Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 13.01.2022: Lamptey,Pogba, Zakaria, Arthur, Bissouma, Tielemans, Haidara

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Paris St-Germain wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, huku Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28 pia akitaka kuhamia klabu hiyo ya Ligue 1. (L'Equipe - subscription required)

Manchester United wanamtaka beki wa kulia wa Brighton, Tariq Lamptey. Brighton wanataka pauni milioni 40 kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye ameichezea timu ya U-21 ya Uingereza. (Mail)

Klabu hiyo ya Old Trafford pia imefanya mawasiliano na wawakilishi wa kiungo wa Borussia Monchengladbach na Uswizi Denis Zakaria, 25. (Christian Falk - Sport Bild)

th

Arsenal wamefanya mawasiliano na Juventus kuhusu mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 25. Pia wanamlenga kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 24. (Goal)

The Gunners pia bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, lakini watakuwa na shida kufadhili uhamisho wa Mserbia huyo kufikia mwisho wa mwezi. (Sky Sports)

Wakati huo huo meneja wa PSG Mauricio Pochettino bado anawasiliana na Man Utd kuhusu uhamisho wa majira ya joto. Meneja wa sasa wa muda Ralf Rangnick, hata hivyo, anamtaka bosi wa Ajax Erik ten Hag. (Le Parisien, via Sun)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Chelsea Antonio Rudiger sasa anapanga kusalia Stamford Bridge. Mjerumani huyo, 28, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao alikuwa akihusishwa na kutaka kuondoka. (Bild, via Teamtalk)

Aston Villa wanawinda saini ya kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma, 25(Telegraph)

Leicester City na Filip Benkovic wamekubali kufuta kandarasi ya beki huyo wa Croatia mwenye umri wa miaka 24. (Leicester Mercury)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Ousmane Dembele anatazamiwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu na Manchester United wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. (Mirror)

Tottenham wamekataa ombi la winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, kutoka Ajax. (Talksport)

Newcastle wanatayarisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa RB Leipzig na Mali Amadou Haidara, 23. (Mail)

Tottenham wanataka kusajili wachezaji watatu muhimu katika dirisha la uhamisho. Spurs wako kwenye mazungumzo na Wolves kuhusu kiungo wa kati wa Uhispania Adama Traore, 25, na wanatafuta beki wa kulia na mshambuliaji. (Telegraph)

Leeds wanavutiwa na beki wa pembeni wa Torino na Nigeria Ola Aina, 25(Calciomercato - in Italian)

Newcastle wametuma ofa mpya ya pauni milioni 28 kwa mlinzi wa Sevilla na Brazil Diego Carlos. Hapo awali The Magpies walikuwa na ofa ya pauni milioni 25 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 iliyokataliwa. (Talksport)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wana nia ya kutaka kumnunua kwa mkopo mshambuliaji wa Barcelona na Uholanzi Memphis Depay, 27 (Di Marzio)

Mlinda lango wa West Ham Lukasz Fabianski anakaribia kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alistaafu kazi ya kimataifa na Poland mwaka jana(Sun)

Manchester United itaweka kipaumbele kandarasi mpya kwa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 unakamilika Juni 2023. (ESPN)

Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl anasema itakuwa vigumu kuhakikisha wachezaji muhimu wanasalia katika klabu hiyo, licha ya kununuliwa kwa klabu hiyo hivi majuzi.