Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2022: DR Congo 'Tumetoka mbali sana tangu Zaire mwaka 1974'
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya DR Congo Gabriel Zakuani anasema nchi hiyo imeimarisha mchezo wake wa soka tangu waliposhiriki michuano ya kombe la dunia kama Zaire, mwaka 1974.
Leopards watakuwa wenyeji wa Morocco katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa Kombe la Dunia leo Ijumaa mjini Kinshasa kabla ya mechi ya marudianoitakayochezwa huko Casablanca Jumanne ijayo.
Mwaka 1974, Zaire - ambayo sasa inafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - iliandikisha historia wakati ilipokuwa nchi ya kwanza kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.
Kwa bahati mbaya histori ya mabingwa hao wa Afrika wa wakati huo inakumbukwa kwa jinsi walivyofungwa mabao 9-0 na Yugoslavia na mbwembwe zisizo za kawaida za Mwepu Ilunga ambaye alikimbia nje ya ukuta wa ulinzi kwa mpira wa faulo wa Brazil na kuupiga mpira nje ya uwanja.
"Nadhani nchi imetoka mbali," Zakuani, ambaye alistaafu majukumu ya kimataifa mwaka 2018,aliambia BBC Afrika Michezo.
"Tunatazamia kuendana na wakati. Wachezaji wako Ulaya, wanacheza katika michezo mikubwa na tofauti sasa itakuwa kuwakilisha nchi.
"Sasa tuna wachezaji wanaoshiriki lifi za daraja la juu duniani, kwa hivyo sio sawa na kuchezesha wachezaji wa nyumbani ambao walijitolea kucheza kwa moyo wao wote .
"Sasa kuna wachezaji ambao wanaweza kushindana katika kiwango cha aina hiyo."
Mara ya mwisho DR Congo ilikaribia kufika fainali ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1974 ilikuwa michuano ya kufuzu kwa michezo hiyo nchini Urusi, wakati mabingwa hao wa Afrika mara bili walimaliza kwa alama moja tu nchuma ya Tunisia.
Kushindwa huko kulichangiwa na pia kukosa kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 lililochezwa mwaka huu nchini Cameroon, lakini Zakuani anaamini hilo sio tatizo.
"Ni wazi kwamba kila mtu amehuzunishwa - sote tunataka kuwa kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika," alielezea.
"HUenda ilikuwa baraka kimpango kwani sasa tuna uchu zaidi, kwa sababu ya kukosa kushiriki michuano hiyo, na kutumia uchungu tuliyokuwa nayo - kutazama mataifa mengine ya Afrika yakishindana katika michuano ya Kombe la Mataifa - kama motisha ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.
"Tulikisolewa sana nyumba DR Congo. Kufuzu kwa Kombe la Dunia kunahitaji kujituma zaidi."
Ushawishi wa Cuper
Zakuani pia anahisi kuteuliwa kwa Muargentina Hector Cuper mnao May 2021kuchukua nafasi ya mkufunzi wa nyumbani Florent Ibenge inaisaidia timu kusonga mbele ili kuweza kutinga katika kiwango cha juu zaidi.
"Ilitubidi kufuata njia ya Florent kwa sababu tulihitaji kuwaunganisha wachezaji wa nyumbani na wachezaji wa Ulaya na wale wanaocheza maeneo mengine duniani," alielezea.
"Nafikiri Florent alifanya vyema wakati tuliposhika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
"Tulihitaji kwenda njia nyingine. Tulijaribu hilo awali na Claude Le Roy,ambaye ni kocha maarufu kote duniani, na hasa katika soka la Afrika.
"Tukiwa na Hector, tuna mawazo mapya hata kama anahangaika na lugha kwa sasa, lakini ana mfasiri wa kufafanua mawazo yake.
"Mazoezi ni ya kiufundi zaidi na ni suala la kuchukua hatua ndogo za ziada. Tuna nia ya kushinda, tunajiimarisha upande wa kimkakati wa mambo - ujuzi zaidi, jinsi ya kuangalia michezo na kupata matokeo hayo. na ndicho kilichomfanya ajumuishwe kwenye timu.
"Kila mtu ana nia ya kujifunza kutoka kwake, kwa sababu ni wazi tuna wachezaji wazuri, lakini tunatatizika kila wakati kupata matokeo hayo muhimu na muhimu ili kutuingiza kwenye mashindano haya makubwa."
Faida ya nyumbani
Sababu nyingine ambayo Zakuani anaamini inaweza kusaidia Leopards katika mechi yao leo Ijumaa ni umati wa mashabiki nyumbani utakaofurikia Stade de Martyrs katika mji mkuu Kinshasa..
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo haijacheza kwenye uwanja huo, ambao pia ulikuwa mwenyeji wa pambano la ngumi la 'Rumble in the Jungle wakati Muhammad Ali alipomshangaza George Foreman mnamo 1974, tangu 2019.
"[Mazingira] hayaelezeki - ni hisia za tamasha," aliongeza.
"Kila mtu amekuwa akingojea siku hii kwa muda mrefu sana. Kila kitu kimewekwa kando. Maswala yote ya kisiasa na mengineo nchini yamesitishwa, wakati huu watu wameweka kado tofauti zao na kuwa kitu kimoja.