Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 18.03.2022: Rashford, Ronaldo, Rice, Tielemans, Hazard, Nunez, Neves

Marcus Rushford

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Barcelona wameonyesha nia yao ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 24.Mwaka 2019 Rashford alisaini mkataba wa United wa kulipwa £200,000-kwa wiki unaoishia June 2023 lakini amekua na kiwango kibovu msimu huu. (Manchester Evening News)Mshambuliaji wa United mreno Cristiano Ronaldo, 37, anajiandaa kusalia Manchester United msimu ujao, huku meneja wa muda Ralf Rangnick akitarajiwa kuondoka. (AS)

.Cristiano Ronaldo

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Cristiano Ronaldo

Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea aliyeko Real Madrid Eden Hazard, 31. Mbelgiji huyo alijiunga Real mwaka 2019. (FootMercato - in French)Benfica imemuwekea bei ya £67m mshambuliaji wake raia wa Uruguay Darwin Nunez, 22, ambaye aliisaidia klabu hiyo ya Ureno kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Nunez anavivutia pia vilabu vya Arsenal, Manchester United naNewcastle. (Mirror)Kinda lenye miaka 19 mlinzi wa Ajax na Uholanzi Ryan Gravenberch anasakwa na Manchester United. (The Athletic - subscription required)

.Declaran Rice

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, .Declaran Rice

Wachezaji wanaowaniwa na Chelsea kuna wasiwasi wasiweze kujiunga na mabingwa hao watetezi wa ligi ya mabingwa Ulaya, anaonya wakala. Klabu hiyo imekua ikihusishwa na wachezaji kadhaa akiwemo kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 23. (Daily Mail)Wakala wa Jorginho anasema kipaumbele kikubwa kwa sasa cha mchezaji huyo mwenye miaka 30 ni kusaini mkataba mpya wa kusalia Chelsea, licha ya kusakwa na magwiji wa Serie A Juventus. (90Min) Antonio Conte hataondoka Tottenham msimu huu, anasema mlinda mlango na nahodha mfaransa Hugo Lloris. Gwiji hilo linaamini muitalia huyo sio wale "wanaokata tamaa mapema katika mazingira yoyote". (Evening Standard)

Divock Origi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Divock Origi

Mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 26, anajiandaa kujiunga na AC Milan mwishoni mwa msimu. (Fabrizio Romano)Vinara wa Championship Fulham wanawataka walinzi wa Liverpool Joe Gomez na Neco Williams. Mchezaji wa kimataifa wa England Gomez, 24, anauzwa na wekundu hao kwa bei ya £23m. Mlinzi wa pembeni wa Wales Williams, 20, kwa sasa anacheza kwa mkopo huko Craven Cottage. (Express