Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Shirika la Umoja wa Mataifa laonya operesheni ya Gaza inaweza kumalizika kesho bila mafuta zaidi

Touma anasema shirika hilo lina makao 150, mengi yakiwa ni shule.

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Risasi iliokosa shabaha yampiga raia wa Rwanda karibu na mpaka wa DRC

    Raia wa Rwanda amepigwa risasi wakati wa mapigano kati ya makundi yenye silaha karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, serikali ya Rwanda imesema.

    Tukio hilo lilitokea Jumatatu katika eneo la mpaka wa Rubavu, msemaji wa Rwanda Yolande Makolo alisema katika taarifa yake.

    "Mwanaume aliyejeruhiwa anapokea matibabu katika Kituo cha Afya cha Cyanzarwe Rubavu," aliongeza.

    Bi Makolo alisema Rwanda "ina wasiwasi mkubwa" kwa kuongezeka "kwa vitendo vya uchochezi" kwenye mpaka wake na DRC

    Alivilaumu "vikundi haramu vyenye silaha vinavyoungwa mkono na Kinshasa" kwa mapigano hayo.

    Msemaji huyo alisema Rwanda itadumisha "njia za kujihami na kuzuia" ili kujilinda dhidi ya ukiukaji wa anga na mipaka yake.

    Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka kwa serikali ya Congo.

    Mara kwa mara Rwanda imekuwa ikiishutumu Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kwa kushirikiana na chama cha Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), ambacho kinajumuisha baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa viongozi wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994. Kinshasa inapinga shutuma hizo.

    Kwa upande wake, DRC inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono wanamgambo wa M23 - kundi la waasi wa kabila la Watutsi wa Congo - madai ambayo Kigali inakanusha.

    Unaweza pia kusoma:

  2. Makumi ya watu wafariki katika ajali nyingine ya boti DRC

    Takriban watu 40 wamekufa maji baada ya boti ya abiria kupinduka kwenye mto magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wiki moja baada ya wengine 47 kufariki katika ajali sawa na hiyo.

    Boti hiyo ya mbao, inayojulikana kwa jina la nyangumi, ilikuwa imebeba abiria na mizigo, ilipopinduka kwenye mto Lulonga Jumamosi usiku.

    Tukio hilo lilitokea karibu na kijiji cha Boyeka katika jimbo la Equateur.

    Abiria hao, wengi wao wakiwa wafanyabiashara, walikuwa wakirejea kutoka katika soko la ndani kuelekea Mbandaka, mji mkuu wa jimbo hilo.

    Idadi ya vifo huenda ikaongezeka huku abiria zaidi wakiripotiwa kupotea.Zaidi ya wengine 200 walinusurika, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Ajali hiyo imekuja siku kumi baada ya boti nyingine kupinduka katika jimbo hilo hilo na kusababisha vifo vya watu kadhaa na idadi na idadi isiyojulikana ya wengine hawajulikani walipo.

    Maboti hutumiwa kama usafiri wa kawaida nchini Congo kwa sababu ya ukosefu wa barabara.

    Hata hivyo, ajali za boti hutokea mara kwa mara kwa sababu ya mizigo mingi, kutokarabatiwa na kusafiri usiku.

  3. Habari za hivi punde, Jeshi la Israeli lasema maeneo 400 yamepigwa Gaza saa 24 zilizopita

    Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema lilipiga shabaha zaidi ya 400 huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, kutoka 320 ilizotangaza katika hatua hiyo hiyo jana.

    Katika taarifa yake iliyotuma kwenye mtandao wake wa X, zamani Twitter, IDF inasema shabaha zake ni pamoja na wapiganaji wa Hamas waliopanga kurusha roketi kuelekea Israel, na shimo la handaki linaloruhusu Hamas kupenya Israeli kupitia baharini.

    Inasema pia vituo vya amri vilivyotumiwa kuweka silaha kwenye misikiti vilipigwa.

    IDF inaongeza kuwa "itaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa raia wasio na hatia".

  4. Dereva wa treni ya chini ya ardhi aliyepiga kelele za kuunga mkono Palestina London asimamishwa kazi

    Dereva wa treni jijini London amesimamishwa kazi kwa kupiga kelele za kuunga mkono Palestina.

    Mamlaka ya Usafiri wa London (TFL) inayohusika na huduma za usafiri jijini humo, ilitangaza kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.

    Maandamano ya kuunga mkono Palestina yalifanyika katika mji mkuu huo wa Uingereza siku ya Jumamosi, yakihudhuriwa na takribani watu laki moja.

    Katika tukio hilo lililotokea katika barabara ya chini ya ardhi siku hiyo hiyo na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, dereva anasikika akiimba "huru, huru" kwa kutumia mfumo wa utangazaji ndani ya treni.

    Baadhi ya abiria waliomo ndani walisikika pia wakitilia mkazo kauli hiii. "Palestina Huru" ambayo ilitumiwa mara kwa mara katika maandamano.

    TFL ilitangaza kuwa dereva huyo alisimamishwa kazi hadi uchunguzi utakapo kamilika.

    Mkurugenzi wa TFL, Glynn Barton, alisema dereva huyo alibainika kutumia mfumo wa ndani ya treni vibaya.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  5. Macron awasili Israel kukutana na Netanyahu

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion nchini Israel, na atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu baadaye leo.

    Madhumuni ya ziara hiyo ni kuonesha mshikamano wa Ufaransa na Israel, kusaidia katika kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas, na kuzuia kuongezeka kwa mzozo wa sasa, washauri wake waliiambia Reuters.

    Macron pia atakutana na Rais wa Israel Isaac Herzog, na viongozi wa siasa kali Benny Gantz na Yair Lapid kutoka upinzani wakati wa ziara yake.

  6. Rubani ambaye hakuwa zamu kazini ashutumiwa kwa kutaka kuiangusha ndege

    Rubani ambaye hakuwa zamu kazini ameshtakiwa kwa makosa 83 ya kujaribu kuua, baada ya kudaiwa kujaribu kuangusha ndege ya abiria wakati wa safari ya ndege Jumapili usiku.

    Mshukiwa alikuwa ameketi kwenye chumba cha marubani cha ndege ya Alaska Airlines nyuma ya nahodha na afisa wa kwanza, kulingana na taarifa ya shirika la ndege.

    Hati ya polisi ilimtaja mshukiwa kama Joseph David Emerson, 44.

    Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Everett, Washington, kuelekea San Francisco, California, ikiwa na abiria 80.

    Wafanyakazi wa Alaska Airlines Flight 2059 waliripoti tukio hilo kwa udhibiti wa safari za anga.

    Katika rekodi ya mawasiliano ya udhibiti wa usafiri wa anga, mmoja wa marubani alisikika akisema: "Tuna mtu ambaye alijaribu kuzima injini nje ya chumba cha rubani, na hasikii kama anasababisha shida yoyote. sasa hivi."

    "Nadhani amrishwa rubani aliongeza. Aliomba kuwepo kwa polisi "mara tu tunapoingia chini na kuegesha".

    Ndege hiyo, inayoendeshwa na Horizon Air, ilipaa saa kumi na moja unusu jioni kwa saa za huko na kufika San Francisco saa moja unusu jioni.

    Abiria Aubrey Gavello aliambia ABC News kwamba waliokuwemo hawakujua chochote kilikuwa kibaya na ndege hiyo hadi mhudumu wa ndege hiyo alipotangaza kwamba ndege hiyo ilihitaji kutua mara moja, baadaye akataja dharura ya kiafya.

    Bi Gavello alikiambia kituo kwamba alimsikia mhudumu wa ndege akimwambia mshukiwa: "Tutakuwa sawa, ni sawa, tutakushusha kwenye ndege."

    "Kwa hivyo nilidhani ilikuwa dharura kubwa ya matibabu," alisema.

    Abiria mwingine alikiambia kituo hicho kuwa hali hiyo ilishughulikiwa kitaalamu na abiria hawakufahamu kuhusu mgogoro huo.

    Katika taarifa, Alaska Airlines ilisema abiria wote waliokuwemo waliweza kusafiri kwa ndege ya baadaye.

  7. Tazama Video: Daraja laangushwa na mlipuko Ujerumani

    Daraja la barabara kuu lililipuliwa katika mlipuko uliodhibitiwa karibu na mji wa Beselich nchini Ujerumani.

    Daraja hilo la Kerkerbachtal lenye urefu wa mita 135 (futi 443) liliporomoka ndani ya sekunde chache baada ya vilipuzi vilivyowekwa kwenye nguzo zake kulipuliwa.

    Daraja hilo, lililojengwa mwaka wa 1960, lilikuwa sehemu ya njia ya zamani inayovunjwa sasa. Barabara mpya inatengenezwa mahali pake, ikienda mbali zaidi na mji.

  8. Jeshi la Israel laishambulia Hezbollah kwa mabomu kujibu mashambulizi ya roketi.

    Jeshi la Israel limesema lilifanya uvamizi katika eneo la wapiganaji wa Hezbollah nchini Lebanon, kujibu mashambulizi ya roketi kaskazini mwa Israel.

    Shambulio hilo lililenga miundombinu ya Hezbollah, ikiwa ni pamoja na mnara na jumba la kijeshi, kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa kwenye akaunti ya jeshi la Israel ya tovuti ya X, zamani ikiitwa Twitter.

    Jeshi lilichapisha video inayoonyesha shambulizi la anga kwenye jengo, na lilisema lilijibu roketi zilizorushwa kutoka upande wa Lebanon mapema Jumatatu.

