Messi PSG: Fahamu jinsi Qatar itakavyonufaika na usajili wa nyota huyo

Chanzo cha picha, Reuters
Chini ya wiki moja iliyopita karibu kila mtu alichukulia kama kawaida kwamba Lionel Messi ataendelea kuiwakilisha Barcelona. Lakini mambo yamebadilikana nyota huyo wa kimataifa sasa ni mchezaji mpya wa PSG (Paris Saint-Germain).
Usajili wa Messi ni nyongeza isiyo na shaka katika klabu ya PSG, ambayo tayari ilikuwa na timu kali ya wachezaji nyota kama Neymar, Kylian Mbappé, Ángel Di María, Sergio Ramos au kipa aliyesajiliwa hivi karibuni Gianluigi Donnarumma, ambaye alishinda Kombe la Euro mwaka mmoja uliopita na mwezi moja uliopita na Italia.
Kwenye karatasi, hakuna klabu ya soka Barani Ulaya ambayo inaweza kuiga uwezo huu sasa wa PSG.
Lakini kutua kwa Messi mjini Paris kuna umuhimu mkubwa zaidi ya michezo.
Wataalam wanasema kwamba kusajiliwa kwa Messi, huenda ni muhimu zaidi na upatanishi katika historia ya kisasa ya mchezo huu, ni sehemu ya mkakati wa kisiasa ya Qatar.
PSG inamilikiwa na Uwekezaji wa Michezo wa Qatar (QSi), kampuni tanzu ya Mamlaka ya Uwekezaji ya Qatar, mfuko huru wa uwekezaji ambao Mkurugenzi Mtendaji wake ni Qatar Emir Tamim bin Hamad Al Zani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakosoaji wanashutumu kuwa PSG ni kilabu inayoungwa mkono na utajiri wa mafuta wa Qatar.
Na mashirika kadhaa wanailaumu nchi hiyo kwa kujificha nyuma ya uwekezaji wa michezo mikubwa kama vile kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022, kuficha mienendo yake ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Lakini usajili wa Messi unaingiliana vipi na siasa ya kubadli taswira ya nchi hiyo ndogo?
Usajili ambao "haungeepukika"
Baada ya Messi kuthibitisha kwamba anaondoka Barcelona, uvumi ulianza kuzagaa mitandaoni kwamba atajiunga na Manchester City au PSG.
Uvumi huo haukushughulikia tu nguvu kubwa ya kiuchumi ya timu zote mbili, bali pia na mantiki ya biashara kwamba kwa PSG ilisaidia kusawazisha usawa.
"Ukiangalia uhusiano wa miaka ya hivi karibuni kati ya Qatar, Barcelona, Paris na Messi, usajili wake ulikuwa jambo ambalo halingeepukika. Na Qatar iliamini kwamba hatimaye hilo litatokea," alisema Simon Chadwick, profesa wa siasa za kimataifa na uchumi wa kimichezoni kutoka Shule ya Biashara ya EM Lyon huko Ufaransa.

Chanzo cha picha, Aurelien Meunier - PSG
PSG ilitenga mabilioni ya kununua wachezaji katika miaka ya hivi karibuni wakiwa na lengo moja tu la kushinda Ligi ya Mabingwa, michuano inayoheshimika sana barani Ulaya. Lakini bado klabu hiyo haijafanikiwa kushinda.
Mwaka 2020 walikaribia fainali lakini waliondolewa katika michuano hiyo na Bayern Munich.
Mchezaji aliyekuwa akiangaziwa sana na vyombo vya habari kabla ya kuwasili kwa Messi alikuwa nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar, ambaye klabu hiyo ilimnunua kwa takriban Euro milioni 220 sawa na (Dola milioni 257) kutoka Barcelona mwaka 2017.
Hakuna uhamisho uliokuwa ghali namna hiyo katika historia ya soka.

Chanzo cha picha, Getty Images
PSG imekuwa ikitafuta ushindi wa Ligi ya Mabingwa kwa udi na uvumba.
"Qatar inataka PSG kushinda Ligi ya Mabingwa mwakani. Ikiwa watashinda mnamo Mei (2022), alafu Novemba mwaka huo huo Qatar itaandaa Kombe la Dunia. Hii itakuwa sifa ya kitaifa na faida za sifa hizo ni sehemu ya mkakati wa Qatar, "anasema Chadwick.
Mkakati wa "kujitakasa kimichezo"
Mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu, kama Human Rights Watch yameilaumu Qatar kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wahamiaji, ''swala ambalo limekuwa kubwa katika ujenzi wa viwanja vya kisasa vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya michuanio ya Kombe la Dunia mwaka 2022, Nchi hiyo pia imelaumiwa kwa "kuendelea kuwabagua wanawake na wapenzi wa jinsia moja ".
Mnamo mwezi Machi, shirika la kimataifa la kutetea haki Amnesty International iliiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Soka Duniani( FIFA) kutaka "hatua madhubuti na za dharura kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa mashindano hayo yanaacha matokeo chanya na ya kudumu kwa wafanyikazi wote wahamiaji nchini Qatar na kuhakikisha haisababishi unyanyasaji zaidi wa wafanyikazi"
Mbali na madai haya, pia kuna madai ya kuhonga ili kushinda kura na wawakilishi wa Qatar kwa wanachama wa FIFA.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kufuatia tuhuma hizo, wakosoaji sasa wanaishutumu Qatar kwa kujaribu kusafisha taswira yake ya kimataifa kupitia mkakati unaojulikana kama "kujitakasa kimichezo''.
"Badala ya kuzungumzia uhamiaji, hali ya kazi na jinsi Qatar inavyoshughulikia jamii yake ya LGTBQ, tunazungumza juu ya Lionel Messi, PSG na mpira wa miguu. Huu bila shaka ni mkakati wa kuvuruga watu na sio wa kuzungumzia mambo muhimu zaidi" , alisema Profesa Chadwick.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo mwaka wa 2017, mamlaka ya Qatar ilipitisha sheria mpya za kuboresha haki za wafanyikazi baada ya kufikia makubaliano na Shirika la Kazi la Kimataifa la Umoja wa Mataifa.
Ingawa wakati huo, taarifa ya serikali ilielezea kuwa mageuzi haya "yatachukua muda, rasilimali na kujitolea."
Kulingana na Chadwick hakuna shaka kwamba : PSG ni klabu ya nchi na "Qatar haiwezi kupinga."
"Umiliki wa klabu hiyo uko mikononi mwa QSi ambayo inahusishwa na hazina ya fedha zinazotokanaa utajiri wa Qatar.
Rais wa QSi, Nasser al Khelaifi, ni jamaa wa familia ya kifalme ya Qatar na pia ni mwenyekiti wa PSG. "
"Qatar haina demokrasia. Familia ya kifalme ndi serikal. hakuna mjadala: nchi ya Qatar inaamiliki PSG, "aliongeza kusema mtaalamu huyo.














