Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Israel yasema uvamizi wa Gaza ulikuwa "maandalizi ya hatua inayofuata ya mapigano"
Jeshi la Israel lilifanya "uvamizi uliolenga" maeneo kadhaa kaskazini mwa Gaza usiku kucha kwa kutumia vifaru
Moja kwa moja
Yusuf Jumah
Habari za hivi punde, Hamas yasema takriban mateka 50 waliuawa tangu mashambulizi ya Israel yaanze
Msemaji kutoka tawi la kijeshi la Hamas anasema takriban mateka 50 wanaoshikiliwa na wapiganaji wake huko Gaza wameuawa kutokana na Israel kushambulia kwa mabomu Ukanda huo, kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Hamas tarehe 7 Oktoba.
Abu Ubeida hakutoa maelezo zaidi.BBC bila shaka haiwezi kuthibitisha idadi hii kwa njia huru
Jeshi la Israel limewatambua mateka 224 wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.
Soma zaidi kuhusu mateka ni nani hapa.
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Erdogan asema nchi za Magharibi hupuuza sheria wakati 'damu ya Waislamu inapomwagika'
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameshambulia jibu la serikali za Magharibi kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza - akisema nchi za Magharibi hazichukui hatua kwa sababu "damu iliyomwagika ni damu ya Waislamu".
"Ni nini kilitokea kwa Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu?"Aliuliza."Wao [Magharibi] hawataitazama ikiwa haitoshelezi kusudi lao. Kwa nini? Kwa sababu damu inayomwagika ni damu ya Waislamu."
Jana, Erdogan alighairi safari ya Israel na kusema kuwa anajutia kusalimiana kwa mkono na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York mwezi uliopita.
Hayo yakiarifiwa waziri wa mambo ya nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina - ambayo inasimamia Ukingo wa Magharibi unaokaliwa lakini sio Gaza - alielezea mashambulizi ya anga ya Israel kama "vita vya kulipiza kisasi".
Akizungumza nchini Uholanzi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague, Riyad al-Maliki alisema shambulio hilo la bomu lilikuwa baya zaidi kuliko mashambulizi ya awali ya Israel, na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano.
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Ziara ya Mfalme Kenya yazua mwito mpya wa kurudishwa kwa fuvu
Wazee wa jamii ya Nandi nchini Kenya wametoa madai mapya kwa Uingereza kurudisha fuvu la Koitalel arap Samoei, chifu pamoja na kiongozi wa kiroho na kijeshi aliyeuawa na Waingereza mwaka 1905.
Matakwa hayo mapya yanakuja siku chache kabla ya ziara ya Mfalme Charles III nchini Kenya tarehe 31 Oktoba.
Samoei, ambaye aliongoza upinzani mkali dhidi ya wakoloni, aliuawa na mwanajeshi wa Uingereza Kanali Richard Meinertzehagen, baada ya kuwalaghai Samoei na viongozi wengine wa Nandi kuhudhuria mkutano wa mapatano.
Kulingana na gazeti la Daily Nation la Kenya, wazee hao pia wanataka kurejeshewa vitu vyao vya kitamaduni vilivyoibiwa na kufidiwa kwa ukatili waliofanyiwa jamii wakati wa utawala wa kikoloni, ikiwa ni pamoja na mauaji, kuwekwa kizuizini na kuwahamisha watu wa jamii wa Nandi kwa nguvu.
Fuvu la Samoei linaaminika kuwa katika mkusanyiko wa makumbusho mahali fulani nchini Uingereza.
Wazee wa Nandi wameiomba mara kwa mara Uingereza kurejesha mabaki yake.
"Tunamsihi Mfalme Charles, tunahitaji kupata fuvu hilo ili lirudishwe Nandi kwa mazishi ya heshima," David Samoei aliambia kituo cha runinga cha KTN News mapema mwaka huu.
Ukeketaji: Mwanamke akutwa na hatia ya kupeleka mtoto Kenya ili kukeketwa
Mwanamke mmoja amepatikana na hatia ya kumpeleka mtoto wa Uingereza wa miaka mitatu barani Afrika kwa ukeketaji.
