Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Shirika la Umoja wa Mataifa laonya operesheni ya Gaza inaweza kumalizika kesho bila mafuta zaidi

Touma anasema shirika hilo lina makao 150, mengi yakiwa ni shule.

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. RSF yalishtumu jeshi la Sudan kwa kushambulia ubalozi wa Ufaransa

    Kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Forces (RSF) kimeshutumu jeshi la Sudan kwa "kushambulia kwa mabomu ubalozi wa Ufaransa" katika mji mkuu wa nci hiyo.

    Katika chapisho kwenye mtanda wa X, zamani ikijulikana kama Twitter, RSF ilidai shambulio hilo lilisababisha "uharibifu mkubwa kwenye kituo hicho".

    "Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinashutumu vikali shambulio la anga la kiholela dhidi ya ubalozi wa Ufaransa," ilisema.

    "Kitendo hiki cha kinyama ni ukiukaji wa mikataba, kanuni na sheria za kimataifa. Tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kulaani ukatili huu."

    Jeshi la Sudan na Ufaransa hazijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

    Vita vya miezi sita kati ya RSF na jeshi la Sudan vimesababisha vifo vya watu 9,000 na wengine karibu milioni sita kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

    Mnamo Aprili, raia wa Ufaransa alijeruhiwa katika shambulio dhidi ya msafara ambao pande zinazopigana zililaumiana.

    Hapo jana RSF ilidai kuwaua zaidi ya wanajeshi 500 katika shambulio dhidi ya msafara wa kijeshi katika kiji ya Omdurman na Khartoum, ikiwa ni pamoja na "wapiganaji wa akiba waliojumuishwa jeshini hivi karibuni".

    Maelezo zaidi:

  3. Korea Kaskazini kufunga ubalozi wake nchini Uganda

    Korea Kaskazini inatarajiwa itafunga ubalozi wake nchini Uganda, na hivyo kumaliza nusu karne ya uwepo wa kidiplomasia katika mojawapo ya washirika wake wa muda mrefu zaidi barani Afrika.

    Hatua hiyo ilitangazwa Jumatatu, baada ya mkutano kati ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni na balozi wa Korea Kaskazini Jong Tong Hak.

    Taarifa kutoka ofisi ya rais wa Uganda iliyoangaziwa na shirika la habari la AFP ilisema: "Balozi Jong alimweleza rais kwamba Korea Kaskazini imechukua hatua ya kimkakati ya kupunguza idadi ya balozi barani Afrika, Uganda ikijumuisha, ili kuongeza ufanisi wa huduma za nje za nchi. taasisi." "Urafiki wetu mzuri utaendelea na utaimarishwa na kuendelezwa zaidi," Bw Jong alinukuliwa akisema.

    Korea Kaskazini ilianzisha uhusiano wake na Uganda muda mfupi baada ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1962.

    Pyongyang ilimuunga mkono Idi Amin aliponyakua mamlaka mwaka 1971, akivipatia vikosi vyake mafunzo na silaha.

    Korea Kaskazini ilifungua ubalozi huo mjini Kampala mwaka mmoja baadaye.

    Rais Museveni amefanya ziara kadhaa nchini Korea Kaskazini, ambapo alikutana na kiongozi wa zamani Kim Jong Il, babake kiongozi wa sasa Kim Jong Un.

  4. Nigeria yazindua chanjo ya umma dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi

    Nigeria imeanza kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya virusi vya human papillomavirus (HPV) katika jitihada za kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya saratani ya shingo ya kizazi.

    HPV, virusi vya kawaida huenezwa kwa njia ya kujamiiana , inaweza katika matukio machache kusababisha saratani ya shingo ya kizazi.

    Mnamo 2021, utafiti mkubwa uligundua chanjo ya HPV ilikuwa na uwezo wa kupunguza visa vya saratani ya shingo ya kizazi kwa karibu 90%.

    Waziri wa Afya wa Nigeria Muhammad Pate aliiambia BBC kuwa kipindi hicho ni muhimu kwani"takribani wanawake 12,000 kila mwaka wana kiwango cha juu cha saratani ya mlango wa kizazi [nchini Nigeria]".

