Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Wachezaji waliosajiliwa dakika za mwisho England

Kandarasi zote mpya kabla ya dakika ya mwisho ya dirisha la uhamisho England

Moja kwa moja

  1. Leicester inakaribia kumsajili Dennis Praet

  2. Arsenal yakataa kumuuza Iwobi

    Everton wamekataa ombi la dau la £30m kumnunua winga wa Arsenal Alex Iwobi huku ofa ya mkopo ya beki wa Man United Chris Smalling pia ikikataliwa.

    Everton inatarajiwa kurudi na ofa ilioimarishwa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 lakini ofa hiyo italazimiuka kuwa zaidi ya £40m kukubaliwa.

    Iwobi hataki kuondoka lakini yuko tayari iwapo makubaliano yataafikiwa.

  3. Habari za hivi punde, Man City yamsajili Joao Cancelo kutoka Juventus

    Manchester City wamekamilisha usajili wa beki wa kulia wa Ureno Joao Cancelo kutoka Juventus kwa dau la £60m.

    Makubaliano hayo yatamfanya beki wa City Danilo, 28, kuhamia Juventus kwa dau la £34.1m.

    Cancelo, 25, ameweka kandarasi katika katika uwanja wa Etihad hadi 20125 na anakuwa mchezaji wa tatu kusainiwa na klabu hiyo baada ya Angelino na Rodri.

  4. Brighton yamsajili mchezaji wa PSG

  5. Newcastle yamsaini beki wa Sweden Emil Krafth

  6. Ubaguzi!

  7. Ubaguzi dhidi ya Mo Salah kuchunguzwa

    Chapisho la kibaguzi katika mtandao wa Twitter lililomlenga mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah linachunguzwa na maafisa wa polisi.

    Everton inachunguza iwapo ujumbe huo ulitumwa na mtumiaji wa Twitter ambaye ana uhuysiano na klabu hiyo.

  8. Sessegnon kuhamia Tottenham

    Tottenham wameafikia makubaliano na Fulham kumsaini beki wa kushoto wa Uingereza wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Ryan Sessegnon kwa dau la £25m.

    Makubaliano hayo yatafanya kiungo wa kati wa Tottenham Josh Onomah kuhamia Fulham.

    Dau hilo la Sessegnon , mwenye umri wa miaka 19 aliyefunga magoli mawili katika mechi 35 msimu uliopita akiichezea Fulham ilioshushwa daraja huenda ikapanda hadi £30m.

    Kwa kuongezea Spurs ilipendekeza kumsaini kiungo wa kati wa Real Betis na Argentina Givani lo Celso ambaye atahudumu kwa mkopo wakiwa na sheria ya kumununua kabisa.

  9. Habari za hivi punde, Lukaku kuhamia Juventus kwa dau la £ 74

  10. Je Mbwana Samatta atajiunga na EPL?

    Klabu ya Brighton inayocheza ligi ya Primia ya England inaongoza msururu wa klabu zinazomuwania mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta.

    Klabu nyengine za England ambazo zinamuwania Samatta ni Aston Villa, Watford, Leicester na Burnley.

    Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza Samatta ana thamani ya Pauni milioni 12.

    Samatta ambaye bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na mabingwa wa Ubelgiji KRC Genk pia amezivutia klabu za Roma ya Italia na Lyon ya Ufaransa.

    Mshambuliaji huyo ambaye aliongoza kwa kupachika mabao msimu uliopita nchini Ubelgiji ameweka wazi kuwa anataka kuelekea nchini England msimu ujao.

    "Kwa sasa hivi siwezi kusema sana, ni kitu ambacho kipo kwenye mchakato nasubiria kitakapokuwa tayari na wakati utakapofika nitaweza kukizungumza. Lakini sijioni tena Genk, namuomba Mwenyezi Mungu litimie, lakini ikishindikana bado nina mkataba na Genk," aliiambia runinga ya Azam TV ya Tanzania wiki iliyopita.

  11. Romelu Lukaku: Inter Milan waafikiana bei na Man United

    Inter Milan na Manchester United wameafikiana kuhusu usajili wa mshambuliaji Romelu Lukaku.

    Inter sasa itatoo kitita cha pauni milioni 74, dau ambalo Man United walikuwa wakilitaka toka awali.

    Lukaku amepigwa faini na United baada ya kukicha mazoezi ya timu hiyo bila ruhusa ya uongozi, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake kuchochea uhamisho.

    Mchezaji huyo amekuwa akifanya mazoezi na klabu yake ya zamani Anderlecht kwa siku mbili zilizopita.

    Ajenti wa Lukaku, Federico Pastorello, alilazimika kwenda jijini London jana ili kukutana na wawakilishi wa Man United ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.

    Usiku wa jana, Pastorello alituma picha katika mtandao wake wa Instagram akiwa kwenye ndege na Lukaku na kuandika maelezo yafuatayo: "Tayari kwa kupaa. Muelekeo Milano."

  12. Habari za hivi punde, Juventus wakataa kumuuza Dybala!

  13. Dybala kujiunga na Tottenham

  14. Habari za hivi punde, Dybala anakaribia kuandikisha mkataba na Tottenham

    Tottenham wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala .

    Makubaliano hayo hayajaafikiwa lakini Suprs wana matumaini ya kukamilisha makubaliano hayo kabla ya saa moja zaa za Afrika Mashariki.

    Spurs ilianza kumwania Dybala baada ya uhamisho wa kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes kufeli.

  15. Habari za hivi punde, Kieran Tierney kutia saini kandarasi ya miaka 5 Arsenal

  16. West Ham yamsaini ajeti

    West Ham wamekamilisha usajili wa dau la £8m la mchezaji mwenye umri wa miaka 22 raia wa Switzerland na mshambuliaji wa Albian Ajeti kutoka FC Basel.

    Ajeti alifunga magoli 15 katka mechi 35 akiichezea klabu hiyo ya Swiss msimu uliopita

  17. Habari za hivi punde, David Luiz ajiunga na Arsenal

    Arsenal imeafikia makubaliano na Chelsea kumsaini beki wa kati wa Chelsea David Luiz kwa dau la £8m.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 raia wa Brazil atatia saini kandarasi ya miaka miwili.

    Beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney naye atajiunga kwa dau la £25m, akitia saini kandarasi ya miaka mitano.

    Ukaguzi wa matibabu wa wachezaji wote wawili utafanyika hii leo kabla ya saa moja usiku ambayo ndio saa ya mwisho ya dirisha hilo la uhamisho.

  18. Neymar anaelekea Real Madrid?

    Uhamisho huu sio lazima ufanikiwe leo lakini huenda ukawa bora zaidi msimu huu.

    Neymar amehusishwa na uhamisho wa kurudi Bercelona lakini huenda Real Madrid wakashindana na mabingwa hao wa Uhispania kupata saini ya mchezaji huyo.

    Gazeti ,moja la Uhispania limeripoti kwamba Real iko tayari kuipatia PSG £ 110m pamoja na kiungo wa kati Luca Modric.

  19. Wayne Rooney kuwa mkufunzi mchezaji Derby

  20. Mandzukic kwenda Man United?

    Manchester United imerudia mazungumzo yake na mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic kutoka Juventus kuchukua mahala pake Romelu Lukaku kulingana na chombo cha habari cha Sky nchini Italy.