Virusi vya corona: Muuguzi wa Kenya asimulia alivyotengwa kwa kuwahudumia wagonjwa wa corona

Chanzo cha picha, Eunice Mwabili
Muuguzi mmoja nchini Kenya alijikuta akiwa ananyanyapaliwa na kunyanyaswa baada ya kumuhudumia mgonjwa wa coorona wakati alipokuwa katika zamu ya usiku.
Eunice Mwabili anasema kuwa alikuwa akimuhudumia kitaaluma - alikuwa amevalia vifaa vyote vya kujikinga wakati akimuhudumia mgonjwa huyo ambaye alikuwa amewekwa katika chumba cha kilichotengwa katika hospitali hiyo.
Ilipofika asubuhi, marafiki zake na majirani walianza kumkwepa na kumuogopa kwa kuhisi labda alikuwa amepata maambukizi ya virusi vya corona.
Haijajulikana nani alitoa taarifa hizo kuwa alikuwa anamuhudumia mgonjwa wa corona - lakini jina lake na namba yake zilikuwa kwenye mitandao ya kijamii.
Mgonjwa huyo alipona lakini taarifa hazikuwa zimepotea - tayari kuna athari kubwa imetokea dhidi yake.
Alianza kupokea simu kutoka kwa watu asiowafahamu-baadhi wakiwa wanataka kujua ni wapi anafanyia kazi na marafiki zake walitakakujua hali yake ya kiafya.
"Huko nje ninaonekana kama nina corona tayari. iliniathiri sana. Taarifa hiyo ilikuwa hata kwenye vyombo vya habari. Ilionyeshwa kwenye TV," bi. Mwabili aliiambia BBC.
Jirani yake mmoja alimuita kwa kelele na kumwambia: "Nasikia umepata corona kwa sababu ulikuwa unamuhudumia mgonjwa wa corona."
Mtu huyo alimwambia mume wake kuwa ananionea huruma "kwa sababu ya kile kilichotokea kwa mke wake".
"Unaweza kuamini mpaka leo, rafiki yangu huyo hajanipigia kutaka kujua ninaendeleaje baada ya lile tukio," alisema.

Chanzo cha picha, Kenyan Ministry of Health
Si peke yake ambaye anakutana na unyanyapaa kutokana na virusi vya corona nchini Kenya.
Hata baadhi ya waliopona wanaona kuwa inawawia vigumu.
Hata wale ambao wamepona corona imewawia vigumu kukubalika kwa jamii zao.
Hivi karibuni waziri wa afya Mutahi Kagwe alizungumzia kuhusu mtu ambaye alikuwa amepona kabisa na corona lakini hakuruhusiwa kurudi kwenye kwaya aliyokuwa anaimba.
Waziri anasema kuwa wagonjwa wanapotoka hospitalini huwa wanakumbana na unyanyapaa kwa kiwango kikubwa.
Unyanyasaji mtandaoni
Mtandao wa kijamii unasababisha hofu.
Mwanaume mmoja niliwasiliana naye ili aeleze maisha ya karantini yakoje na akakataa kujibu akiwa na hofu ya kunyanyapaliwa mtandaoni baada ya taarifa kutoka.
Aliwahi kuwekwa karantini kwa muda wa siku 14 kama hatua ya kuhakiki kuwa hana maambukizi maana kuna baadhi ya watu katika gorofa lao walikutwa na virusi vya corona lakini yeye hakuwa amepata virusi hivyo.

Pia unaweza kutazama:

Hata kabla ya taifa hilo kutangaza mgonjwa wa kwanza mwenye maaambukizi ya corona, kwenye mitandao wa kijamii wa Facebook ujumbe wa kibaguzi kutoka kwa mbunge aliyekuwa anawataka watu kukaa mbali na raia kutoka China eneo ambalo corona ilianzia, ulisambaa.
Mwezi Aprili, Brenda Cherotich, alikuwa miongoni mwa wagonjwa wa corona ambaye alipona na kuhojiwa katika televisheni kuhusu hali yake.
Maofisa walitaka atoe ushuhuda wa kuleta matumaini, kuonyesha kuwa ukiumwa corona si lazima ufe unaweza kuokoka- lakini badala yake alikutana na unyanyasaji dhidi yake.
Si muda mrefu, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 27-anayeishi pwani ya Mombasa "ilidaiwa kuwa alikufa baada ya kukwepwa na wahudumu wa afya" kwa kuhofiwa kuwa na corona, baba yake aliliambia gazeti la 'The People Daily'.
'Nilikuwa naogopa kutoka nje'
Kwa mhudumu wa afya kama bi. Mwabili, unyanyapaa dhidi yake ulianza wakati Davis Muturi alipofika katika hospitali hiyo ya kanisa katoliki ambayo nesi huyo anafanya kazi mwishoni mwa mwezi Machi.
Mwanaume huyo mwenye miaka 40 alikuwa amerudi kutoka Marekani, wiki moja kabla.
Alienda kujitenga na kuiomba familia yake kuchukua tahadhari kwa kuhamia kwa ndugu kwa muda.
"Nilikuwa na mtoto mdogo wa mwezi mmoja ambaye nilikuwa sijamuona, na mke wangu alishtuka na kuogopa sana kuwa nnawataka waondoke na mimi nibaki peke yangu na sikuwa nataka kuwaona. Lakini baadae alielewa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kuwalinda wao," aliiambia BBC.
Baada ya siku saba, alienda hospitali kufanya vipimokwa sababu nilikuwa naogopa ripoti za kwenye mitandao ya kijamii kuhusu virusi vya corona - na alitaka kuhakikisha kuwa hana maambukizi.

Chanzo cha picha, AFP
"Picha ambayo mtandao wa jamii umeweka ni kama kila mtu anayetoka nje ya nchi ana maambukizi tayari," alisema.
Lakini baada ya kufanya vipimo, jina lake na namba yake ya simu ziliwafikia watu bila yeye kujua ni nani alisambaza taarifa hizo - huku watu mtandaoni wakiwa wanadai kuwa ana virusi vya corona.
Hata kama alikutwa hana corona , alikuwa anaogopa kutoka nje kwa sababu angeshutumiwa kuwa anataka kuwaambukiza watu wengine.
Aliwasiliana na bi.Mwabili kuona namna taarifa zake zilivyowafikia watu: "Akaniambia kuwa hata wafanyakazi wenzie pia walikuwa wanamuhoji kwa nini hajitengi . Lakini sikuwa hata na maambukizi."
Taarifa ya Polisi kuvuja
Bi Mwabili alitakiwa kufika kituo cha polisi jioni kujieleza kuhusu vipimo vya bwana Muturi.
Maofisa walitaka taarifa kuhusu wagonjwa wa corona ikiwa sehemu ya uchunguzi wa kuwasaka wale waliotoroka katika kituo cha karantini.

Chanzo cha picha, Davis Muturi
Inaonekana taarifa za polisi ndio zilivuja.
"Sifahamu haswa namna gani jina na taarifa kuhusu mteja wangu zilivyosambaa kwa watu," alisema.
Hospitali ililaumu taarifa hizo kutolewa na polisi walisema kuwa wanafanya uchunguzi.
Bi. Mwabili anasema kuwa anapata wakati mgumu zaidi baada ya taarifa hizo kuvuja, ilimbidi apumzike kwa wiki nzima.
"Wakati niliporejea kazini, baadhi ya wafanyakazi wenzangu walinihoji kama nilikuwa karantini?'... Unakuwa unawaza hawa wanawaza nini katika akili zao mpaka kunihoji hivyo."


Zaidi ya mwezi sasa, bi. Mwabili anasema kuwa watu jasiri huwa wanapitia wakati mgumu.
Changamoto hiyo imemfanya imempa ujasiri kufanya kazi yake vizuri zaidi , na kuona kuwa mgonjwa awe ana corona au hana ila jukumu lake kumuhudumia.
Huku Bwana Muturi, anasema kuwa wakati alipobaini kuwa hana virusi vya corona, alikuwa hawezi kusubiri kumuona mtoto wake mpya.
"Siku hiyo hiyo , ilibidi familia yangu warudi haraka, sikuweza kuruhusu familia yangu kukaa mbali nami kwa usiku mwingine."