    "Takriban 90% yao hupoteza maisha kwa sababu hiyo," aliongeza.

    Kampeni hiyo ya kitaifa ilianza Jumanne na wizara ya afya inalenga kuwachanja wasichana milioni 16.6 wenye umri wa kati ya miaka tisa na 14 kufikia mwisho wa 2025.

    Imeunganishwa katika ratiba ya kitaifa ya chanjo ya Nigeria.Ufikiaji ni pamoja na ushirikiano na shule na viongozi kutoka nyanja za kidini na za kiraia.

  5. Li Shangfu: Waziri wa ulinzi wa China afutwa kazi

    China imemfuta kazi rasmi waziri wake wa ulinzi Li Shangfu, miezi miwili baada ya kutoweka katika maisha ya umma.

    Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu kuondolewa kwake, wala hakuna mtu atakayechukua nafasi yake kutangazwa.

    Kufukuzwa kwake kunafuatia kufutwa kazi hivi karibuni kwa maafisa kadhaa wakuu wa kijeshi, akiwemo Qin Gang-ambaye aliondolewa kama waziri wa mambo ya nje mwezi Julai.

    Bw Qin na Bw Li pia waliondolewa kwenye nyadhifa zao katika Baraza la Serikali, wizara ya nchi hiyo, siku ya Jumanne.

    Wabunge wakuu wa China, Kamati ya Kudumu ya Bunge la Wananchi, waliidhinisha kuondolewa kwa wanaume hao wawili, shirika la utangazaji la serikali CCTV liliripoti.

    Kufukuzwa kwake kunaiacha China bila waziri wa ulinzi huku ikijiandaa kuwakaribisha maafisa wa ulinzi wa kigeni mjini Beijing wiki hii.

    Reuters iliripoti mwezi uliopita kwamba alikuwa chini ya uchunguzi kwa washukiwa wa rushwa kuhusiana na ununuzi wa vifaa na maendeleo.

    Mara ya mwisho alionekana hadharani tarehe 29 Agosti, katika kongamano la usalama la Beijing na mataifa ya Afrika.Alikuwa tu kwenye wadhifa huo tangu Machi.

    Mhandisi wa anga ambaye alianza kazi yake katika kituo cha kurushia satelaiti na roketi, Jenerali Li amekuwa na mteremko mzuri kupitia safu ya wanajeshi na wasomi wa kisiasa wa China.

  6. Wagaza waliohamishwa: 'Tunahitaji usitishaji mapigano sasa'

    Faysal Shawaa yuko Gaza lakini amelazimika kuondoka nyumbani kwake, pamoja na mkewe na mwanawe.Aliambia BBC Radio 4 hali aliyonayo ni ngumu sana.

    "Tunakosa kila kitu; chakula, dawa na bila shaka hakuna umeme. Tuna bahati tuna nishati ya jua ambayo inakuja saa mbili au tatu kwa siku."

    Shawaa alisema zaidi ya kwamba "ni huzuni" na kwamba wanasubiri habari njema "ili kukomesha mashambulizi ya mabomu ya jeshi la Israel kila mahali."

    Aliongeza: "Huko Gaza wanaua watu kila dakika. Wanaharibu miundombinu, majengo, kila kitu kinaharibiwa.

    "Hatuna chochote kilichosalia huko Gaza."

    Shawaa alieleza kuwa kila usiku wanasikia mirindimo ya anga karibu "kila mahali" na kwamba "tunahitaji usitishaji vita sasa. Tunahitaji suluhu kwa hali hiyo.

    "Kila mwaka tunakuwa na aina fulani ya uvamizi wa Israel huko Gaza, wanaharibu Gaza na kisha tunaijenga upya Gaza. Inatosha."

    Mamlaka ya afya ya Gaza inasema hospitali katika Ukanda huo 'zimeanguka kabisa'

    Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza imetoa taarifa kwenye Telegram ikisema kuwa hospitali katika Ukanda wa Gaza "zimeanguka kabisa".

    “Tunathibitisha kuwa hospitali 12 na vituo vya afya 32 havina huduma, na tunahofia kuwa zaidi zitakosa huduma katika saa zijazo kutokana na kulenga na kukosa mafuta,” ilisema taarifa hiyo.

