Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 27.12.2021: Bale, Isco, Mbappe, Rudiger, Torres, Maitland-Niles, Kel

Iliyochapishwa

Mshambulizi wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 32, na kiungo wa kati wa Uhispania Isco, 29, ndio wagombea wakuu wa kuondoka Real Madrid mwezi Januari, huku kandarasi za wachezaji wote wawili zikimalizika msimu wa joto. (Marca)

Real Madrid inazidi kuwa na uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kutoka Paris St-Germain na, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu ya kigeni kuanzia Januari 1, mustakabali wake hautaamuliwa hadi Machi baada ya mechi ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa kati ya klabu hizo mbili. . (AS, via Mail)

Real Madrid pia wanatarajia mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, kujiunga nao bila malipo mwishoni mwa msimu huu. Huku ikiwa imesalia miezi sita pekee katika mkataba wake, klabu hiyo ya Uhispania ina matumaini ya kutimiza matakwa ya mshahara ya Rudiger. (Telegraph - subscription required)

Mshambulizi wa Manchester City Ferran Torres, 21, yuko nchini kwao Uhispania na atafanyiwa vipimo vya afya Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester United inalenga wachezaji wanne wa Ujerumani wanaotarajiwa kuwasajili. Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz, 18, mlinzi wa kushoto wa Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka 18 Luca Netz, kiungo wa kati wa RB Lepizig Eric Martel na beki wa kati wa VfL Bochum Armel Bella-Kotchap, 20, wote ni miongoni mwa wanaolengwa na meneja wa muda Ralf Rangnick. (Sun)

Newcastle United wanapanga kumsajili kiungo wa Marseille Boubacar Kamara. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, huku Manchester United na Chelsea pia zikivutiwa. (Sun)

Kiungo wa kati wa Uingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, yuko tayari kuondoka Arsenal na kujiunga na Roma ya Italia kwa mkopo. (Goal)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes ana nia ya kumsajili beki wa kati Mwingereza Lloyd Kelly, 23, kutoka kwa wanaowinda kujiunga na championship Bournemouth ili kusaidia kukabiliana na matatizo ya safu ya ulinzi ya timu yake. (Telegraph - subscription required)

Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel amependekeza kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 21, atarejea Stamford Bridge kupigania nafasi ya kujiunga na The Blues baada ya kumalizika kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Crystal Palace. (Metro)

Nahodha wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza John Terry anatarajiwa kurejea klabuni hapo kusaidia maendeleo ya vijana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 aliacha nafasi yake kama msaidizi wa kocha wa wakati huo wa Aston Villa Dean Smith msimu wa joto ili kutafuta taaluma katika usimamizi. . (Athletic - subscription required)