Amina Noor, 39, ndiye mtu wa kwanza kukutwa na hatia ya kusaidia mtu ambaye si Mwingereza kufanya ukeketaji na wa pili kufunguliwa mashtaka kwa ufanisi chini ya Sheria ya Ukeketaji ya 2003.
Noor, kutoka Harrow kaskazini-magharibi mwa London, alizaliwa Somalia lakini ana uraia wa Uingereza.
Mwaka wa 2006 alimpeleka mtoto katika nyumba ya kibinafsi nchini Kenya kwa ajili ya upasuaji huo.
Noor aliiambia mahakama ya Old Bailey kwamba ukeketaji unafanywa kwa sababu za kitamaduni na ulikuwa utaratibu ambao yeye mwenyewe alikuwa amepitia akiwa mtoto.
Ilikuwa ni mwaka wa 2015 tu ambapo msichana huyo - ambaye sasa ana umri wa miaka 21 na ambaye hawezi kutambuliwa - alimwambia mwalimu wa shule kwamba alifanyiwa ukeketaji na polisi walijulishwa.
Kufuatia uchunguzi katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Chuo Kikuu mnamo 2019 ilibainika kuwa sehemu ya uke wa msichana huyo ilikuwa imetolewa kabisa.
Akitoa ushahidi katika kesi yake Amina Noor alidai alikuwa amekumbana na shinikizo la kitamaduni ili utaratibu ufanyike.
Noor alisema kwamba yeye na mwanamke mwingine walimchukua mtoto huyo kwa gari la tuk-tuk na aliambiwa asubiri nje ya nyumba.
Nini kimetokea leo?
- Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imesema takriban watu 7,000 wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita hivyo ikiwa ni ongezeko la zaidi ya 500 tangu jana.
- Jeshi la Israel linasema kuwa uvamizi wa usiku mmoja huko Gaza haukusababisha vifo vya wanajeshi wa Israel.Hapo awali, tulisikia IDF ilipiga "vikundi vingi vya magaidi, miundombinu na vituo vya kurusha makombora ya vifaru" wakati wa uvamizi huo.
- Jeshi la Israel limewatambua mateka 224 wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza, ikiwa ni ongezeko la wawili tangu kufanyiwa marekebisho mara ya mwisho.
- Baadhi ya Wapalestina wamezungumza na vyombo vya habari vya kimataifa wakiomboleza vifo vya watoto wao akiwemo baba wa mtoto wa miezi miwili.
- Malori mengine12 yaliyokuwa yamebeba misaada yamevuka hadi Gaza asubuhi ya leo, na kufanya jumla ya malori yaliongia Gaza tangu Oktoba 21 hadi 74 - lakini hakuna mafuta yanayopitia.
- Hamas inasema ilirusha msururu mwingine wa roketi katikati mwa Israel kutoka Gaza - hakuna majeruhi walioripotiwa mara moja
Mahakama ya Juu ya Nigeria imetupilia mbali pingamizi za uchaguzi zilizotolewa na Atiku Abubakar na Peter Obi
Mahakama ya Juu nchini Nigeria imetupilia mbali pingamizi zote mbili za upinzani dhidi ya ushindi wa Rais Bola Tinubu.
Wagombea hao wawili wakuu wa upinzani walikuwa wanataka kutengua uchaguzi wa urais wa Februari, kwa madai kuwa ulikumbwa na kasoro.
Mahakama ya Malalamiko ya Uchaguzi iliidhinisha ushindi wa Bw Tinubu mwezi uliopita, lakini upinzani ulisisitiza kuwa mahakama ya juu zaidi ya Nigeria inapaswa kufuta uamuzi huo.
Matokeo ya uchaguzi wa rais hayajawahi kubatilishwa nchini Nigeria.
Majaji hao kwanza walitupilia mbali pingamizi lililotolewa na Atiku Abubakar, ambaye aliibuka wa pili katika uchaguzi huo, na kisha kulikataa la Peter Obi, ambaye aliibuka wa tatu.
Uchaguzi huo ulikuwa wenye ushindani mkali zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka wa 1999, na wagombea watatu wenye nguvu kwa mara ya kwanza.Bw Tinubu alishinda kwa 37% ya kura zilizopigwa, dhidi ya 29% za Bw Abubakar na 25% za Bw Obi.
Wael Al-Dahdouh: Familia ya mwandishi wa Al Jazeera yauawa katika shambulio la Gaza
Familia ya mwandishi wa habari wa Al Jazeera imeuawa katika shambulio la anga la Israel huko Gaza, mtandao huo umethibitisha.
Mke wa Wael Al-Dahdouh, mwanae wa kiume na bintiye wote waliuawa katika kambi ya wakimbizi katikati mwa Gaza siku ya Jumatano, Al Jazeera ilisema katika taarifa.
Baadaye iliripoti kuwa mjukuu wake pia alikufa.
Al Jazeera ililaani mauaji hayo na "shambulio la kiholela" lililofanywa na Israel huko Gaza.
Kulingana na shirika hilo la habari, familia ya Bw Al-Dahdouh ilikuwa ikiishi katika nyumba katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Gaza baada ya kufurushwa kutoka kaskazini mwa Gaza kufuatia onyo la Israel kwa wakazi kuhamia kusini kutokana na hatua za kijeshi zinazoendelea.
Wanafamilia wengine walisemekana kuzikwa chini ya vifusi.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilithibitisha kuwa lilifanya shambulizi lililolenga Hamas katika eneo ambalo watu wa familia ya Bw Al-Dahdouh waliuawa, kulingana na CNN.
Alipoulizwa na BBC kuhusu kupoteza maisha ya raia katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, yakiwemo ya wanahabari na familia zao, msemaji wa IDF Lt Kanali Peter Lerner alisema "kupoteza maisha yoyote ni janga".
Picha zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha Bw Al-Dahdouh akilia hospitalini, akiwa ameshikilia kile kilionekana kuwa mwili wa bintiye mwenye umri wa miaka saba na kupiga magoti juu ya mwili wa mwanawe.
"Hakuna mahali salama katika Gaza hata kidogo," alisema katika tafsiri ya Kiingereza ya mahojiano na Al Jazeera.
Bw Al-Dahdouh ni mkuu wa ofisi ya Al Jazeera Arabic huko Gaza na amefanya kazi katika shirika hilo la habari kwa miaka kadhaa.
Al Jazeera ilisema "ina wasiwasi mkubwa juu ya usalama wa wenzetu huko Gaza na kushikilia mamlaka ya Israeli kuwajibika kwa usalama wao".
"Tunaitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kukomesha mashambulizi haya dhidi ya raia, na hivyo kulinda maisha ya watu wasio na hatia."
Takriban waandishi wa habari 24 wameuawa hadi sasa katika mzozo wa hivi punde kati ya Israel na Gaza, kulingana na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari.
Gaza imekuwa chini ya mashambulizi ya kijeshi ya mara kwa mara na Israel kufuatia mashambulizi ya kikatili ya kushtukiza ya wapiganaji wa Hamas tarehe 7 Oktoba, na kuua zaidi ya watu 1,400.Zaidi ya watu 200 bado wanashikiliwa mateka.
Wakati huo huo, wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza inasema karibu watu 6,500 wameuawa huko.Israel imekata usambazaji wa mafuta, umeme na maji mengi katika eneo hilo.Kiasi kidogo cha msaada sasa kinaingia kupitia Misri.
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Uchina: Polisi waokoa paka 1,000, katika msako dhidi ya biashara haramu ya kuuza nyama ya paka
Polisi nchini China wameokoa zaidi ya paka 1,000 dhidi ya kuchinjwa na kuuzwa kama nyama ya nguruwe au kondoo, ripoti za vyombo vya habari vya serikali zinasema .
Wakipokea kidokezo kutoka kwa wanaharakati wa haki za wanyama, polisi walilikamata lori lililokuwa limebeba paka hao katika mji wa mashariki wa Zhangjiagang.
Paka hao walihamishwa hadi kwenye makazi, kulingana na ripoti katika gazeti la The Paper.
Uokoaji ulifichua biashara haramu ya nyama ya paka na kuibua wasiwasi mpya kuhusu usalama wa chakula, ripoti hiyo ilisema.
