibiti maambukizi zaidi ya virusi vya corona.

Wiki iliyopita aliongeza muda wa watu kutoka nje wa kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi hadi Juni 6,2020.

''Najua Wengi wanataka maisha yarudi kama vile ilikuwa lakini wenzagu sitaki niwadanganye. Jukumu la kwanza la serikali ni kulinda maisha ya Wakenya'', alisema.

Marufuku ya usafiri kuingia na kutoka miji mitano ikiwemo Nairobi, pia iliongezwa kwa siku 21.

Unaweza pia kutazama: