Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 18.12.2021: Martial, Mykolenko, Phillips, Rashford, Torres

Chanzo cha picha, PA
Mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, anataka kuondoka Old Trafford haraka iwezekanavyo, anasema wakala wake. (Manchester Evening News)
Martial anaweza kujiunga na aJuventus katika mwezi wa Januari kwa mkataba wa mkopo hadi mwisho wa msimu . (Sun)

Mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 24,yuko tayari kusaini mkataba kwa ajili ya Barcelona. (Sport - in Spanish)
Wamiliki wa klabu ya Newcastle United wameshauriwa kumhamisha Martial ili kuboresha kikosi cha mashambulizi katika klabu hiyo. (Transfer Window Podcast

Liverpool wamemuwekea bei ya pauni milioni 15 kiungo wa safu ya Kati-nyuma Muingereza Nat Phillips, mwenye umri wa miaka . (Athletic)
Everton wamefikia makubaliano na Dynamo Kyiv ya kusaini mkataba na kiungo wa kati-nyuma Nat Phillips, mweney umri wa miaka 25, kwa malipo ya pauni milioni 18. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa safu ya mashambulizi wa Manchester City na Uhispania Ferran Torres, 21, ni mchezaji mkuu anayelengwa na meneja wa Barcelona Xavi wakati kitakapofika kipindi cha uhamisho wa wachezaji mwezi . (Sport - in Spanish)
Chelsea, Barcelona, Bayern Munich na Ajax zote zimewatuma mawakala wake katika klabu ya FC Copenhagen kumwinda kiungo wa kati Msweden midfielder Roony Bardghji mwenye umri wa miaka 16. (Goal)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta yuko makini kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Arthur Melo, mwenye umri wa miaka 25, katka kikosi chake cha Gunners pindi itakapofika mwezi Januari. (FourFourTwo)
Leeds United wamepata pigo katika juhudi zao za uhamisho wa wachezaji mwezi Januari baada ya kiungo wa kati Muingereza John Swift, 26, kusema anataka kuendelea kubakia katika Reading. (Reading Chronicle)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanamtaka kiungo wa safu ya nyuma -kushoto wa AC Milan na Ufaransa Theo Hernandez, 24, kwa ajili ya kukaba nafasi ya mlinzi wa England Ben Chilwell. (El Nacional - in Catalan)
Arsenal wanavutiwa na kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Arthur Melo, 25, pamoja na winga wa Uswidi mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski.(Calciomercato-in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Dynamo Kiev wa Ukraine Vitaliy Mykolenko, 25, kwa £20m. (Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamemtambua Illan Meslier wa Leeds United kama mlinda mlango bora chipukizi nchini Uingereza - lakini walipomtuma mlinda mlango Tony Coton kumtazama Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21, ilibainika kuwa aliruhusu mabao saba huko Manchester City Jumanne.(Mail)
Newcastle United wameamua kuvunja mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati Muingereza Matty Longstaff na kumchukua Aberdeen. (Chronicle)
Unaweza pia kutazama:













