Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 01.01.2022 : Alvarez, Coutinho, Trippier, Rudiger, Traore
Chelsea watalazimika kutoa ofa ya mlinzi wa kati Mjerumani Antonio Rudiger, 28, ya malipo ya juu zaidi kwa wiki kuliko mchezaji yeyote yule wa the Blues ili kumshawishi aongeze zaidi mkataba wake ambao unaisha mwishoni mwa msimu . (Football Insider)
Rudiger anataka kusaini marupurupu ya zaidi ya pauni milioni 16 kwenye mkataba wake na Chelsea na asaini mkataba na Real Madrid kama wakala huru katika msimu huu . (ABC - in Spanish)
Tottenham wanataka kusaini mkataba na mchezaji nyota wa Barcelona na Brazil mwanye umri wa miaka 29- Philippe Coutinho kwa uhamisho huru, Wacatalonia lakini bado wanasubiri kumtoa kwa pauni milioni 17 huku kukiwa na uwezekano wa klabu za Everton na Arsenal kuwa na nia ya kumchukua. (El Nacional - in Catalan)
Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 16.8 zinazohitajika kwa ajili ya kipengele cha mkataba cha kitakachowawezesha kusaini mkataba na mshambuliaji wa River Plate Muargentina Julian Alvarez mwezi Januari , huku wakiwa mbele ya having Bayern Munich, Barcelona, Real Madrid na Inter Milan katika mbio za kusaini mkataba na kijana huyo mwamye umri wa miaka 21. (Sport - in Spanish)
Newcastle wanakaribia kufikia mkataba kwa ajili ya kiungo wa kati-kulia wa Atletico Madrid Muingereza Kieran Trippier, 31, huku kukiwa na vipengele vinavyohusu kushuka kwa daraja la Primia Ligi vikiwa miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa. (Athletic - subscription required)
Tottenham bado wanaendelea kumsana mshambuliaji wa Wolves na Uhispania mwenye umri wa miaka 25 Adama Traore. (Fabrizio Romano via This is Futbol)
Norwich wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mchezaji wa safu ya nyuma-kulia mwenye umri wa miaka 26- Sion na kiungo wa nyuma-kulia Guadeloupe Dimitri Cavare atakaba nafasi ya Max Aarons, ambaye anaendelea kuhusishwa na taari fa za kuondoka katika klabu hiyo ya Carrow Road. (Jeunes Footeux via Norfolk Live)
Manchester City wanajiandaa kumruhusu winga mwenye umri wa miaka 19 anayetazamiwa kufanya vyema siku zijazo Mholanzi Jayden Braaf kuondoka kwneye klabu hiyo Januari huku klabu kadhaa zikimtaka kwa mkataba wa bei nafuu huku akikaribia kumaliza mkataba wake. (Manchester Evening News)
Sunderland wanakaribia kukamilisha mkataba na winga wa Manchester City mwenye umri wa miaka 24 Patrick Roberts. Muingereza huyo kwa sasa anacheza kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Ufaransa ya Troyes. (Football Insider)
rsenal imewatambua Mchezaji wa Real Sociedad na Uswidi Alexander Isak, 22, na nyota wa Lille na Canada Jonathan David, 21 kama chaguo linalowezekana ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji. (The Athletic - subscription required)
Chelsea wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye anaweza kuwa chaguo nafuu kuliko nyota wa West Ham na England Declan Rice, 22. (Daily Telegraph's Matt Law on the London is Blue podcast, via Chelsea Chronicle)
Leeds wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Giovanni Simeone, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Verona kutoka Cagliari, majira ya joto. (L'Arena, via Sport Witness)
Barcelona wamemfanya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Alvaro Morata, 29, ambaye kwa sasa yuko Juventus kwa mkopo kutoka Atletico Madrid, kuwa lengo la kuu la Januari. (AS - in Spanish)