Nyama ya paka inaweza kuuzwa kwa yuan 4.5 ($0.61; £0.51) kwa kila gramu 600 ,wanaharakati walisema.Paka mmoja anaweza kutoa gramu 3000 hadi 3600.
Haikuwa wazi ikiwa paka hao waliookolewa walikuwa wamepotea au kipenzi.Walikuwa wakisafiria kuelekea kusini mwa nchi ambako walipaswa kuliwa kama mishikaki ya nyama ya nguruwe na kondoo na soseji.
Kwa mujibu wa gazeti la The Paper, wanaharakati mjini Zhangjiagang walikuwa wameona idadi kubwa ya paka wakiwa wamezuiliwa kwenye masanduku ya mbao yaliyotundikwa kwenye rundo na kuifuatilia kwa siku sita.
Paka hao walipopakiwa kwenye lori tarehe 12 Oktoba, walisimamisha gari na kuwaita polisi.
Mzozo wa Israel-Palestina:Haya ndio unayohitaji kujua
Vifaru vya Israel vyavamia Gaza
- Jeshi la Israel lilifanya "uvamizi uliolenga" maeneo kadhaa kaskazini mwa Gaza usiku kucha, kwa kutumia vifaru na tingatinga kuingia ukanda huo.
- Si mara ya kwanza kwa Israel kuthibitisha uvamizi wa mpakani tangu Hamas iliposhambulia tarehe 7 Oktoba
- Lakini lugha ya IDF kuhusu shambulio hilo ina nguvu zaidi kuliko uvamizi uliopita, ikisema ilikuwa "sehemu ya maandalizi ya hatua zinazofuata za mapigano"
- IDF pia inasema ilishambulia malengo 250 ya Hamas kwa usiku mmoja, ikiharibu miundombinu, sehemu za kurusha makombora na "makundi mengi ya kigaidi"
Uhaba wa mafuta Gaza
- Umoja wa Mataifa unaendelea kutoa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa uhaba wa mafuta huko Gaza
- Shirika la Umoja wa Mataifa linalowawakilisha Wapalestina huko Gaza linasema kuwa limepata baadhi ya mafuta, ambayo yatapewa kipaumbele kwa kuchuja na kusafisha maji.
- Lakini inasema juhudi zingine za kibinadamu, kama kuoka mkate, zimesitishwa
- Hapo awali ilionya operesheni yake inaweza kumalizika ifikapo Jumatano usiku, kwani hakuna mafuta yaliyoruhusiwa kuingia Gaza tangu tarehe 7 Oktoba
- Israel inapinga ukubwa wa mgogoro wa mafuta - na inashutumu Hamas kwa kuhifadhi akiba ya bidhaa hiyo muhimu
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Hatutavamia nchi yoyote - Waziri Mkuu wa Ethiopia
Waziri Mkuu Abiy Ahmed anasema Ethiopia haitavamia taifa lolote jirani baada ya maoni yake ya hivi majuzi juu ya hitaji la nchi yake kumiliki eneo la bahari lililozua hali ya wasiwasi katika eneo hilo.
Akihutubia taifa katika viwanja vya mji mkuu, Addis Ababa, kuadhimisha Siku ya Jeshi Alhamisi, Bw Abiy alisema Ethiopia "haitawahi kuvamia" nchi yoyote.
"Jeshi letu halijawahi kuanzisha mashambulizi na sasa hatutashambulia mtu yeyote," alisema.
"Hofu imetolewa kwamba kunaweza kuwa na uvamizi wakati Ethiopia hivi karibuni ilisisitiza haja ya kujadili baadhi ya masuala ... hakuna chochote ambacho Ethiopia inakusudia kufikia kupitia uvamizi. Ningependa kuwahakikishia kwa nguvu kwamba hatutavuta kichocheo. ndugu zetu kupata mahitaji yetu kwa nguvu," Waziri Mkuu aliongeza.
Inakuja siku chache baada ya Bw Abiy kuwaambia wabunge kwamba kupata eneo la bahari ni "suala la kuwepo" kwa nchi yake.
Ethiopia ilikosa bandari kufuatia kujitenga kwa Eritrea mwaka 1993, na tangu wakati huo imekuwa ikitegemea Djibouti kwa zaidi ya 85% ya uagizaji na mauzo ya nje.
