Virusi vya Corona: Shule ya baba na mama

Iliyochapishwa

Shule nyigi katika maeneo mbalimbali duniani zimefungwa wakati nyingine hazijui lini zitafunguliwa, hii ikiwa ni hatua ambayo serikali za nchi husika zimechuka kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Na sasa wazazi wanapaswa kuchukua jukumu hilo la kuwafundisha watoto nyumbani, na kuziba mwanya huo.

Hata hivyo kuna nyenzo nyingi ambazo ziko mtandaoni kwa ajili ya kuwasaidia wazazi kuwafundisha watoto wao nyumbani, licha ya kwamba hakuna anayetarajia kuwa wanaweza kufanya kazi sawa na walimu.

Lakini kuna ugumu kiasi gani kufanikisha masomo hayo kuendelea nyumbani na je wanaweza kutulia na kusoma nyumbani?

Mwalimu mmoja nchini Tanzania ameeleza ugumu uliopo wa kutumia teknolojia ili kuwafundisha wanafunzi.

Mwalimu anasema kuwa ni vigumu kwa wanafunzi kuelewa na baadhi ya wazazi wanashindwa kuwasaidia watoto wao kumaliza kazi zao hata komputa hawana wengine.

Wakati kwa upande wa wazazi, bi Shafia Twahir anasema kuwa yeye ana watoto wadogo na anakutana na changamoto kwa sababu hajawahi kufundisha na watoto kutulia ni ngumu sana.

"Mimi ni mzazi na mtoto kanizoea, hivyo mara nyingine anaweza kudhani tunataniana."

Aidha walimu wamekuwa wakitumia kazi kupitia whatsapp kutuma kazi kwa wanafunzi.

Huku mzazi mwingine Ambele Mwakatobe anasema "ualimu ni taaluma na mimi sio mwalimu, hivyo unaweza mnakuta mnabishana na anamuamini mwalimu wake zaidi yangu," ameongeza kusema kuwa wakati yeye anasoma ni tofauti na jinsi wanavyosoma sasa, hata ukianza tu kwa kutamka ABCD... wanafunzi wa sasa wanatamka tofauti na watu waliosoma zamani.

Je, shule zinawezaje kuwasaidia wazazi kufundisha?

Kama shule zinaweza kutuma nyenzo za kufundishia mtandaoni na kutuma maelekezo ya mtaala ambao unaotumika shuleni , je hali hii itasaidia.

Shule za sekondari wanaweza kutumia mfumo huu wa mtandao zaidi ya wanafunzi wa shule za msingi, kwa sababu ni rahisi kwa walimu na wanafunzi kuwasiliana kupitia simu na kusahihishiwa kazi zao.

Na vilevile wanafunzi wa sekondari wanaweza kutumia komputa au hata wanamiliki simu ambazo zinaweza kuwasaidia kujifunza wakiwa nyumbani.

Inawezekana ni wakati muafaka kwa shule kuhamia kutumia mfumo wa mtandao ili kuhakikisha masomo ya kila siku yanaendelea.

Mfumo wa mtandao unawawezesha watoto kufanya kazi zao na kutuma ili waweze kusahihishiwa.

Masomo ya mtandaoni yanasaidia

Shule nyingi wanapaswa kutumia mitandao ili kuwasaidia usoma hesabu.

Wazazi wanapaswa kufuatilia namna ya kupata vitamu na walimu kuandaa kazi ambazo wanafunzi wanaweza kufanya wakiwa nyumbani.

Ni muhimu kwa wazazi kuwa wadadisi kuuliza ni namna gani wanaweza kupata nyenzo ambazo hazitawakuwa na gharama kubwa kuwasaidia watoto wao katika masomo,

Vitabu gani ni muhimu kununua watoto wao.

Wataalamu wengi wa elimu walikuwa wanahoji kwa muda mrefu hata kabla ya janga la corona kuwa mfumo wa elimu unapaswa kubadilika.

Wakati huu ndio mawazo ya kuweka mfumo mpya wa kusoma ndio unaanza au unafikiriwa kuanza.

Ingekuwa njema kuwa na njia mbadala ya kujifunza na njia ya mtandao ndio sahihi .

Ni njema kuwafundisha watoto jinsi dunia inavyofanya kazi wakiwa wadogo ili kuwavutia zaidi na huo ni mfumo wa mtandao.

Lakini kwa sasa, ni vyema mzazi kutathimini ni njia gani inaweza kuwasaidia kusoma wakiwa nyumbani.

Si kujifunza peke yake…

Kumbuka kuwa kujifunza ni muhimu, lakini watoto wanapaswa kuwa na muda wa kucheza na kufanya shughuli nyingine za nyumbani na kutoka nje kwa wakati sahihi.

Ni vyema kwa wao kucheza na wakati kama huu michezo ya ndani ni muhimu ili kuchangamsha akili na vilevile wazazi wanapaswa kutenga muda ili watoto wao waweze kuongea na watoto wenzao kupitia mtandao au ndugu zao wengine badala ya kujifungia ndani peke yao.

Zoom au Skype zinaweza kuwasaidia kuwasiliana na marafiki zao.

Mzazi jaribu kutafuta filamu za zamani ambazo ulikuwa unapenda kuangalia ukiwa mdogo ili uangalie nao na kuwafundisha.

Wahamasishe kusoma vitabu mbalimbali mtandaoni kuna zaidi ya vitabu 3,000 ambavyo si vya kununua mtandaoni , mtoto au kijana anaweza kuvitumia akiwa nyumbani.

Ni muhimu kuongelea maisha ya baadae na namna unavyotaka yarudi kuwa kama ya kawaida.