Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 30.12.2021: Haaland, Kane, Dembele, Trippier, Henderson, Hernandez

Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane
Iliyochapishwa

Manchester City itasubiri hadi msimu wa joto kuimarisha safiu yao ya mashambulizi. Mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane na Haaland miongoni mwa wachezaji wanaolengwa. (ESPN)

Matumaini ya Barcelona kuongeza mkataba wa winga wa Ufaransa Ousmane Dembele yamepata pigo baada ya mazungumzo kuvunjika. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 unamalizika majira ya joto. (Gerard Moreno, via 90 Min)

Borussia Dortmund wanatazamia kuweka pamoja mpango wa kujaribu kumshawishi mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kusalia nao, huku mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 katika klabu hiyo ukitarajiwa kuamuliwa mwishoni mwa Februari. (Bild, via Mail)

Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle United wanatumai kukamilisha dili la kumnunua beki wa kulia wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier, 31, wiki ijayo na, baada ya kuumia kwa mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson, 29, pia watajaribu kusajili fowadi mwezi Januari. (Telegraph - subscription required)

Chelsea wameuliza kuhusu kupatikana kwa beki wa kushoto wa Ufaransa Theo Hernandez, 24, ambaye AC Milan haitafikiria kumuuza kwa chini ya euro 60m (£50.5m). (Tuttosport, via Football Italia)

Meneja wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amemwambia mlinda mlango wa Uingereza Dean Henderson kwamba hataruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari, huku Tottenham wakifuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Manchester Evening News)

Kipa wa Spurs Hugo Lloris, 35, yuko tayari kurejea katika klabu yake ya zamani ya Nice wakati mkataba wake na klabu hiyo ya London utakapokamilika msimu wa joto. (Foot Mercato, via Mail)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Sevilla hawana nafasi ya kuongeza ofa yao kwa mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial baada ya Manchester United kukataa hatua ya klabu hiyo ya Uhispania kumchukua kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Mundo Deportivo, via Mirror)

Besiktas wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Uturuki Cenk Tosun kutoka Everton kwa mkopo. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 na klabu ya Goodison Park unamalizika majira ya joto. (Fanatik - in Turkish)

Borussia Monchengladbach imethibitisha kwamba kiungo wa kati wa Uswizi Denis Zakaria, 25, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal, Leicester City na Everton miongoni mwa wengine, ataondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (90 Min)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Napoli wana nia ya kumsajili mlinzi wa Manchester United Alex Tuanzebe na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa mkopo wa msimu mzima kwa Aston Villa unaweza kupunguzwa ili aweze kujiunga na timu hiyo ya Italia. (Sky Sport Italia, via Football Italia)

Juventus watakuwa tayari kumuuza winga wa Uswidi Dejan Kulusevski mwenye umri wa miaka 21 kwa euro 35-40m (£29m-34m) mwezi Januari, huku Arsenal, Tottenham na Bayern Munich wakiwa washindani wakuu. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)