    Pia ilionya kuwa "milango ya hospitali kubaki wazi haimaanishi kuwa inatoa huduma kwa mafuriko ya watu waliojeruhiwa".

    Taarifa hiyo iliongeza ombi kwa jumuiya ya kimataifa kusambaza mafuta kwa hospitali, kutuma "wajumbe maalum wa matibabu kuwaokoa waliojeruhiwa katika uvamizi wa Israel" na kutoa wito kwa "wenzake wote waliostaafu na watu wa kujitolea kutoka kwa wataalamu wote kujiunga na hospitali mara moja."

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  7. Umoja wa Mataifa wasema operesheni yake Gaza itakamilika kesho 'kama hatutapata mafuta'

    Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya juu ya uwezekano wa kukomesha shughuli yake ya kutoa misaada katika Ukanda wa Gaza.

    Juliette Touma ameambia kipindi cha BBC Radio 4 cha World At One kwamba "tusipopata mafuta kwa haraka, tutalazimika kusimamisha shughuli zetu katika Ukanda wa Gaza kuanzia kesho (Jumatano) usiku".

    Pia anasema shirika la Umoja wa Mataifa likisimamisha shughuli zake, watu wa Gaza "watafadhaika zaidi na kupoteza matumaini."

    Msemaji wa jeshi la Israel Jonathan Conricus amesema kuwa Hamas inahifadhi mafuta.

    Touma pia alisema kuwa wafanyakazi sita zaidi wa UNRWA wameuawa, na kufanya jumla ya wafanyakazi wa shirika hilo ambao wamefariki Gaza kufikia 35.

    "Tunaomboleza kupoteza wenzetu," alisema.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  8. Wakazi wa Lebanon wakimbia makazi yao huku mashambulizi ya mpakani yakiendelea

    Mashambulizi ya mpakani kati ya wanamgambo Lebanon Hezbollah na jeshi la Israel yameongezeka, na wakazi wa kusini mwa Lebanon wanakimbia makwao, wakihofia kuwa ghasia zinaweza kuongezeka zaidi.

    Shirika la Kimataifa la Uhamiaji linakadiria kuwa karibu watu 20,000 wamekimbia makazi yao tangu vita vya Israel na Hamas vilipozuka, tarehe 7 Oktoba, wengi wao kutoka maeneo ya kusini mwa nchi.

    Tumekuwa katika vijiji vilivyo kwenye mpaka katika siku za hivi karibuni, na nyingi hazina watu, maduka yamefungwa na mitaa ikiwa imeachwa.

    Katika jiji la kusini la Tiro, mamia ya watu, bila mahali pa kwenda, wamepata hifadhi katika shule za umma ambazo zimegeuzwa kuwa makao.

    Ijapokuwa mashambulizi ya mpakani yameshika kasi, vurugu hizo hadi sasa zimedhibitiwa.

    Lakini wengi hapa bado wanakumbuka uharibifu ulioletwa na vita vya mwezi mzima kati ya Israeli na Hezbollah, na wanaogopa kwamba historia inaweza kujirudia.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  9. Israel yasambaza vijikaratasi huko Gaza kuomba msaada wa kutafuta mateka

    Jeshi la Israel limesambaza vijikaratasi kaskazini mwa Gaza kuomba habari kuhusu mateka wanaoshikiliwa na Hamas - na kutoa ulinzi na fidia kama malipo.

    Vijikaratasi hivyo vilivyoandikwa - kwa Kiarabu zinasema: "Ikiwa nia yako ni kuishi kwa amani na kuwa na maisha bora ya baadaye kwa watoto wako, fanya kitendo cha kibinadamu mara moja kwa ushiriki habari zilizothibitishwa na muhimu kuhusu mateka wanaozuiliwa katika eneo lako.

    "Jeshi la Israel linakuhakikishia kwamba litawekeza juhudi kubwa katika kukupa usalama wewe na nyumba yako, na utapata zawadi ya kifedha. Tunakuhakikishia usiri kwa hili."

    Lakini shirika la habari la Reuters lilipata mtu mmoja akirarua kijikaratasi cha kuomba msaada.

    "Hatujali, fanya chochote unachotaka [Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu], sisi sote huko Gaza tunakuambia, tunapinga, kutoka mashariki hadi magharibi," mtu huyo alisema, huku umati uliomzunguka ukipiga makofi.

    "Ikiwa wanataka kutupiga kwa mabomu, wanaweza pia kutupiga kwa mabomu tukiwa hapa, hatutaondoka," mtu huyo, Abu Ramadan, aliendelea.

    "Hatutahamishwa wala kuhama, tumepoteza makazi na maisha yetu. “Tunaishi katika sehemu hii isiyo salama na hakuna mahali pa kulala, hakuna chakula, hakuna maji, hakuna hata maji yanayofaa kwa wanyama, lakini namshukuru Mungu, tutakaa, tutakaa hapa hadi tupate ushindi Mungu akipenda.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  10. Watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wawateka karibu raia 40 nchini Chad na Cameroon

    Takriban raia 40 wa Chad na Cameroon wametekwa nyara katika mji wa Touboro kaskazini mwa Cameroon, meya wa eneo hilo amesema.

    Celestin Yandal aliambia BBC kwamba watu wanaoshukiwa kuwa majambazi waliwalenga na kuwavizia wafanyabiashara wa Chad Jumapili Oktoba 22, walipokuwa wakirejea nyumbani kutoka soko la Touboro ambako kwa kawaida hufanya biashara ya ng'ombe.

    Alisema watu wengine "wanaoondoka Chad kwenda Cameroon, wakiwemo wanafunzi, na wale wanaorejea kwenye mpaka wa Chad" pia walifukuzwa.

    Wizara ya Usalama wa Umma ya Chad ilifichua kuwa vikosi vyao vya usalama mpaka sasa vimewaachia huru mateka wanane ambao wanaripotiwa kuwa salama.

    Wizara ya Ulinzi ya Cameroon bado haijajibu ombi la BBC la kutoa maoni yake kuhusu hatua zilizochukuliwa kuwaokoa mateka wa Cameroon, lakini afisa mmoja wa usalama alisema wanajeshi wanajitahidi kuwakomboa waliotekwa nyara.

    Cameroon na Chad zinashiriki mpaka wa kilomita 1100 uliozongwa na visa vya utekaji nyara, wizi na shughuli zingine haramu.

    Nchi hizo mbili zinazokabiliwa na migogoro ya kiusalama hivi majuzi ziliazimia kuzidisha ushirikiano ili kulinda raia na mali zao.

  11. Watu wataanza kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya chakula'

    Hebu turejee sasa Gaza, ambapo ndege za Israel zilishambulia zaidi ya maeneo 400 katika muda wa saa 24 zilizopita - jeshi la Israel linasema kuwa linalenga miundo mbinu ya Hamas.

    Emad Abuaassi, Mpalestina aliyehamia Gaza kutoka Blackpool nchini Uingereza chini ya mwaka mmoja uliopita, anasema amekuwa akiishi na zaidi ya watu 50 wa familia yake katika nyumba ya kaka yake huko Khan Younis.

    Yuko na mke wake, Stephanie, na watoto wao wanne.Asubuhi hii aliweza kupata pasta lakini hakuwa na mkate.

    Katika ujumbe kwa BBC, anasema: "Nadhani katika siku mbili, tatu zijazo watu wataanza kuuana kwa ajili ya chakula kidogo hapa.

    "Wewe nenda kanunue mkate kidogo, utaona watu wanachomana visu kwa ajili ya mfuko wa mkate."

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  12. Tazama mateka aliyeachiliwa na Hamas akimsalimia kwa mkono mtekaji wake

    Tumesikia hivi punde kutoka kwa Yocheved Lifschitz, 85, ambaye aliachiliwa jana usiku kutoka Gaza na Hamas.

    Picha za wakati alipoachiliwa zinaonyesha akiwasalimu kwa mkono mtu mwenye bunduki wa Hamas.

    Hapo awali binti yake Sharone aliiambia BBC kwamba ishara hiyo ililingana na tabia ya mama yake: "Ni yeye."

    Katika mkutano wa wanahabari alisema alitekwa nyara kutoka kwenye nyumba yake , akapigwa kwa fimbo, na kushikiliwa kwenye mahandaki chini ya Gaza kwa wiki mbili, kabla ya kuachiliwa jana usiku.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  13. Kupigwa kwa vijiti, kulala kwenye godoro ndani ya handaki na milo ya tango na jibini

    Yocheved Lifschitz anaelezea mazingira ambayo yeye na mateka wenzake waliwekwa, ambayo anasema yalikuwa safi.

    Anasema walilala kwenye magodoro sakafuni kwenye mahandaki chini ya Gaza, huku daktari akija kuwatembelea kila baada ya siku mbili hadi tatu.

    Mateka ambaye alijeruhiwa vibaya katika ajali ya pikipiki akiwa njiani kuelekea Gaza alitibiwa majeraha yake.

    Lifschitz anaongeza kuwa mhudumu wa afya alikuja kuwaona ili kuwaletea dawa walizohitaji.

    Haya ndiyo tuliyosikia wakati wa mkutano huo wa habari na mateka aliyeachiliwa huru wa Hamas, Yocheved Lifschitz, katika hospitali ya Tel Aviv.

    • Mzee huyo mwenye umri wa miaka 85 alisema"amepitia makubwa "na alipata michubuko alipokuwa akitekwa nyara kutoka kwa kibbutz yake huko Israel kwa pikipiki.
    • Akisaidiana kutoa simulizi ya mama yake , binti yake Sharone - ambaye aliwasili Tel Aviv kutoka London asubuhi ya leo - alisema Lifschitz na mateka wenzake walipigwa kwa fimbo.
    • Sharone pia alisema mama yake alishuhudia"mtandao mkubwa" wa mahandaki chini ya ardhi yanayoendeshwa na Hamas, ambao aliufananisha na "utando wa buibui"
    • Sharone alisema baada ya kufika Gaza, watekaji wa mama yake walisema"wanaamini katika Quran"na kwa hivyo hawatamdhuru.
    • Lifschitz mwenyewe aliendelea kuelezea hali safi na walinzi ambao walitunza "kila undani".Walilishwaj ibini nyeupe na tango- chakula ambacho watekaji pia walikila .
    • Akizungumzia mateka wengine waliochukuliwa na Hamas, Sharone alisema mama yake alihisi"hadithi haijaisha hadi kila mtu arudi"

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  14. Mahakama ya Kenya yaongeza muda wa amri ya kuzuia kutumwa kwa polisi nchini Haiti

    Mahakama Kuu ya Kenya imeongeza muda wa amri ya kuzuia kutumwa kwa polisi hadi Haiti au nchi nyingine yoyote ikisubiri kusikilizwa zaidi.

    Mapema mwezi huu mahakama ilisema walalamishi hao wameibua masuala muhimu ya kitaifa na maslahi ya umma.

    Kenya ilikuwa imejitolea kuongoza kikosi cha kimataifa kwenda Haiti kusaidia kukomesha ghasia za magenge. Pia iliahidi kupeleka maafisa wake 1000 kwa misheni hiyo.

    Ekuru Aukot aliyekuwa mgombeaji urais na mmoja wa walalamishi alisema katiba hailengi kutumwa kwa polisi nje ya nchi.

    Aliongeza kuwa atalishtaki Baraza la Mawaziri kwa kudharau mahakama baada ya wao kuidhinisha kutumwa licha ya agizo la mahakama.

    Bunge litahitaji kuidhinisha idhini hiyo kabla ya kuanza kutumwa.

    Hata hivyo, timu ya wanasheria wanaowakilisha bunge la kitaifa iliambia mahakama kwamba bunge hilo haliwezi kujadili suala hilo hadi maagizo yatakapoondolewa.

    Haiti imekumbwa na ghasia za magenge kwa miezi kadhaa. Kumekuwa na visa 3000 vya mauaji na visa 1500 vya utekaji nyara kwa ajili ya fidia kulingana na Umoja wa Mataifa.

    Waziri Mkuu Ariel Henry alikuwa ametoa wito wa usaidizi wa kimataifa akisema serikali imezidiwa nguvu.

    Unaweza pia kusoma

  15. Mamia ya wafanyikazi washindwa kujitokeza kutoka mgodi wa Afrika Kusini

    Zaidi ya wafanyakazi 500 katika mgodi mmoja nchini Afrika Kusini wamekuwa chini ya ardhi tangu Jumapili katika kile kinachoonekana kuwa mzozo kati ya vyama viwili vya wafanyakazi.

    Chama cha Kitaifa cha Wafanyakazi wa Migodi (NUM) kilisema wafanyakazi katika mgodi wa One Gold Modder East karibu na Johannesburg walikuwa wanazuiliwa chini ya ardhi kinyume na matakwa yao.

    Taarifa ya NUM ilisema: "NUM inatoa wito kwa vyombo vya kutekeleza sheria nchini Afrika Kusini kuingilia kati na kwenda chini chini na kuwakamata wahuni wanaowashikilia wanachama wetu kinyume na matakwa yao."

    Hata hivyo, chama pinzani cha Chama cha Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (Amcu), kilisema wafanyakazi wengi walikuwa wakifanya maandamano kushinikiza mgodi huo kuitambua Amcu.

    Wawakilishi kutoka mgodi wenyewe wameomba amri ya mahakama ili kukomesha kile ambacho wamekielezea kama kuketi chini ya ardhi kinyume cha sheria.

  16. Wizara ya Afya Gaza: Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel tangu tarehe 7 Oktoba yafikia 5,300.

    Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imeripoti Jumanne kuwa idadi ya vifo katika ukanda huo tangu kuanza kwa vita kati ya Hamas na Israel imeongezeka na kufikia watu 5,300 huku watu wengine wengine 18,000 wakijeruhiwa.

    Mkurugenzi wa hospitali za Ukanda wa Gaza, Muhammad Zaqout, alisema katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita, hospitali hizo zilipokea watu 120 waliofariki na wengine kadhaa kujeruhiwa.

    Alieleza kuwa wahudumu kumi na saba waliokuwa wakifanyakazi ya kuwasafirisha majeruhi waliuawa. Aliongeza kuwa magari 25 ya kubebea wagonjwa pia yameharibiwa.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  17. Waasi wa ADF wawaua raia 23 mjini Beni, DRC

    Takriban raia 23 waliuawa katika shambulio la asubuhi na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) huko Oicha , Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Kundi hilo limekuwa likiendesha shughuli zake katika miezi ya hivi karibuni huko Magharibi mwa Uganda na mnamo Julai lilianzisha shambulio dhidi ya shule na kuwaua wanafunzi mnamo Juni 16, 2023, katika Shule ya Sekondari ya Lhubiriha, katika mji wa mpaka wa Kusini-magharibi wa Mpondwe, wilaya ya Kasese.

    Wiki moja iliyopita waliwashambulia watalii na dereva wao katika Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth. Watatu hao waliuawa, na gari lao kuchomwa moto, shirika la Isis linaloshirikiana na ADF lilidai kuhusika na shambulio hilo

    Jeshi la Uganda UPDF na wenzao wa jeshi la DRC , FRDC wamekuwa wakipigana pamoja ili kusambaratisha kundi la waasi la ADF lenye mfungamano na Isis. Kundi hilo awali liliundwa nchini Uganda.

    Unaweza pia kusoma

  18. Watu wengi wakamatwa Nigeria kwa madai ya harusi ya wapenzi wa jinsi moja

    Vikosi vya usalama nchini Nigeria vimewakamata zaidi ya watu 70 kwa madai kwamba waliandaa karamu yawapenzi wa jinsi iliyojumuisha sherehe ya harusi kati ya wanaume wawili.

    watu hao walimamatwa Jumamosi katika mji wa Gombe, jimbo lenye Waislamu wengi kaskazini mwa Nigeria, lakinitaarifa hiyo ilithibitishwa Jumatatu.

    "Tuliwakamata washukiwa 76 wa jinsi moja wakifanya karamu ya kuzaliwa iliyoandaliwa na mmoja wao, ambaye alipaswa kumuoa bibi harusi wake wa kiume kwenye hafla hiyo," Buhari Saad, msemaji wa Kikosi cha Usalama na Ulinzi wa Raia wa Nigeria, aliliambia shirika la habari la AFP.