Ethiopia na Eritrea walipigana vita vya mpaka kwa miaka miwili kati ya 1998 na 2000.
Mvutano ulipunguzwa kati ya nchi hizo mbili mnamo 2018 wakati Bw Abiy na Rais Isaias Afwerki wa Eritrea walipotia saini makubaliano ya amani.
Bahari ya Uchina Kusini: Biden asema Marekani itailinda Ufilipino ikiwa China itaishambulia
Rais wa Marekani Joe Biden ameionya China kwamba Marekani itailinda Ufilipino endapo kutakuwa na shambulio lolote katika eneo linalozozaniwa la Bahari ya China Kusini.
Maoni hayo yanakuja siku chache baada ya kugongana mara mbili kati ya meli za Ufilipino na Uchina kwenye maji yanayogombaniwa.
Bwana Biden alisisitiza ahadi yake ya ulinzi ya "ironclad" kwa Ufilipino.
Manila imepinga madai ya Wachina kuhusu umiliki wa sehemu ya bahari hiyo kukata vizuizi vinavyoelea na kukaribisha vyombo vya habari kurekodi kile inachokiita hatua hatari za Beijing baharini.
Kauli ya Bw Biden kuhusu Bahari ya Kusini ya China siku ya Jumatano ndiyo yenye nguvu zaidi tangu mvutano kati ya Beijing na Manila ulipozidi katika miezi ya hivi karibuni.
"Nataka kuwa wazi - nataka kuwa wazi sana: Ahadi ya ulinzi ya Marekani kwa Ufilipino ni dhabiti. Makubaliano ya ulinzi ya Marekani na Ufilipino ni ya dhabiti," alisema.
Ahadi Iliyotiwa saini mwaka wa 1951, Mkataba wa Ulinzi wa Mutual unazifunga Marekani na Ufilipino, koloni lake la zamani, katika kulindana katika tukio la shambulio la silaha.
"Shambulio lolote dhidi ya ndege za Ufilipino, meli, au vikosi vyenye silaha vitalazimisha kutumika kwa Mkataba wetu wa Ulinzi wa Pamoja na Ufilipino," aliongeza katika hotuba yake kwenye Ikulu ya Marekani Jumatano, alipokuwa akimkaribisha Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese.
Unaweza pia kusoma
Kwa nini Israel inataka uvamizi wa ardhini uonekane uko karibu?
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Tom Bateman
- Nafasi, BBC News
Hili ndilo jambo ambalo ungetarajia kabla ya uvamizi wa ardhini - askari wakichunguza kutafuta na kuharibu ulinzi ardhini.
Picha zinaonyesha vifaru na tingatinga za kivita zikiingia. Kauli ya Israel inahusu mapigano ya ardhini, ingawa picha hazionyeshi hili.
Inasema wanajeshi walitoka "mwisho wa shughuli".
Lakini ni vigumu kusema hii inatupa dalili nyingi zaidi kuhusu muda wa operesheni ya ardhini.
Lugha inayotumiwa na jeshi la Israel ina nguvu zaidi kuliko mashambulizi ya awali ikisema hii ni "sehemu ya maandalizi ya hatua zinazofuata za mapigano".
Lakini vita vya maneno ni muhimu pia. Israel inataka kuonyesha kwamba uvamizi unakaribia kwa sababu tatu:
- Kumaliza ari ya kuteleza mashambulio ya ardhini upande wa Palestina
- Kwa ndani ya Israeli inataka kuonyesha kwamba majibu yanakuja, na
- Kuweka shinikizo kwa Hamas - hasa juu ya mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Mbunge wa Kenya alaumiwa kwa kuvaa skafu ya Palestina
Mbunge wa Kenya aliamriwa kuvua skafu ya kitamaduni ya Wapalestina aliyokuwa amevaa wakati wa vikao vya bunge siku ya Jumatano.
Farah Maalim alisema alikuwa amevaa skafu hiyo kwa mshikamano na Wapalestina mjini Gaza, huku kukiwa na mapigano kati ya Israel na Hamas.
Alisema Palestina "inahitaji kuungwa mkono na kila mtu nchini Kenya".
Lakini spika wa Bunge la taifa aliamuamuru mbunge huyo kuvua skafu akisema vazi hilo linakiuka kanuni za bunge.
Wabunge wenzake pia walimlaumu mbunge huyo kwa "kutoheshimu" kanuni za Bunge.
Haya yanajiri siku chache baada ya polisi nchini Kenya kuwazuilia watu watatu kwa muda mfupi kwa kushiriki katika mkutano watu wanaoiunga mkono Palestina katika mji mkuu, Nairobi.
Rais William Ruto ameeleza kuunga mkono kikamilifu wa serikali yake kwa Israel katika mzozo unaoendelea.
Mahakama ya juu nchini Nigeria kutoa uamuzi kuhusu pingamizi la kura ya urais
Mahakama ya Juu zaidi ya Nigeria inatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu iwapo itaunga mkono au kutounga mkono ushindi wa rais Bola Tinubu ambao ulikuwa na utata katika uchaguzi.
Wapinzani wake wawili wakuu, Atiku Abubakar wa Peoples Democratic Party na Peter Obi wa Labour Party, wanatafuta kubatilisha uchaguzi wa urais wa Februari, kwa madai kuwa ulikumbwa na kasoro.
Mahakama ya Juu ilikuwa na siku 60 kutoa uamuzi wake. Lakini imeamua kuharakisha uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za wapinzani Jumatatu.
Bw Abubakar alitoa ushahidi mpya, akisema cheti ambacho Rais Tinubu aliwasilisha kwa halmashauri ya kusimamia uchaguzi kinatofautiana na kile kinachodaiwa kutolewa na Chuo Kikuu cha Jimbo la Chicago.
Mpinzani mwingine, Bw Obi, alisema kuwa Bw Tinubu hakuwa na sifa za kuwania urais wa Nigeria wakati huo.
Wanasisitiza kuwa mahakama ya juu zaidi nchini inafaa kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Malalamiko ya Uchaguzi, ambayo iliidhinisha ushindi wa Bw Tinubu mwezi uliopita.
Iwapo itaunga mkono uamuzi wa mahakama ya chini, hiyo itakuwa ni kufuata mtindo ulioonekana katika chaguzi zilizopita katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika, ambapo matokeo ya uchaguzi wa urais hayajawahi kubatilishwa.
Marekani: Mamia ya polisi wanamsaka mshukiwa anayehofiwa kuwaua kwa risasi watu 16 Maine
Mamia ya maafisa wa polisi wanaendelea na msako wa kumtafuta mtu aliyejihami kwa bunduki baada ya ufyatulianaji risasi mkubwa katika mji wa Lewiston katika jimbo la Maine nchini Marekani, huku takriban watu 16 wakihofiwa kuuawa.
Mshukiwa wa shambulio hilo ametajwa kwa jina la Robert Card, na ni mwalimu wa bunduki ambaye alifunzwa na jeshi la Marekani katika mji wa Saco, Maine, kulingana na taarifa ya polisi ya serikali iliyoonekana na Associated Press.
Taarifa hiyo ilisema kuwa alikuwa amekaa katika kituo cha afya ya akili katika majira ya joto ya 2023 na alitishia kupiga risasi kwenye kituo hicho.
Ofisi ya Sherifu wa Kaunti ya Androscoggin ilitoa picha mbili za mshukiwa, ikisema kuwa yuko majumbani na kuomba usaidizi wa umma kumtambua.
Walionyesha mtu mwenye ndevu aliyevalia sweta ya kahawia akiwa amebeba bunduki akiingia kwenye jengo.
Polisi pia walishirikisha umma picha ya gari jeupe, wakisema bampa yake ya mbele inaaminika kuwa imepakwa rangi nyeusi, na kumtaka yeyote anayeitambua awasiliane na polisi.
Ikulu ya White House inasema Rais Biden amefahamishwa kuhusu hali ya Lewiston na ataendelea kupokea taarifa.
Picha za setilaiti zinazoionyesha Gaza mwanzoni mwa vita na sasa
Picha za satelaiti zinazotufikia sasa, zinaonyeshaa maeneo ya Gaza mwanzoni mwa vita, na sasa.
