Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 23.03.2022: Salah, Dybala, Kessie, Hazard, Jovic
Kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 25 amefikia mkataba wa miaka minne na Barcelona na atajiunga na klabu hiyo ya Nou Camp msimu huu wa joto wakati mkataba wake na AC Milan utakapokamilika. (Guardian)
Juventus wanatayarisha kitita kikubwa cha fedha ili kumnasa mshambuliaji wa Misri mwenye umri wa miaka 29 Mohamed Salah kutoka Liverpool hadi Turin. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester United wanamfikiria mkufunzi wa Sevilla Mhispania Julen Lopetegui, 55, huku wakiendelea kutafuta mrithi wa kudumu wa Ralf Rangnick. (Marca kwa Kihispania)
Mshmabuliaji wa Serbia Luka Jovic, 24, sio sehemu ya mpango wa mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti na pia ataondoka klabu hiyo ya Uhispania msimu huu wa joto. (Marca)
Newcastle wameongeza juhudi za kumsajili beki wa kati wa Bournemouth wa miaka 23-Muingereza Lloyd Kelly katika mkataba wa pauni milioni 12. (Express)
Winga wa Ubelgiji Eden Hazard amechanganyikiwa na kughadhabishwa na klabu ya Real Madrid, ambayo ina nia ya kumuuza kiungo huyo wa miaka 31- msimu huu wa joto. (Goal)
Mshambuliaji wa Brazil Raphinha, 25, amekata ombi la kwanza la Leeds United kuhusu mkataba mpya. (UOL - in Portuguese)
Mshambulizi wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Ruud van Nistelrooy, 45, anaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwa kocha wa PSV Eindhoven. (Mirror)
Nyota wa Brazil Neymar, 30, anapokea £600,000 kwa mwezi zaidi ya Muargentina Lionel Messi, 34, katika klabu ya Paris St-Germain. (L'Equipe, via Star)
Arsenal na Tottenham wanamfuatilia winga wa Galatasaray mwenye umri wa miaka 23- Mturuki Muhammed Kerem Akturkoglu. (Aksam - in Turkish)