Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 09.09.2021: Lewandowski, Rice, Rudiger, Bellingham, Messi, Ozil, Kessie

Antonio Rudiger

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Antonio Rudiger
Iliyochapishwa

PSG wanamtaka mlinzi wa Ujerumani wa miaka 28- Antonio Rudiger, ambaye mkataba wake na Chelsea umesalia na chini ya mwaka mmoja kumalizika. (Le10Sport - in French)

Robert Lewandowski

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lewandowski ameshinda kombe la Ligi ya Ujerumani mara mbili mbili msimu uliopita pamoja na Champions League akiwa Bayern Munich

Real Madrid watamsaka mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, ikiwa watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland,21, kutoka Borussia Dortmund msimu ujao. (AS - in Spanish)

Manchester United wamemtambua mchezaji wa kimataifa wa England na West Ham Declan Rice, 22, kama chaguo lao la kwanza dirisha la uhamisho litakapofunguliwa majira ijayo ya kiangazi. (Manchester Evening News)

Declan Rice (right) celebrates an England goal against Iceland in a Nations League game at Wembley

Chanzo cha picha, Rex Features

Real Madrid na klabu kadhaa za Ligi ya Primia zinamfuatilia kwa karibu mchezaji wa Fulham Fabio Carvalho, 19. Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ureno, ana chini yam waka mmoja katika mkataba wake kabla ya kuondoka uwanja wa Craven Cottage. (Mail)

Borussia Dortmund wamekubaliana juu ya mkataba mpya na kiungo wa kati England Jude Bellingham,18, na hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo msimu ujao licha ya kwamba ananyatiwa na klabu kadhaa za Ligi ya Primia. (90Min)

Lionel Messi,34, amesisitiza kuwa mkataba wake na klabu ya Paris St-Germain inajumuisha kifungu ambacho kitamwezesha kuipatia kipaumbele uwakilisha wa Argentina kimataifa badala ya kuichezea klabu hiyo kuelekea michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujayo nchini Qatar. (Sport - in Spanish)

Lionel Messi posing with his PSG shirt

Chanzo cha picha, PSG

Barcelona italazimika kuilipa Liverpool kima cha euro milioni 20 (£17.1m) kama marupurupu ya ziada ikiwa mchezaji nyo wa Philippe Coutinho,29, ataiwakilisha zaidi ya mara 100 klabu hiyo ya La Liga. Mchezaji huyo amecheza mechi 90 za Barca tangu alipojiunga nao kutoka

Uhamisho wa mkopo wa kiungo wa kati wa Leicester Nampalys Mendy,29, kwenda Galatasaray umegonga mwamba kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal hawezi kufika Istanbul kabla ya dirisha la uhamisho la Uturiki kufungwa. (Foot Mercato via Get French Football News)

Franck Kessie huenda akaondoka AC Milan mwezi Januari mwakani baada ya kiungo huyo wa kati wa Ivory Coast aliye na miaka 24, kukataa ofa ya mkataba wa thamani ya euro milioni 6.5 kwa mwaka kutoka kwa klabu hiyo ya Serie A. (Tuttosport - in Italian)

Ivory Coast's Franck Kessie

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Franck Kessie huenda akaondoka AC Milan mwezi Januari baada ya kukata ofa ya mkataba mpya

Liverpool ni miongoni mwa klabu zinazomtaka Kessie, ijapokuwa Milan huenda ikatafuta mkataba wa kubadilishana wachezaji, ikizingatiwa kwamba kiungo wa kati wa klabu hiyo ya Ligi ya Primia na Uhispania Thiago Alcantara, 30, anahamia San Siro. (Il Milanista - in Italian)

Mlinzi wa zamani wa Arsenal David Luiz, 34, anapania kurejea nyumbani kwao Brazil baada ya kupuuza ombi la Marseille. (Le10Sport - in French)

Mchezaji mwingine wa zamani wa Arsenal, Mesut Ozil, 32, ananyatiwa na klabu kadhaa za MLS na Qatar baada ya mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Ujerumani kumalizika Fenerbahce. (AS - in Spanish)