Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 26.07.2020: Havertz, Bielsa, Wilson, Koulibaly, Maddison

Iliyochapishwa

Chelsea wanamatumaini kwamba kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen Kai Havertz mwenye umri wa miaka 21 atajiunga na Mjerumani mwenzake Timo Werner na kuwa mchezaji mkuu wa tatu kusaini mkataba na klabu hiyo msimu huu hatakama hawatafuzu kwa Championi Ligi mwaka ujao. (Mail on Sunday)

Mchezaji maarufu wa Barcelona Lionel Messi ameiambia klabu hiyo kwamba meneja wa Leeds Bielsa anapaswa kuwa ndiye mtu atakayechukua nafasi ya Quique Setien na kuwa kocha mpya katika Nou Camp. (Sun on Sunday)

Crystal Palace wanamlenga meneja wa Burnley -Sean Dyche kama meneja wao ajaye, huku hali ya baadae ya Roy Hodgson ikiwa mashakani baada ya utendaji wake mbovu . (Sunday Mirror)

Tottenham Hotspur wanaongoza katika katika mbio za kumfukuzia mshambuliaji wa Bournemouth Muingereza Callum Wilson. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anaweza kupatikana kwa pauni milioni 10. (Sun on Sunday)

Mkurugenzi wa michezo wa Napoli Cristiano Giuntoli anasema hakuna timu ambayo inamtaka kiungo wa kati- nyuma Kalidou Koulibaly licha ya kuongezeka kwa tetesi kwamba Manchester City, Manchester United, Liverpool na Barcelona zote zinamtaka mchezaji huyo mwenue umri wa miaka 29-year siku zijazo (Goal)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer yuko tayari kuchukua hatua za mwisho za kuvuruga nia ya Napoli ya kumchukua Mbrazili anayechezea Lille anayechezatimu ya Brazili ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 mlinzi Gabriel Magalhaes, 22. (Sunday Express)

Kiungo wa kati wa Leicester James Maddison, mwenye umri wa miaka 23, amekataa nia ya Manchester United ya kumtaka aingie kikosini na badala yake akasaini mkataba mpya na wa muda mrefu na Foxes ambao unaaminiwa kuwa wa thamani ya pauni £95,000 kwa wiki. (Talksport

Sintofahamu juu ya ya baadae ya kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, mwenye umri wa miaka 27, imeifanya klabu ya Manchester United kujiuliza maswali juu ya uhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, na Jack Grealish mwenye umri wa miaka 24 wa Aston Villa. (Mail on Sunday)

Arsenal wataweza tu kusiani mkataba na kiungo wa kati wa Atletico Madrid Thomas Partey msimu huu kama watamlipa mchezaji huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 27 pauni milioni 45 ya kipengele cha kumuachilia kamili . (Sunday Express)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Toni Kroos anasema hali ya mchezaji mwenzake Gareth Bale katika klabu hiyo sio nzuri kwa mtu yeyote na raia huyo wa Wales alikasirika baada ya hatua yake ya kuhamia China kuzuiwa msimu uliopita. (Goal)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa hatuatakuwa na shughuli nyingi za wa wachezaji katika msimu wa dirisha la uhamisho, akisema kuwa hawezi kamwe kuharibu hali iliyopo ya uwiano na utulivu wa kikosi chake kwa kuwa na wachezaji wengi kupita kiasi. (Sunday Mirror)

Manchester United wanamfuatilia kwa karibu mlindalango aliyethamanishwa na Atletico Madrid kwa pauni milioni Slovenia Mslovania Jan Oblak, mwenye umri wa miaka 27, kama mchezaji mbadala wa mhispania David de Gea lakini Chelsea wanamtaka (Sun on Sunday)

Inter Milan wanaangalia uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa Manchester United raia wa Chile, Alexis Sanchez kwa mkataba wa kudumu na mkataba wake wa mkopo unatarajia kumalizika mwezi ujao wake (Sky Sports Italia via Sunday Mirror)

Arsenal, West Ham na Everton wote bado wana nia ya kusaini mkataba na difenda wa Barcelona Mfaransa Samuel Umtiti, 26, kwa deni. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Serie B side Benevento wanataka kumsaini mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na England Daniel Sturridge, mwenye umri wa miaka 30, kwa uhamisho wa bila malipo. (Mail on Sunday)

Valencia wanajiandaa kumnunua kipa wa Chelsea na Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, pamoja na mchezaji nyota wa Manchester City Mhispania David Silva, 34. (90min)

Winga wa Bayern Munich Leroy Sane, 24, amemsihi beki wa Austria David Alaba, 28, kusalia katika klabu hiyo badala kurejea tena katika klabu yake ya zamani Manchester City, ama kwenda Real Madrid. (Sport Bild, via Independent)