Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 23.11.2019: Haaland, Bale, Giroud, Eriksen, Suarez, Shaqiri

Iliyochapishwa

Manchester United, Arsenal na vilabu vingine vikuu vya ulaya huenda vikapigwa na butwaa kwasababu RB Leipzig itakuwa nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa Red Bull Salzburg wa miaka 19 Erling Braut Haaland kwa £25.7m pekee. (Sport Bild, via Sun)

Manchester United inasalia kuwa klabu inayomvutia Gareth Bale ikiwa ataamua kurejea katika ligi ya primia huku hatima ya nyota huyo wa kimataifa wa Wales wa miaka 30- katika klabu ya Real Madrid ikiwa haijulikani. (Talksport)

Crystal Palace inataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 33, lakini huenda masharti ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ikawa kikwazo ya wao kuafikiana. (Express)

Mchezaji wa safu ya kati Christian Eriksen, 27, huenda akaondoka Tottenham, licha yakuwasili kwa Jose Mourinho London kaskazini. (Mail)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anapania kumsajili beki wa Leicester City na Portugal Ricardo Pereira, 26, kuchukua nafasi ya Kieran Trippier ambaye amehamia Atletico Madrid. (Express)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich, amefutiliambali tetesi kwamba huenda akauza klabu hiyo, huku wanadani wake wa karibu wakisisitiza kuwa upendo wake kwa klabu hiyo imefufuliwa na mageuzi ya Frank Lampard. (Telegraph)

Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa RCSKA Moscow ya Urusi Fedor Chalov, 21, na itamnunua kiungo huyo mwezi Januari ikiwa marufuku dhidi ya klabu hiyo itaondolewa. (Mirror)

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Luis Suarez, 32, amekiri ''uwezekano'' wa kuhamia soka ya daraja la kwanza nchini Marekani. (ESPN)

Bayern Munich wanajiandaa kufanya mazungumzo na Mauricio Pochettino, 47, baada ya kufutwa na Tottenham Hotspurs wiki hii. (Metro)

Frank Lampard anasisitiza kuwa hatawahi kufuata mfano wa Mourinho kuongoza mahasimu wa Chelsea jiji ni London, Tottenham Hotspurs. (Times)

Meneja wa Arsenal Unai Emery ameshauriwa na shujaa wa zamani wa klabu hiyo Robert Pires kuwasajili zaidi wachezaji wa Uingereza. (Athletic via Mirror)

Mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema, 31, anatafakari ofa ya Real Madrid ya kurefusha mkataba wake kwa miaka miwili. (ESPN)

Mshambuliajiwa Real Mbelgiji Eden Hazard, 28,amefichua kuwa Paris St-Germain iliwahi kuwasiliana nae kuhusu suala la kutaka kumsajili, hatahivyo amesema kuwa atarejea Ufaransa kuchezea klabu yake ya zamani Lille. (L'Equipe - in French)

Borussia Dortmund inataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus wa miaka 25- Mjerumani Emre Can. (Bild - in German)

Manchester United inatarajia kulipwa zaidi ya £850,000 na Juventus kufikia mwisho wa msimu huu kama sehemu ya masharti ya uhamisho wa Cristiano Ronaldo kujiunga na miamba hao wa Italia. (mirror)

Ole Gunnar Solskjaer amebeza tetesi kuwa Nemanja Matic anajiunga na Tottenham Hotspur baada ya mchezaji huyo wa safu ya kati wa Manchester United, 31, kujibu katika mtandao wa kijamii ujumbe uliodokeza kuwa ana mpango wa kuungana na Jose Mourinho. (Metro)