Picha ya juu hapa chini inaonyesha Beit Hanoun kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mnamo tarehe 10 Oktoba, 2023, na ya chini inaonyesha eneo hilo hilo siku 11 baadaye.
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Habari za hivi punde, Jeshi la Israel latekeleza mashambulizi ‘yanayolenga’ kaskazini mwa Gaza
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limefanya "uvamizi uliolengwa" usiku kucha kaskazini mwa Gaza kwa kutumia vifaru.
Lilisema uvamizi huo ulifanyika kama sehemu ya "maandalizi ya hatua zinazofuata za mapigano" na "ulipiga vikundi vingi vya magaidi, miundombinu na vituo vya kurushia makombora ya vifaru", katika chapisho la Alhamisi, likishirikisha umma video ya operesheni hiyo.
"Wanajeshi hao wametoka katika eneo hilo na kurejea katika eneo la Israel," iliongeza taarifa hiyo.
Hapo awali, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema katika hotuba ya televisheni kwamba vikosi vya IDF bado vinajiandaa kwa uvamizi wa ardhini, lakini hakutoa dalili zozote za wakati litakapoanza.
Israel iliwaambia wakaazi milioni 1.1 wa Jiji la Gaza na maeneo mengine ya kaskazini kuondoka kwa usalama wao wenyewe wiki iliyopita.
Lakini Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aliiambia BBC kuwa baadhi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Gaza wanaanza kurejea huku hali ikizidi kuwa mbaya kusini mwa nchi hiyo.
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Jeshi la Israeli linapinga madai ya Umoja wa Mataifa kuwa mafuta yanakaribia kuisha Gaza
Jeshi la Israel (IDF) limepinga madai ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kwamba mafuta yataisha hivi karibuni katika ukanda wa Gaza.
“Ninavyojua, bado kuna umeme katika Ukanda wa Gaza. Na ripoti hii inatia shaka kidogo,” msemaji wa IDF, Lt Kanali Jonathan Conricus alisema katika mkutano wa moja kwa moja, akirejelea ripoti ya UNRWA kutoka tarehe 16 Oktoba.
"Tulijibu madai ya UNRWA kuwaelekeza mahali ambapo Hamas - ambayo inasimamia Ukanda wa Gaza - chanzo cha mafuta, na bidhaa nyinginezo. Yote ni ndani ya Ukanda wa Gaza.
"Kuna mafuta ya kutosha kwa siku nyingi kwa hospitali na pampu za maji kufanya kazi. Vipaumbele tu ni tofauti. Hamas wanapendelea kuwa na mafuta yote kwa ajili ya uwezo wake wa kupigana vita, na kuwaacha raia bila,” aliongeza.
Hospitali mjini Gaza zinakabiliwa na kesi za dharura huku kukiwa na hofu kwamba usambazaji wa mafuta unaweza kuisha katika saa zijazo, kulingana na UN.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani, Dkt Richard Peeperkorn,awali aliiambia BBC kwamba hospitali zinazosaidiwa na Umoja wa Mataifa zinaendeshwa kwa jenereta "katika viwango vya chini tu kwa ajili ya shughuli za kuokoa maisha".
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
Macron aionya Israel kuhusu "uvamizi mkubwa" wa ardhini Gaza.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa tahadhari juu ya uvamizi "mkubwa" wa ardhini wakati akizungumza mjini Cairo mapema leo.
Rais huyo wa Ufaransa alisema kuwa uvamizi mkubwa wa ardhini katika Ukanda wa Gaza utakuwa "kosa."
Ameongeza kuwa jambo hilo litawadhuru raia bna halitaihakikishia Israel usalama wa muda mrefu. Lakini wakati huo huo, alisisitiza kwamba "Ufaransa inatambua haki ya Israeli ya kujilinda."
Aliongeza: "Kuhusiana na uingiliaji wa ardhini, ikiwa unalenga kabisa vikundi vya kigaidi, hili ni chaguo kwa Israeli, lakini ikiwa ni operesheni kubwa ambayo itahatarisha raia, basi katika hali hii nadhani litakuwa kosa kwa Israeli.”
Unaweza pia kusoma:
- Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
- Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
- Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
- Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas