Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan

Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan

Moja kwa moja

  1. Neymar na Brazil watua Robo fainali, Mechi imemalizika ugani Samara: Brazil 2-0 Mexico

  2. Hata benchi la Brazil ni moto wa kuotea mbali!, 95' Brazil 2-0 Mexico

    Nguvu mpya Fernandinho alimtengeza Neymar, Neymar akafyatua kombora, kipa Guillermo Ochoa akagusa, lakini mwindaji Roberto Firmino hakuchelea kuihakikishia Brazil nafasi yake Robo fainali!

  3. Willian apumzishwa baada ya uhodari dhidi ya Mexico., 91' Brazil 2-0 Mexico

    Kiungo huyu wa Chelsea amekuwa kibarua kwa mabeki wa Mexico!

    Willian

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Willian
  4. Neymar amuona Firmino, 89' Brazil 2-0 Mexico

    ............na kumpa bao lake la kwanza Kombe la Dunia

  5. Firminnnnnnnnnnnnnooooo: hadi kimiani!, 88' Brazil 2-0 Mexico

  6. China ya dakika 2 zimesalia Samara, 86' Brazil 1-0 Mexico

    Brazil imeshiriki kila robo fainali tangu 1990.

    Mexico haijawahi kuvuka hatua ya mchujo tangu 1986.

  7. Mexico hawabanduki; Wabaki na matumaini, 86' Brazil 1-0 Mexico

    Kocha Juan Carlos Osorio bado anahisi kuna uwezekano kubaki Urusi.

    Juan Carlos Osorio

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio
  8. Neymar ni soka au sarakasi?, 83' Brazil 1-0 Mexico

    Ingawa hakuna takwimu kamili, Neymar ni mchezaji aliyesalia sakafuni kwa muda mrefu Kombe la Dunia 2018.

    Neymar sakafuni

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Neymar sakafuni
  9. Paulinho ampisha Fernandinho, 80' Brazil 1-0 Mexico

    Brazil wageuza mbinu na kujaribu kulinda uongozi wao mechini.

  10. Refa mwenye huruma, 80' Brazil 1-0 Mexico

    Refa wa Italia Gianluca Rocchi ametoa kadi saba za njano hatua ya makundi.

    Ametajwa kuwa mmoja wa marefa wenye huruma Kombe la Dunia.

    Gianluca Rocchi

    Chanzo cha picha, BBC Sport

    Maelezo ya picha, Gianluca Rocchi
  11. Mexico eneo hatari la Brazil, lakini bila mafaniko., 74' Brazil 1-0 Mexico

  12. Neymar sakafuni, lakini sio jereha hatari, 71' Brazil 1-0 Mexico

    Layun amemwumiza mshambulizi huyo wa Brazil.

    Anatarajiwa kurejea!

  13. Mexico waaachilia, lakini hadi kwa mabeki, 70' Brazil 1-0 Mexico

  14. Brazil barabarani.....hatari langoni, 68' Brazil 1-0 Mexico

    Pasi baada ya pasi, hatua baada ya nyingine, miondoko ya aina yake kutoka mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia.

  15. Neymar awapiku Messi na Ronaldo, 67' Brazil 1-0 Mexico

    Imemchukua Neymar shuti 38 pekee kufunga mabao 6 Kombe la Dunia wakati kufunga mabao kama hayo, ilimlazimu Lionel Messi kujaribu mara 67 na Ronaldo kuachilia mikwaju 74 Kombe la Dunia.

    Neymar

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Neymar
  16. Wiiiiiiiiiiiillllllllliiiiiaaaaaaannnnnnn....lakini Ochoa atoa!, 63' Brazil 1-0 Mexico

  17. Casemiro nje ya robo fainali, 62' Brazil 1-0 Mexico

    Kiungo wa Brazil Casemiro amelishwa kadi yake ya pili ya njano Urusi 2018.

  18. Nipo pia: Neymar kwa Mbappe, 60' Brazil 1-0 Mexico

    Ni mashindano kati ya Neymar na Mbappe ....

    Bao la Neymar

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Bao la Neymar
  19. Paulinhoooo aachilia shuti, lakini Ochoa amnyima, 59' Brazil 1-0 Mexico

  20. Heshima kwa Brazil.....ufungaji mabao, 57' Brazil 1-0 Mexico

    Brazil ndio timu yenye mabao mengi zaidi kwenye historia ya Kombe la Dunia.

    Bao la Neymar ni la 227 kufungwa na A Seleção!