Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 30.04.2020: Reguilon, Pochettino, Sane, Sancho, Ndombele, Pedro, Edouard
Arsenal wameripotiwa kuwasiliana na Real Madrid kuhusu uhamisho wa beki wa Uhispania Sergio Reguilon, 23, ambaye yupo Sevilla kwa mkopo. (ABC, via Star)
Mauricio Pochettino ni chaguo la kwanza la mmiliki mtarajiwa wa Newcastle kuchukuwa nafasi ya mkufunzi Steve Bruce na wako tayari kumlipa £19m kwa mwaka. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Bayern Munich Hansi Flick amefanya mazungumzo ya simu ya dakika 30 na winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, kujadili uwezekano wa uhamisho wake. (Bild, via Goal - in German)
Winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, amepewa ofa ya nafasi saba na Manchester United katika juhudi za kumshawishi ajiunge na klabu hiyo. (Mirror)
Kiungo wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23, anatathmini hatima yake ya baadae katika klabu ya Tottenham, huku Barcelona wakimmezea mate. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Roma Paulo Fonseca anataka kumsajili winga wa Chelsea na Uhispania Pedro, 32. (Corriere dello Sport - in Italian)
Arsenal wameambiwa lazima walipe zaidi ya £25m ikiwa wanataka kumnunua mshambuliaji wa Celtic na Ufaransa Odsonne Edouard, 22. (Express)
Mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens, 32, anataka kuhamia London, huku Chelsea ikiwa bado inamnyatia kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Mail)
Leicester inataka kumsajili beki wa Saint-Etienne Mfaransa Wesley Fofana, 19. (Le10 Sport - in French)
AC Milan huenda ikamuuza kipa wa zamani wa Uhispania Pepe Reina, dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Kipa huyo wa miaka 37- sasa yupo kwa mkopo Aston Villa. (Calciomercato)
Nigel Pearson atasalia kama mkufunzi wa Watford, hadi mwisho wa msimu licha ya kuwa mkataba wake unamalizika mwezi Mei. (Sky Sports)
Arsenal ina mpango wa kufanya uhamisho wa bure na mkataba wa kubadilishana wachezaji dirisha la uhamisho litakapofunguliwa msimu wa joto kutokana na changamoto za kifedha zilizochangiwa na janga la corona. (Mail)
Kiungo wa kati wa Chelsea Itali Jorginho, 28, amedokezea uwezekano wake kuondoka klabu hiyo baada ya kuchezea Blues kwa msimu mmoja kutokana na ukosoaji unaomkabili kutoka kwa mashabiki. (FourFourTwo)
TETESI ZA SOKA JUMATANO
Manchester United huenda wakalazimika kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, kwa bei ya chini kutokana na athari za janga la corona katika mchezo wa soka. (Goal)
Arsenal watamuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa dau la £30m kwasababu hawataki aondoke klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo. (Sun)
Gunners bado haijampatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 31. (ESPN)
West Ham inatarajiwa kukataa ofa iliyowasilishwa na Chelsea ya kumnunua kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21. (Goal)
Newcastle na Everton wanang'ang'ania saini ya kiungo wa kati wa Ajax na Netherlands Donny van de Beek. Manchester United na Real Madrid pia wamehusishwa na nyota huyo wa miaka 23. (Le10 Sport - in French)
Everton wamempatia ofa ya mkataba wa miaka minne kiungo wa kati wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Arsenal na Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Monaco na Ufaransa Wissam Ben Yedder, 29. (L'Equipe - in French)
Everton imefanya mazungumzo na Barcelona kumhusu beki wa miaka 20 Jean-Clair Todibo. Kinda huyo wa Ufaransa sasa yupo Schalke kwa mkopo. (Mail)
Liverpool imeanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Lille na Nigeria Victor Osimhen, 21. (Le10 Sport - in French)
Newcastle wanapania kumbadilisha mkufunzi wao Steve Bruce with Flamengo na Jorge Jesus, ambaye aliongoza klabu hiyo ya Brazil mwaka 2019 kushinda taji la Copa Libertadores. (Goal)
Arsenal italazimika kuilipa Real Madrid euro milioni 50 sawa na (£44m) wakitaka kumsaini kwa mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, ambaye anachezea klabu hiyo kwa mkopo. (AS - in Spanish)
Arsenal wanajizatiti kumzuia winga wao wa miaka 18, Bukayo Saka anayenyatiwa na klabu zingine za Ligi ya Primia asiondoke, kwa kumpatia mkataba mpya. (90min)
Chelsea wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Paris St-Germain Mfaransa Kays Ruiz-Atil,17, ambaye mkataba wake unamalizika 2021. (L'Equipe - in French)
TETESI ZA SOKA JUMANNE
Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, na kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 27, kumnunua Sancho. (Sun)
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund anasema "amenyamaza " kuhusu hatma ya baadae ya Jadon Sancho. Winga huyo wa England, 20, amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United. (Sport1 - in German)
Mshambuliaji wa Everton Moise Kean, 20, amehusishwa na tetesi za kuhamia Napoli.
Mtaliano huyo huenda akachukuliwa hatua za kinidhamu na Everton kwa kukiuka muongozo wa serikali wa kukabiliana na coronavirus mapema wiki hii. (Corriere dello Sport - in Italian)
Wachezaji nyota wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, na Ousmane Dembele, 22, wako tayari kujumuishwa kwa mkataba wa kubadilishana wachezaji msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Chelsea walimtaka Coutinho lakini sasa wanamnyatia kiungo matata wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 20. (Athletic - subscription required)
Arsenal wamewasilisha ofa ya £43m kumnunua kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ghana Thomas Partey, 26. (Express)
Liverpool wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Lille Victor Osimhen, 21, ijapo kuwa Leicester na Chelsea pia wanamng'ang'ania raia huyo wa Nigeria . (Le Foot Mercato - in French)
Arsenal wamekosa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United wa miaka 15 Omari Forson kwa mkataba wa kitaalamu. (Mail)
Manchester United wamehusishwa na uhamisho wa beki wa Real Valladolid na Ghana Mohammed Salisu, 21. (AS - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Leicester Wilfred Ndidi amesema anafurahia sana uwepo wake katika klabu hiyo, licha ya tetesi zinazomhusisha Mnigeria huyo wa miaka, 23, na uhamisho wa Manchester United ama Arsenal. (Teamtalk)
Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, amesema ana matumaini ya kurejea Real Madrid mkataba wake wa Mkopo wa msimu mzima Arsenal utakapomalizika. (Movistar - in Spanish)
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa amesema mkufunzi wake wa zamani wa Chelsea Antonio Conte huenda "asidumu" msimu mzima katika klabu kama Real Madrid. Conte amekuwa mkufunzi wa Inter Milan tangu Mei 2019. (ESPN)
Mkufunzi wa zamani wa Tottenham na Chelsea Andre Villas-Boas amesema hatarudi tena katika Ligi ya Premier. (Mail)
Mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min huenda akakosa mazoezi ya Ligi ya Primia. Raia huyo wa Korea Kusini, 27, ambaye yuko nyumbani kwa huduma ya kitaifa atalazimika kujitenga atakaporudi. (Evening Standard)
TETESI ZA SOKA JUMATATU
Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, ambaye yuko kwa mkopo Bayern Munich, aliambiwa na Liverpool kuwa hawana mpango wa kumsajili tena mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil wa miaka 27- walipokuwa wanajadili uwezekano wake kurejea katika klabu hiyo. (Mirror)
Arsenal wamejiondoa katika mazungumzo ya mkataba wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang. Kiungo huyo wa kimataifa wa Gabon mwenye umri wa miaka 30-anatarajiwa kuondoka katika uwanja wa Emirates, huku klabu za Manchester United, Inter Milan, Barcelona, Real Madrid na Chelsea zikitaka kumsaini. (Mirror)
Kipa wa Manchester United, Mhispania David de Gea,29, amesema kuwa anataka kusalia Old Trafford kwa "miaka mingi" lakini nafasi yake inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Muingereza Dean Henderson, 23, ambaye ameonesha umahiri wake baada ya kusajili kwa mkopo kutoka Sheffield United. (Mail)
Ajenti wa zamani wa Neymar, Wagner Ribiero amesema mshambuliaji huyo wa Brazil na Paris St-Germain, 28, alitaka kujiunga na Chelsea alipokuwa na miaka 17. (Mail)
Beki wa Paris St-Germain na Ubelgiji Thomas Meunier "ameshawishiwa" na mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho kuhusu uhamisho wa msimu wa joto, lakini kiungo huyo wa miaka 28- huenda akapewa mkataba mpya Parc des Princes. (L'Equipe, via Teamtalk)
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard amezungumza na mshambuliaji wa Napoli Dries Mertens na anatarajia kumpata kiungo huyo wa Ubelgiji wa miaka 32, kwa uhamisho wa bure. (Mail)
Beki wa Uholanzi Jetro Willems, 26, amedokeza kuwa anataka kuhamia Newcastle kwa mkataba wa kudumu baada ya kuchezea klabu hiyo mwanzo wa msimu kutoka Eintracht Frankfurt kabla ya kujeruhiwa. (Goal)
Chelsea watamkosa kipa wa Ajax Andre Onana kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon anajiandaa kurejea Barcelona. (Express)