    Washukiwa hao ni pamoja na wanaume 59 na wanawake 17, huku 21 kati ya wanaume "wakikiri kwa utashi wao kuwa ni wapenzi wa jinsi moja ", aliongeza.

    Ni msako wa hivi punde zaidi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja nchini Nigeria, ambapo sheria ya mwaka 2014 ilikataza uhusiano wa watu wa jinsia moja na ndoa.

    Sheria hiyo ilianzisha kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa wale wanaopatikana na hatia kwa makosa hayo.

    Mwezi Agosti, vikosi vya usalama viliwakamata watu 67 kwa madai ya kuhudhuria harusi ya wapenzi wa jinsi moja katika jimbo la Delta kusini, lakini mahakama iliwaachilia kwa dhamana.

  19. Mzozo wa Israel na Hamas: Nini kilichojiri hivi punde?

    Ni saa tano kamili kwa saa za Afrika. Ikiwa ndio kwanza unajiunga nasi, haya ndiyo mapya zaidi kuhusu mzozo wa Israel na Hamas:

    • Mateka walioachiliwa: Mateka wawili wanaoshikiliwa na Hamas - Nurit Cooper, 79, na Yocheved Lifschitz, 85 - waliachiliwa jana usiku. Binti Yocheved ameiambia BBC kwamba mama yake anaonekana "yuko sawa" na ana nia ya kusambaza habari ambazo zinaweza kuwafanya watu wengi kuachiliwa. Mwanaume na mwanamke hao ni miongoni mwa watu zaidi ya 200 ambao bado wanazuiliwa ndani ya Gaza
    • Mashambulio ya mabomu Gaza: Umekuwa usiku mwingine wa mashambulizi makali ya anga huko Gaza. Jeshi la Israel linasema shabaha 400 zilipigwa katika muda wa saa linasemamaeneo 400 yamepigwa katika mud awa saa 24 zilizopita
    • Msimamo wa ukatili: Waziri Mkuu wa Israel Bejamin Netanyahu asema Israel inachukua "msimamo wa ukatili" ili "kuondoa Hamas"
    • Msaada wa hivi punde: Msafara wa tatu wa malori 20 ya misaada uliingia Gaza jana kutoka Misri - lakini mashirika ya misaada yameonya kuwa haitoshi.
    • Ziara ya Ufaransa: Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili Israel leo asubuhi kwa mazungumzo na viongozi wa Israeli

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  20. Vita vya Israel na Hamas: Binti wa mateka aliyeachiliwa huru na Hamas anasema mama 'anaonekana yuko sawa'

    Binti ya Yocheved Lifshitz, mmoja wa mateka walioachiliwa jana usiku, amemtembelea mama yake hospitalini nchini Israel na kuiambia BBC kwamba mama yake "anaonekana yuko sawa".

    "Wauguzi wanazungumza tu, wanasema yuko vizuri na ana hamu kuzungumzia yaliyompata na kutoa habari kwa familia za mateka wengine ambao alikuwa nao."

    Sharone Lifshitz alizungumza mama yake alipokuwa amelala, alimwambia mtangazaji wa BBC Radio 4 Today Mishal Husain: "Sina la kusema.

    "Nilikaa karibu naye kwa muda wa saa moja kisha tukatoka na kaka yangu yuko naye. Kila mtu amechoka sana. Amepitia mengi."

    Sharone anaongeza: "Kuona mama yangu tena ni jambo la kushangaza. Kumshika mkono, kumbusu tu uso wake, na shavu lake, ni jambo ninalojivunia sana, anashangaza."

    Sharone alizungumzia kuhusu picha zilizotangzwa za mama yake za kumuonyesha kwa muda mfupi akiwa ameshika mkono wa mmoja wa watekaji nyara.

    "Jinsi alivyotembea kisha akarudi kwa watekaji wake na kusema asante lilikuwa ya kushangaza kwangu. "Ninangoja tu kuwa na wakati mzuri naye."nimuulize mengi.

    Anaongeza: "Bado kuna zaidi ya watu 200 huko hatufai kufurahi binafsi tu bali tufanye kazi kuelekea kuachiliwa kwa kila mtu."