Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ligi Kuu ya Ulaya: Kwa nini kuziadhibu klabu hizi 12 kunaweza kuwa wazo baya
Ulimwengu wa soka umeshtushwa na tangazo la uanzishwaji wa ligi kuu ya bara Ulaya.
Wengi wanafikiria kwamba ni wazo baya kwa shirikisho la soka duniani FifA na lile la bara Uropa la UEFA na hadi kwa ligi kama ile ya PrImia na shirikisho la soka nchini Uhispania.
Wazo hilo pia linaonekana baya kwa makundi ya mashabiki wa timu sita kuu katika ligi ya England - Liverpool, Manchester City, Man United, Chelsea, Tottenham na Arsenal.
Klabu nyingine sita ni Barcelona, Real Madrid na Atlético de Madrid za Uhispania; na Juventus, AC Milan na Inter , nchini Italy.
Chini ya mfumo uliopendekezwa , klabu hizi 12 zitaungana na klabu nyengine tatu anzilishi ambazo hazijathibitishwa na klabu nyengine tano ambazo zitalazimika kufuzu kila mwaka.
Zitacheza mechi za katikati ya wiki katika ligi mbili za timu 10 na klabu hizo kuu na kuelekea katika makundi ya muondoano na hatimaye kucheza fainali kila mwezi Mei.
Ili kuchukua mahala pa ligi ya mabingwa Ulaya, waanzilishi kwa pamoja watakusanya dola 4.22 bilioni kupitia malipo ya miundo mbinu pamoja na Euro 3.5 billion za uwajibikaji.
"Klabu hizo 12 zinapendekeza kushindana katika ligi zao za kitaifa kama kawaida.
Mpango huo unaonekana mbaya hadi Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameapa kutafuta njia ya kuuzuia licha ya kujulikana kuwa mapenzi mkuu wa soka.
Wataalamu ikiwemo Gary Neville , mchezaji wa zamani wa Man United wote wamevunjwa moyo.
Ligi hiyo ya Superleague Ulaya inaonekana kama njia ya kujipatia fedha , kwasababu itakuwa biashara ambayo klabu anzalishi hazitalazimika kushushwa daraja.
Wengi wanahisi ni kinyume na historia ndefu ya soka hususan na ligi za chini zinazojikwamua kutokana na athari za mlipuko wa corona.
Neville anaamini kwamba hakuna fursa na kwamba hilo litatekelezwa licha ya upinzani mkubwa.
Nchini England, wengi wanataka mamlaka ya soka duniani kuadhibu klabu hizo sita.
Kuzipiga marufuku ni adhabu inayofikiriwa na wachezaji wa klabu hizi ili kushindana katika michuano ya Ulaya katika kombe la Dunia.
Hasira ya mashabiki
Hatahivyo kila mtu anapaswa kupumua na kufikiria kwasababu kuchukua hatua kali dhidi ya klabu hizi kunaweza kutoa athari tofauti.
Inaweza kuwa vigumu kwa mamlaka ya Ligi ya Primia kuungwa mkono na mashabiki kwa kwenda kinyume na historia ya kandanda.
Ligi ya Primia ilijiondoa katika ligi ya England mwaka 1992 na mamlaka ya kandanda na mashabiki walikuwa na hasira kali wakati huo.
Huku idadi kubwa ya mapato ya matangazo ya ligi ya Primia yakienda katika klabu za ligi ya Primia , wengi katika soka tayari wanakosoa hatua hiyo.
Wanahoji kwamba fedha zinazofikia ligi za chini ni chache mno , huku mfumuko kwa miaka mingi katika dau la uhamisho wa wachezaji na mishahara ukisukuma klabu nyingi kushindwa kujisimamia hata kabla ya mlipuko wa corona.
Je ni kipi kitakachofanyika baadaye?
Ligi inayopendekezwa ya Super League inaweza kutumika kuleta majadiliano.
Klabu kuu kwa muda mrefu zimekuwa zikitaka mabadiliko katika kombe la klabu bingwa ambayo yatazifaidisha kifedha na ukweli kwamba tangazo hili linajiri siku moja kabla ya UEFA kuthibitisha uandikishaji upya wa mkataba sio swala la kushangaza.
Kuongeza mechi katika kalenda ya soka isiyo na nafasi sio kitu ambacho klabu yoyote kuu inahitaji.
Hivyobasi mpango wa kupendekeza ligi ya Superleague pengine huenda ukatoweka katika siku chache zijazo baada ya UEFA kuamua kuchukua jukumu.
Kama Neville anavyozungumza , kitu kama hicho kilitokea katika ligi ya Primia mwaka 2020 ambapo kulikuwa na mpango wa kutaka kuimarisha klabu kuu kwa jina ''Project Big Picture''.
Upande mwingine klabu kuu huenda zikatafuta jibu baya kutoka kwa mamlaka ya kandanda ili kuweza kusonga zaidi.
Pengine ligi iliyo huru huenda ndio kile ambacho wamiliki wanafikiria, badala ya ligi ya kila wiki inayoenda sambamba.
Sio Klabu ni Biashara
Mtindo unaopigiwa upatu ni ule wa michezo wa Marekani kama vile Mpira wa kikapu , ambapo timu husafiri maelfu ya maili ili kucheza.
Wanaandaa mechi ughaibuni katika viwanja vya kando , na kuzipeleka timu katika miji tofauti bila kujali jinsi mashabiki wa nyumbani watakavyopokea wageni.
Suala la kwamba wamiliki wao huchukulia klabu hizo kama biashara ni funzo .
Nne kati ya klabu zilizopendekezwa kama klabu anzilishi za Super league zina wamiliki Wamerakani ambao hawana hamu ya kandanda isipokuwa utajiri wa faida yao.
Tunaweza kufikiria kwamba wamiliki wa klabu hizi wanawaza kwamba kundi la timu 20 barani Ulaya linaweza kufyonza fedha zote kutoka kwa mapato ya matangazo ya kandanda na ufadhili.
Timu zenu zinaweza kucheza mara kadhaa kwa mwaka na kwanini zisichezee katika mji wa Madrid ama debi za City kutochezwa katika uwanja wa uliojaa mashabiki mjini Rio Shanghai au Los Angeles?
Kwanini muweke klabu za Uropa pekee ikiwa munaweza kuongeza klabu za Amerika ya kusini , Marekani na China. Ili kukabilinaa na tishio hilo, serikali na ligi za taifa ni sharti zijumuishe timu zote 12 katika michuano.
Fursa tofauti za kubadilisha ligi ya Klabu bingwa na kuhakikisha kwamba soka katika viwango vyote inaweza kujikimu inaweza kupotea.
Kwa sasa inaonekana kwamba klabu zinatumaini ya kupata jibu kwa swali hili.