Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Israel yasema uvamizi wa Gaza ulikuwa "maandalizi ya hatua inayofuata ya mapigano"

Jeshi la Israel lilifanya "uvamizi uliolenga" maeneo kadhaa kaskazini mwa Gaza usiku kucha kwa kutumia vifaru

Moja kwa moja

Yusuf Jumah

  1. Mzozo wa Israel na Hamas: Biden anasema 'hana imani' na idadi ya waliouawa Gaza

    Rais wa Marekani Joe Biden alisema "hana imani na idadi ambayo Wapalestina wanaitumia" alipoulizwa kama Israel inafanya vya kutosha "kupunguza majeruhi ya raia" katika mkutano na waandishi wa habari hapo awali.

    "Sina dhana kwamba Wapalestina wanasema ukweli kuhusu idadi ya watu waliouawa. Nina hakika watu wasio na hatia wameuawa, na ni garama ya kuanzisha vita," Biden aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

    "Waisraeli wanapaswa kuwa waangalifu sana ili kuhakikisha kuwa wanazingatia kuwalenga watu ambao wanaeneza vita hivi. Na ni kinyume na maslahi yao wakati hilo halifanyiki. Lakini sina imani na idadi ambayo Wapalestina wanaitumia,” aliongeza.

    Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas mjini Gaza inasema kuwa zaidi ya watu 6,500 sasa wameuawa tangu Oktoba 7, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 2,700.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  2. Urusi inasema imefanya mazoezi ya shambulio 'kubwa' la nyuklia

    Urusi imefanya mazoezi ya uwezo wake wa kufanya shambulio "kubwa" la nyuklia, Kremlin inasema.

    Mazoezi ya kijeshi yalihusisha kutoa "jibu kwa shambulio la nyuklia la adui", Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu alisema.

    Televisheni ya serikali ilimuonyesha Shoigu akimsimulia Rais Vladimir Putin kuhusu maozezi hayo.

    Haya yanajiriwakati bunge la Urusi likiwa tayari limeunga mkono kuondolewa kwa uidhinishaji wa Moscow wa mkataba wa kimataifa ambao unapiga marufuku majaribio yote ya kimwili ya vichwa vya nyuklia.

    Urusi na Marekani hufanya mazoezi ya utayari wa nyuklia ya mara kwa mara.

    Mazoezi hayo mwaka huu yalihusisha "kutoa shambulio kubwa la nyuklia na vikosi vya kimkakati vya kushambulia kukabiliana na shambulizi la nyuklia la adui", Bw Shoigu aliripoti kwa Rais Putin.

    Taarifa ya Kremlin ilisema kuwa "urushaji wa makombora ya balestiki na ya kusafiri" ulifanyika.

    Mapema mwezi huu, Bw Putin alisema Urusi imefanya ‘’jaribio la mwisho la mwisho la mafanikio’’ la kombora la nyuklia.

    Majaribio ya hivi punde yanaonekana kama maonyesho ya nguvu ambayo yanaambatana na Moscow kufutilia mbali makubaliano ya kimataifa ya kupiga marufuku majaribio ya nyuklia.

    Unaweza pia kusoma:

    • Vita vya Ukraine: Putin asema Urusi kupeleka vichwa vya nyuklia Belarus ni onyo kwa Magharibi
    • Je Urusi inaweza kutekeleza tishio lake la kutumia silaha za nyuklia huko Ukraine?
  3. Viongozi wa Hamas, Islamic Jihad na Hezbollah wakutana Lebanon

      • Author, Jeremy Bowen
      • Nafasi, Mhariri wa kimataifa akiripoti kutoka Israel

    Katika muda wa saa 24 zilizopita, picha imeonekana ya viongozi wa Hamas na Kundi la Islamic Jihad nchini Lebanon, wakikutana na Hassan Nasrallah, kiongozi wa wanamgambo wa Kiislamu wa Shia na harakati ya kisiasa ya Hezbollah.

    Ni chombo chenye nguvu zaidi nchini Lebanon, chenye nguvu zaidi kuliko taifa la Lebanon, na tawi lake la kijeshi linaungwa mkono, linafunzwa na kuwekewa silaha na Iran.

    Wairani wanaona Hezbollah kama sehemu muhimu ya mkakati wao wa ulinzi wa katika eneo. Pengine ina makombora 150,000 ya aina tofauti na maelfu ya wapianaji waliofunzwa, walio na uzoefu mkubwa wa vita kutokana na mapigano katika vita nchini Syria kwa niaba ya utawala wa Assad huko.

    Moja ya hofu na hatari kubwa ya haya yote ni kwamba kunaweza kutokea vita vingine kati ya Israel na Hezbollah huko Lebanon, ambacho ni kikosi chenye nguvu sana.

    Nadhani makundi hayo yanazungumza wakati wote, kusema kweli , lakini wamechagua kufanya mkutano huu hadharani - kwa namana moja kuweka shinikizo kwa Israeli na kwa sehemu kwa sababu wao pia wanakabiliana na shinikizo.

    Wanakabiliwa na ukosoaji ambao wamekuwa wakizungumza juu ya kuipiga Israeli, na sasa kwa kuwa fursa imewadia, wengine wanasema, "Kwa nini usifanye?" Nimesikia hata baadhi ya Wapalestina wakisema, "Hezbollah wametuangusha."

    Hata hivyo, hakujawa na dalili nyingi kwamba Iran inataka haya yatokee.

    Kuizuia Iran na washirika wake wa Lebanon ni sababu kuu iliyofanya Marekani ipeleke kundi moja la wanajeshi katika bahari ya Mediterania huku lingine likiwa njiani kuelekea Ghuba.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mohammed Deif: Mfahamu kiongozi wa Hamas anayewanyima usingizi Israel
    • Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Je, ni nini kilichotokea 1967 wakati israel ilipokabiliana kijeshi na mataifa matatu ya kiarabu katika vita vya siku sita?
    • Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Tunachojua kufikia sasa kuhusu raia wa Israel waliotekwa na Hamas
  4. Netanyahu anasema Israel inajiandaa kwa uvamizi wa ardhini Gaza lakini hakusema ni lini

    Ni saaa kumi na mbili unusu kwa saa za Afrika Mashariki na ikiwa unajiunga nasi, katika vita vya Israel-Gaza hiki ndicho kimekuwa kikitokea:

    • Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amekariri kuwa Israel inajiandaa kwa uvamizi wa ardhini huko Gaza, lakini hakutoa dalili zozote kuhusu muda huo.
    • Azimio la kushughulikia hali ya Israel na Gaza limeshindwa tena katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa - wakati huu likikabiliwa na kura za turufu kutoka Urusi na China.
    • Zaidi ya hayo, Israel imeendelea kumtaka Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ajiuzulu kutokana na matamshi aliyotoa kuhusu vita vya Gaza kutotokea "katika ombwe"
    • Umoja wa Mataifa pia umeonya kwamba mafuta katika ukanda wa Gaza yataisha mara moja, na kulazimisha kufungwa kwa hospitali na makazi.
    • Shirika la Afya Duniani limewataka Hamas kuwaachilia mateka wote kwa misingi ya matibabu.

    Unaweza pia kusoma:

  5. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 26.10.2023