Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.03.2022: Raphinha, Lewandowski, Origi, Rudiger, Mitchell

Divock Origi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Divock Origi akishangilia kufugia Liverpool bao
Iliyochapishwa

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 26, anafanya mazungumzo na wapinzani wa Serie A, AC Milan na Inter Milan kuhusu uwezekano wa uhamisho msimu huu wa joto. (90min)

Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa Bayern Munich na nahodha wa timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski, 33. (Sport - kwa Kihipania)

Robert Lewandowski

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona pia wameungana na Liverpool, Manchester City na Bayern Munich katika mbio za kumsaka winga waLeeds na Brazil Raphinha, 25, ambaye anauzwa kwa £60m. (Mirror)

Manchester City ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ligi ya Primia zinazomfuatilia beki wa Crystal Palace Tyrick Mitchell baada ya mchezaji huyo wa miaka 22- kujuishwa katika timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza. (Sun)

Mlinzi wa Chelsea Marcos Alonso, 31, anasema "angependelea" kucheza tena La Liga. Mhispania huyo alichezea Real Madrid ligi moja tu kupitia mfumo wao wa vijana. (AS - kwa Kihispania)

Nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 32, yuko katika njia panda kati ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na the Blues ama kukubali ofa ya mwaka mmoja kutoka kwa Barcelona. (Express)

Cesar Azpilicueta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta

Mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Antonio Rudiger, 29, anaweza kuwa beki wa tatu wa Chelsea kuondoka Stamford Bridge mkataba wake unapoelekea kumalizika msimu wa joto na tayari amepewa mkataba na Juventus. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Blackburn na Chile Ben Brereton Diaz, 22, ananyatiwa na Sevilla ambao wanataka azibe nafasi ya tisa ya klabu hiyo ya La Liga. (Estadio Deportivo - kwa Kihispania)

West Ham huenda wakajaribu tena kumnunua mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez, baada ya kiungo huyo wa miaka 22 kukataa dau la £50m la kuvunja rekodi ya klabu hiyo mwezi Januari. (Standard)

Darwin Nunez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal wanamfuatilia mshambuliaji wa Benfica Darwin Nunez

Leeds wanataka kumsajili winga Muingereza Ryan Kent kutoka Rangers, huku mchezaji huyo wa maika 25- akiwa na kipengee kuachiliwa kwa £20m katika mkataba wake. (Football Insider)

Arsenal na Tottenham watahitaji kulipa pauni milioni 20 kumsajili beki wa chini ya miaka 21- wa Middlesbrough Djed Spence, ambaye mchezo wake huko Nottingham Forest kwa mkopo unaridhisha. (Express)

Benfica na Sporting Lisbon wanapania kumnunua winga wa Barcelona Francisco Trincao, ikiwa kiungo huyo wa miaka 22 anayechezea Wolves kwa mkopo hatajiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa kudumu wa pauni milioni 25. (Record - in Portuguese)

Kiungi wa kati wa Barcelona Mhispania Gavi, 17, na beki wa Uruguay Ronald Araujo wamekataa kusaini mkataba mpya waliyopewa na klabu hiyo. (Marca -kwa Kihispania)