Ni wakati kuuliza: Je kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anaiweza kazi ya kuifunza klabu hiyo?

Iliyochapishwa

Ole Gunnar Solskjaer alionekana amevunjika moyo wakati alielekea kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kipigo cha 4-2 huko Leicester City.

Wakati raia huyo wa Norway alitembea kwenda kona ya uwanja kuwapa moyo mashabiki waliokuwa wanaondoka, alikumbana na shangwe za huruma, hasira na viti vilivyokuwa wazi.

Leicester walistahili ushindi wao walistahili kushinda hata zaidi. Manchester United walistahili kushindwa na hata kushindwa zaidi.

Meneja huyo wa United alionekana kuchaganyikiwa wakati mwingine wakati Leicester walikichanganya kikokosi kilichojengwa kwa gharama kubwa lakini kilichokosa mpangilio na uongozi.

Kama meneja, Solskjaer atabeba lawama nyingi lakini baadhi ya maafiaa wa klabu hiyo pia wako taabani baada ya mechi hii.

Pia kuna swali watu zaidi watauliza ikiwa matokeo duni ya Machester united yataendelea.

Je Solskjaer ni mtu sahihi kuendelea kuongoza Manchester United?

Solskjaer sasa ndiye wa kulaumiwa, huenda alipata marafika wachache wenye huruma kati ya mashabiki waliokuwa wamebaki wakati aliamua kutembea kwenda walikokuwa.

Kati ya waliomtetea ni Solskjaer ni aliye na rekodi ya pointi sawa na yeye kocha Jurgen Klopp wa Liverpool, na wawili hao wanakutana huko Old Trafford siku ya Jumapili.

Kati ya mechi zake 104 za kwanza huko Liverpool, Klopp alishinda pointii 196 za ligi huku Solskjaer akiwa ameshinda pointi 194 wakati kama huo huko Old Trafford. Ushindi wa Jumapili ungemweka mbele ya Klopp.

Lakini tatizo lilipo upande wa Solskjaer ni kwamba kasi inaongekezeka kutoka kipindi hiki. Katika mechi 123 za Klopp, alishida na pointi 283 ikiwa ni kama pointi 2.30 kwa kila mechi.

United haionyeshi dalili yoyote ya kuikaribia Liverpool ya Klopp, ambaye alishinda Ligi ya mabingwa mwaka 2019 na Ligi ya Primia mwaka 2020.

Hii inaweka matumaini makubwa kwa mechi ya wikendi huko Old Traffoerd. Ni muhimu kwa United hasa kwa Solskjaer kwasababu alionekana kuchanganyikiwa na kushindwa la kufanya wakati Leicester walikimbia na ushindi.

Hata baada ya kuwabadilisha Scott McTominay na Jesse Lingard kwa Greenwood na Matic wakati matokeo yalikuwa 2-1, kulikuwa na hofu iliyoathiri matokeo yote ya Manchester united.

Hizi zimekuwa wiki chache mbaya kwa Manchester United na meneja wao.

Baada ya ushindi uliofuatia kurejea kwake Ronaldo na mabao yake mawili na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle, Solskjaer ameshindwa na Young Boys, akashinda West Ham United kabla ya kupoteza nyumbani dhidi yao katika kombe la EFL, wakashindwa na Aston Villa nyumbani na kushinda sekunde za mwisho dhidi ya Villarreal kabla ya kulimwa nyumbani na Everton.

Kuna wachezaji wazuri katika timu ya United kwa mfano Luke Shaw, Maguire, Pogba, Ronaldo, Greenwood, Fernandes na Jadon Sancho lakani mara nyingi yaonekana kuwa United na Soskjaer wanatumaini kuwa washambulizi wao watapata njia ya kushinda badala ya kuwa na mpangalio bora wa mechi.

Watahitaji kuimarika dhidi ya Livepool.

Solskjaer sasa ana kibarua kigumu dhidi ya Atalanta nyumbani katika Ligi ya mabingwa na kisha dhidi ya Liverpool ambao wameiona mianya katika safu ya ulinzi ya United.