Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 04.04.2020: Varane, Costa, Bale, Coutinho, Kane

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabigwa wa Italian Juventus wako tayari kumuuza winga wao raia wa Brazil Douglas Costa, 29, kwa Manchester City kama sehemu ya makubaliano ya kuweza kumsajili Gabriel Jesus, 23. (Calcio Mercato, in Italian)
Real Madrid imejipanga kupuuza mapendekezo yoyote kutoka kwa Manchester City ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Raphael Varane, 26. (Star)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti ameanzisha mpango wenye uwezo mkubwa wa kuwashawishi kiungo wa kati wa Real Madrid Gareth Bale, 30, na James Rodriguez, 28, kuhamia Goodison Park. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea iko katika majadiliano na mchezaji raia wa Brazil Philippe Coutinho, 27, kuhusu usajili wa msimu ujao ambaye kwasasa yuko kwa mkopo Bayern Munich kutoka Barcelona. (Sun)
Manchester Unite wamearifiwa kwamba hawana tena fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane kwasababu ya kandarasi yake ya muda mrefu ambayo inamalizika 2024. (Manchester Evening News)

Mlinzi Matthijs de Ligt imejitokeza kwamba analengwa na Manchester United huku mshambuliaji huyo wa miaka 20, akisema kwamba ana wakati mgumu wa kumakinika Juventus. (Express)
Newcastle United bado haijakata tamaa katika kumsajili kiungo wa kati wa Lille, Boubakary Soumare, 21, licha ya kwamba Real Madrid pia nayo imeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo raia wa Ufaransa. (Sport, in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini Liverpool pia nayo inamfuatilia kwa karibu ikilenga kumsajili Soumare na tayari imeanza majadiliano. (Teamtalk)












