Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 19.02.2022: Kane, Haaland, Azpilicueta, Eze, Van de Beek, Gavi

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Real Madrid wamewasilisha ofa ya mwisho kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, ambayo inaweza kuwa pigo kwa matumaini ya Manchester United, Chelsea na Manchester City ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway(Sport via Sun)

Harry Kane, 28, atasubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua mustakabali wake wa Tottenham, huku nahodha huyo wa Uingereza kwa sasa hataki kujadili kuongezwa kwa mkataba wake. (Standard)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wamekasirishwa kufuatia kushindwa kumpata mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 22, huku Mikel Arteta sasa akikabiliwa na kinyang'anyiro cha kusuluhisha kitendawili cha mshambuliaji wa klabu hiyo(Mirror)

Dusan Vlahovic

Thomas Tuchel anasema Cesar Azpilicueta bado ni "muhimu sana" kwa mipango yake ya Chelsea licha ya kandarasi ya beki huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 32 kumalizika.(Mail)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wamempa Azpilicueta mkataba wa miaka miwili na chaguo la kurefusha kwa msimu zaidi huku wakipania kumnasa nyota huyo wa Chelsea kutoka Stamford Bridge(Fabrizio Romano via Express)

Chelsea ni miongoni mwa klabu zinazomwinda kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi, 17. (El Nacional).

Mchezaji Mwingereza Eberechi Eze, 23, ana furaha katika Crystal Palace huku kukiwa na nia kutoka Newcastle. (Standard)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, anapendelea kuhamia Chelsea ikiwa ataondoka katika klabu hiyo ya La Liga. (Fichajes - in Spanish)

Wilfried Zaha anaweza kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto kwani The Eagles wanataka kupokea ada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, 29, kabla ya mkataba wake kumalizika msimu wa joto wa 2023.(Mail)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, atajaribu kuipa kisogo Manchester United kwa uzuri na kupata uhamisho wa kudumu wa kwenda Everton msimu huu wa joto ikiwa atawasaidia kuendelea kucheza Ligi ya Premia huku akiwa huko kwa mkopo.(Mirror)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Winga wa Tottenham na Uholanzi Steven Bergwijn, 24, anaivutia AC Milan. (Calciomercato)

Uhamisho wa kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira, 26, kwenda Flamengo uko hatarini kuporomoka, matokeo ambayo yataifanya Manchester United kupoteza mamilioni(Sport Witness,Via Mirror)

Marcelo Bielsa amekataa kuzungumzia mustakabali wake huku kukiwa na uvumi iwapo atasalia kuwa kocha mkuu wa Leeds kwa msimu mwingine.(Independent)