Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 06.03.2022: Pogba, Saka, Wijnaldum, Haaland, Onana, Christensen, Diaby, Kepa,

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wamewasiliana na wakala wa Paul Pogba Mino Raiola kuhusu uwezekano wa kiungo huyo wa kati wa Manchester United kurejea Turin msimu ujao. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Pogba itabidi akubali kupunguziwa mshahara iwapo atarejea Juve, ambao wanaona harakati zao za kumpata itakuwa ngumu huku Paris St-Germain na Real Madrid zikiwamo pia katika kinyang'anyiro cha kumnasa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Kiungo wa kati wa Ungereza Bukayo Saka hana mpango wa kuondoka Arsenal, licha ya Liverpool kuonesha nia ya kutaka kumnunua nyota huyo wa miaka 20. (Sun on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji wa chini ya miaka -21 Amadou Onana kutoka Lille, ambayo inataka zaidi ya £20m kumuachilia kiungo huyo wa miaka 20. (Sun on Sunday)
Atletico Madrid wanatathmini uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Paris St-Germain wa miaka 31-Mholanzi Gini Wijnaldum, ambaye inasemekana anazingatia mustakabali wake katika mji mkuu wa Ufaransa chini ya mwaka mmoja ndani ya mkataba wa miaka mitatu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Mlinzi wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25, amekataa kujiunga na klabu pinzani za Ligi ya Primia na anakaribia kufikia mkataba na Barcelona, ambayo imetoa ofa nzuri zaidi ya Bayern Munich. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Reuters
Mkufunzi wa Barcelona Xavi Hernandez anaamini klabu huyo itashinda kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,21, huku meneja huyo wa Uhispania akikataa kukana kwamba alisafiri kwa ndege hadi Ujerumani kukutana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway wiki jana. (Sun Jumapili)
Kocha wa Lazio Maurizio Sarri anapani a kuungana tena na kipa wa Chelsea wa miaka 27- Kepa Arrizabalaga mjini Rome, huku Mkufunzi huyo wa zamani wa Blues akimtambulisha Mhispania huyo kama lengo la mkopo msimu wa joto. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Leeds huenda wkawasilisha dau la kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United wa miaka 20- James Garner msimu wa joto, huku Southampton pia wakimfuatilia kiungo huyo wawa kimataifa wa Uingereza wa chini ya miaka -21 ambaye yuko Nottingham Forest kwa mkopo. (Sun on Sunday)
Arsenal na Newcastle United wanamtaka mshambuliaji wa Sevilla na Morocco wa miaka 24-Youssef En-Nesyri, ambaye alihusishwa na uhamisho wa Manchester United mwezi Januari. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa Real Sociedad raia wa Uswidi Alexander Isak, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Uingereza na Everton Dominic Calvert-Lewin, 24, wametajwa kuwa walengwa wa Arsenal baada ya mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta kusema kuwa mshambuliaji ndiye atakayepewa kipaumbele katika uhamisho wa majira haya ya joto. (Sunday Express)
Bayer Leverkusen itataka ada ya euro milioni 100 itakayovunja rekodi ya klabu kumuuza winga wa Ufaransa Moussa Diaby, 22, ambaye anasakwa na Newcastle. (Sport Witness)
Crystal Palace wameungana na Manchester United, Newcastle na West Ham katika kinyang'anyiro cha kumnasa kiungo wa kati wa wa miaka 22-Mfaransa Boubacar Kamara kutoka Marseille. (Sun on Sunday)
Mlinzi wa Wales Joe Rodon, 24, huensa akaondoka Tottenham msimu wa joto baada ya kuhangaika kupata nafasi chini ya kocha Antonio Conte. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Czech Republic Alex Kral amehusishwa na uhamisho wa klabu ya Montpellier inayoshiriki Ligue 1 ya Ufaransa msimu ujao, huku West Ham wakiwa na uwezekano wa kuchukua chaguo la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 wakati mkopo wake kutoka Spartak Moscow utakapokamilika msimu wa joto. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)












