PSG V Man City: Zimwi la Messi la ukame lamalizika na bao dhidi ya mbingwa wa Uingereza

Iliyochapishwa

Ulikuwa ni uhusiano wenye mafanikio makubwa zaidi wa kocha na mchezaji wake katika nyakati za soka la sasa. Pep Guardiola na Lionel Messi wameshinda makombe 14 pamoja katika kipindi cha miaka minne wakiwa Barcelona na wawili hao wamekuwa wakitawala soka la Ulaya katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja sasa.

Tangu watengane, Guardiola alipoondoka katika klabu hiyo ya Catalan mwaka 2012, no hakuna mchezaji mchezaji aliyefunga mabao mengi katika timu anayofundisha katika ligi ya mabingwa Ulaya zaidi ya Messi.

Uhusiano wao wa muda mrefu na Messi uliokuwa wa mafanikio unaeleza tosha kwanini Guardiola alijaribu kutaka kumsajili Messi msimu huu. Muargentina huyo mwishowe akatimkia Paris St-Germain na jumanne hii anakwenda kukabiliana na meneja wake huyo wa zamani kwenye mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya .

Mabadiliko yaliyoletwa na Guardiola tangu siku ya kwanza

Kikosi cha Barcelona kinachohaha sasa chini ya Ronald Koeman hakiwezi kukaribina hata kiduchu na kile kilichokuwa kikali na kinafanya vizuri chini ya makocha waliopita, hasa Guardiola aliyekuwa na muunganiko mzuri na Messi.

Guardiola alipandishwa kutoka kocha wa timu ya Barca B mpaka kufundisha kikosi cha kwanza mwanzoni mwa msimu wa 2008-09 na alikuwa msimu mzuri usiotarajiwa kwa kutwa makombe matatu.

Messi alifunga mabao 38 msimu huo na kufunga mabao 211 chini ya Guardiola, yakiwemo 73 katika mechi 60 katika msimu wa 2011-12, ambao ulikuwa msimu wa mwisho wa mhispania huo kufundisha Barcelona.

Kwa pamoja wametwaa mataji matati ya ligi kuu ya Hispania 'La Liga', mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya - wakiifunga Manchester United katika fainali zote mbili - mawili ya Copas del Rey, matatu ya Super Cups, mawili ya Uefa Super Cup na mawili mengine ya Fifa Club World Cup.

"Pep mara moja akaleta mabadiliko makubwa ya hamasa na viwango vyetu uwanjani, malengo na kiu ya kufanya vizuri," alisema Messi

"Tulimuamini tangu siku ya kwanza kwa sababu tuliona mambo yalikuwa yakienda sawa sawa na baadae, matokeo yalipoanza kuja, kujiamini kuliongezeka."

Kwa namna gani Messi amekuwa mwiba kwa Pep

Wawili hawa wanakutana Jumanne hii katika mchezo wa makundi wa ligi ya mabingwa Ulaya unaochezwa huko Paris.

Huko nyuma, mchezaji huyo aliyetwaa tuzo sita za mchezaji bora wa mwaka 'Ballon d'Or', hakuwa na masihara.

Muargentina huyo alifunga mabao 6 katika mechi nne za ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya timu zinazofundishwa na Guardiola - ni mabao mengi zaidi kufungwa na mchezaji mmoja katika mashindano hayo dhidi ya meneja wa sasa wa Manchestesr City.

Mei 2015, Messi alifunga mara mbili katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali na kuisaidia Barca kufika fainali nyingine ya ligi ya mabingwa kwa kuifunga Bayern Munich, wakati huo ikinolewa na Guardiola.

"Messi ni mchezaji hatari, ana nguvu, kasi, akiwa kwenye kiwango chake bora kama nilivyokuwa namfundisha," alisema Guardiola. "Ni mchezaji bora wa kwati wote. Namfananisha na Pele.

"Najivunia miaka yote tuliokuwa pamoja."

Messi ametwaa kombe la mwisho la ligi ya mabingwa Ulaya kati ya manne yaliyopita mwaka huo, wakati Guardiola hajatwaa kombe lolote la michuano hiyo bila Messi, msimu uliopita alikaribia kutwaa lakini timu yake ya City ikalala dhidi ya Chelsea katika fainali.

Mara ya mwisho wawili hao kukutana ilikuwa mwaka 2016 kwenye hatua ya makundi wakati Messi alipofunga mabao matatu 'hat-trick' katika ushindi wa 4-0 katika uwanja wa Nou Campna kufunga bao 1 katika kichapo walichokipata pale Etihad cha mabao 3-1

Je Messi anahaha kuzoea mazingira PSG?

Messi hajafanikiwa kufunga katika michezo mitatu aliyoichezea PSG

Yaliyotokea wakati wa usajili hakuna aliyefikiria. Baada ya Barca kushindwa kukidhi vigezo vya kanuni na sheria za matumizi ya fedha ya Laliga, Barcelona ilishindwa kumuongezea mkataba mpya Messi, akatimka Nou Camp.

Alihusishwa na mipango ya kuungana na Guardiola pale City lakini badala yake akajiunga na PSG chini ya kocha Mauricio Pochettino kwa uhamisho huru na kutengeneza safu inayotajwa kuwa hatari ya ushambuliaji akiwa na mshindi wa kombe la duiani, mfaransa Kylian Mbappe na nyota wa Brazil Neymar.

Baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, hasimu wake Cristiano Ronaldo nae aliondoka Juventus na kurejea Manchester United na mreno huyo tayari amekishaifungia timu hiyo ya ligi kuu England mabao 4.

Messi mwenye miaka 34, amekuwa na mwanzo wa hovyo I Ufaransa, utimamu wa mwili na majeraha yakimfanya kucheza michezo mitat tu, akicheza kwa dakika 90 mcheo mmoja tu, huku akiwa bao ajaweza kufumania javu.

Aliingia katika dakika 25 za mwisho Agosti 25 dhdi ya Rens kabla ya mchezo mwingine ambapo PSG walikwenda sare ya kushangaza ya 1-1 dhidi ya Club Bruges katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Ulaya uliopigwa Septemba 15.

Siku nne baada Messi alitolewa katika dakika ya 76 na kocha wake Pochettino, huku wachezaji wengi waliokuwa kwenye benchi la akiba wakihoji uamuzi wa kocha huyo.

"Aligongesha mwamba mara mbili dhidi ya Bruges na Lyon. Etimenta chache tu, angekuwa amefunga mabao mawili mazuri," Mchambuzi wa sokal a Ufaransa Julien Laurens ameiambia BBC.

"Tofauti na Cristiano, kurejea kwenye klabu yake ya zamani anayoijua, Kwa Messi - kila kitu kipya - itamchukua muda kuzoea. Haiwezi kuwa hivyo mara moja- kwamba safu ya ushambuliaji ya wakali watatu wakaanza kusumbu, kuna kazi ya ziada pia inapaswa kufanywa na Pochettino.

Mtaalam mwingine wa sola la Italia James Horncastle aliongeza: "Man City ni sehemu sahihi kwa Messi kufungua mapia lake la mabao. Pengine hatima ilikuwa ni dhidi ya Pen, dhidi ya Man City."