Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 05.03.2022: Traore, Pochettino, Lewandowski, Haaland, Traore, Rudiger, Rice, Klopp
Barcelon bado hawajaamua iwapo watatoa ofa ya kuendelea kubakia na winga Muhispania mwenye umri wa miaka 26- Adama Traore kwa mkataba wa kudumu mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake na Wolves utakapokuwa umemalizika. (AS - in Spanish)
Manager Thomas Tuchel anahofu Chelsea itapoteza mikataba ya walinzi - Cesar Azpilicueta, Antonio Rudiger na Andreas Christensen huku kukiwa na hali ya sintofahamu katika klabu hiyo baada ya mmilikiwake Roman Abramovich kuwaweka sokoni the Blues. Mhispania Azpilicueta, 32, amekuwa akihusishwa na Barcelona, huku Borussia Dortmund wakionyesha nia ya kumchukua Dane Christensen mwenye umri wa miaka 25, na Manchester United wakiripotiwa kuwa makini na mchezaji wa kimataifa wa Ujrumani Rudiger, 29. (Sun)
Meneja wa Paris St-Germain Muargentina Mauricio Pochettino, ambaye amekuwa akihusishwa na kazi ya umeneja katika Manchester United, anaripotiwa kuwa makini kurejea katika kazi yake ya zamani kama meneja wa Tottenham. (Talksport)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema hakuna kilichobadika kuhusu mkataba wake huku mkutaba wake ukitarajiwa kumalizika mwaka 2024. (Sky Sports)
Manchester United wamewaomba wawakilishi wa Robert Lewandowski kuendelea kuwafahamisha kuhusu hali ya baadaye ya mshambuliaji wa katika Bayern Munich, huku klabu ya with Bavaria ikiripotiwa kujaribu kumpanga mchezaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland kama mchezaji atakayemrithi Lewandowski mwenye umri wa miaka 33. (90min)
Wakala wa Haaland Mino Raiola ameripotiwa kuiambia Barcelona kwamba pia watatakiwa kusaini mkataba na mteja wake mwingine, kiungo wa nyuma kulia wa Ajax mwenye umri wa miaka 24- rai awa Morocco Noussair Mazraoui, ili kuongeza fursa yao ya kusaini mkataba na Mnorway. (Sport, via Express)
Borussia Dortmund wanaweza kusaini mkataba na kiungo wa safu ya mashambulizi ya Real Madrid Luka Jovic, 24, kama mchezaji mbadala wa Haaland, 21, iwapo nyota huyo ataondoka msimu huu. (Fichajes - in Spanish)
Everton wanasubiri ofa ya kusaini mkataba na Mshambuliaji wa England mwenye umri wa miaka 24- Dominic Calvert-Lewin na mshambuliaji Mbrazili Richarlison, 24, katika msimu ujao. (Telegraph, subscription required)
Mshambuliaji wa Arsenal Mbrazili mwenye umri wa miaka 20 - Gabriel Martinelli amesema kuwa anataka kubakia katika Gunners "Maisha yake yote" na ameazimia kuisaidia kufiukia Championi Ligi. (ESPN Brasil - in Portuguese)
Armando Broja anaweza kuelekea upande mwingine wa London kuwa na West Ham ikifahamika kuwa yuko tayari kutoa malipo ya pauni milioni 25 kwa mshambuliaji Malbania mwenye umri wa miaka ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika Southampton kutoka Chelsea. (Sport - in Spanish)
Sevilla hawatajaribu kuendelea kumshikilia mshambuliaji wa Manchester United mwenye umri wa miaka 26 Mfaransa Anthony Martial baada ya kuisha kwa mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Football Transfers)
Kiungo wa kati wa West Ham mwenye umri wa miaka 23- Muingereza Declan Rice, ambaye amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na Chelsea na Manchester United, ameelezea bei ya pauni milioni 100 ambayo hammers walimuhusisha nayo kama "wazimu". (Evening Standard)
Arsenal wameripotiwa kuomba uwezekano wa kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Napoli Mhispania Fabian Ruiz, 25, msimu huu. (Area Napoli - in Italian)
Meneja wa Newcastle United Eddie Howe anamtaka kiungo wa kati Muingereza Sean Longstaff asaini kurefusha zaidi mkataba wake ambao klabu imempatia . Mkataba wa sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 unakwisha msimu ujao wa kiangazi. (Sky Sports)
Rais wa Marseille Pablo Longoria amesema kuwa anataka kuendelea kubakia na mlinzi Mfaransa William Saliba baada ya mkataba wa mkopo kutoka Arsenal mwishoni mwa msimu, na kuweka shinikizo kwa meneja wa Gunners, Mikel Arteta kuchukua uamuzio juu ya hali ya baadaye ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Le Provence, via Mirror)
Arsenal wamehusishwa kuhamishwa kwa mlinzi wa Peru mwenye umri wa miaka 21 Jhilmar Lora, ambaye anachezea klabu ya nchini mwake inayofahamika kama Club Sporting Cristal, huku as the Gunners wakitaka kuwaajiri wachezaji kutoka Amerika Kusini msimu huu. (Football London)