    BBC haikuthibitisha uhalisi wa video hiyo iliyochapishwa na jeshi la Israel.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  9. Mzozo wa Israel na Hamas kwa picha: Watu waliojeruhiwa wakimbizwa katika hospitali ya Khan Younis huko Gaza

    Picha zilizowasilishwa na mashirika ya habari katika muda wa saa chache zilizopita zinaonyesha watu waliojeruhiwa wakipelekwa katika Hospitali ya Nasser Medical, katika mji wenye msongamano wa watu wa Khan Yunis uliopo kusini mwa Gaza.

    Kwenye Telegram, chaneli za Hamas zilisema watu katika mji huo wamejeruhiwa na mashambulizi mengi ya anga na uvamizi wa Israel, na kudai mashambulio hayo yalisababisha uliharibu kituo cha mafuta na kusababisha moto.

    Serikali ya Israel ilikuwa imewaambia watu milioni 1.1 kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini kabla ya uvamizi wa ardhini unaotarajiwa. Hii imesababisha mamia kwa maelfu ya watu kutafuta hifadhi katika Khan Younis, hata kama Israel imeendelea kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya Gaza likiwemo eneo la kusini.

    Tahadhari: Baadhi ya wasomaji wanaweza kuona picha zifuatazo kuwa za kuhuzunisha.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  10. Obama: Jinsi Israel inavyopigana vita ni muhimu

    Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ameandika makala ambayo anatoa mawazo yake kuhusu mkakati wa Israel kuelekea kulisambaratisha kundi la Hamas na juhudi za kidiplomasia za Marekani katika eneo hilo.

    Anaanza kwa kusema kwamba Biden, ambaye alihudumu chini yake kama makamu wake wa rais, alikuwa sahihi kutangaza "mshikamano" wa Marekani na watu wa Israeli baada ya shambulio la kushangaza la Hamas.

    "Ninaunga mkono kikamilifu wito wa Rais Biden kuhusu Marekani kuunga mkono mshirika wetu wa muda mrefu katika kukabiliana na Hamas, na kubomoa uwezo wake wa kijeshi," anasema.

    "Lakini hata tunapoiunga mkono Israel, tunapaswa pia kuwa wazi kwamba jinsi Israel inavyotekeleza vita hivi dhidi ya Hamas ni muhimu," anaendelea.

    Anabainisha kuwa uongozi wa Hamas "unaonekana kujificha kimakusudi miongoni mwa raia, na hivyo kuwahatarisha watu walewale wanaodai kuwawakilisha" na anasisitiza kuwa Israel lazima ifanye kila iwezalo ili kuepuka kuwadhuru raia wa Palestina.

    "Mkakati wowote wa kijeshi wa Israeli ambao unapuuza gharama za kibinadamu unaweza kurudisha nyuma," anasema.

    Obama pia anatoa wito wa msaada zaidi kwa walioruhusiwa kufika Gaza na anasema kuwa nchi za Kiarabu ambazo zinafanya kazi ya kurejesha uhusiano na Israel lazima pia zifanye kazi kutafuta utaifa wa Palestina kwa watu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  11. Mzozo wa Israel na Hamas: Marekani inapinga wito wa kusitishwa kwa mapigano

    Sasa si wakati mwafaka wa kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, maafisa wakuu wa White House na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wamesema.

    "Hatuamini kuwa huu ni wakati wa kusitisha mapigano," msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumatatu.

    "Israel ina haki ya kujilinda. Bado wana kazi ya kufanya kuufuata uongozi wa Hamas."

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Mathew Miller aliongeza katika mkutano tofauti wa habari kuwa: "Tunachoendelea kufanya, kuhusiana na suala hili, ni kuzingatia upatikanaji wa msaada wa kibinadamu kwa ajili ya Gaza."

    Miller aliongeza kuwa mjumbe wa Marekani aliyeteuliwa kusimamia mzozo huo, David Satterfield, "anafanya kazi kwa bidii kuanzisha mifumo inayoendelea ya utoaji wa misaada ya kibinadamu, na tunafanya bidii ili kuweka maeneo ambayo raia wanaweza kuwa salama ili kuepuka madhara, ndani ya Gaza. .”

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  12. Mateka raia walioachiliwa na Hamas wawasili Tel Aviv

    Mateka wawili wazee Waisrael walioachiliwa na Hamas Jumatatu Nurit Cooper, 79, na Yocheved Lifshitz, 85 - - wamewasili Tel Aviv kwa matibabu.

    Hamas ilisema iliwaachilia wanawake kwa sababu za "kibinadamu" na kiafya.

    Israel imeishukuru Misri kwa usaidizi wake katika upatanishi uliowezesha kuachiliwa kwao na Shirika la Msalaba Mwekundu kwa "jukumu muhimu" ililofanya kuwarudisha wawili hao nyumbani.

    Mume wa Bi Cooper Amiram, 85, na mume wa Bi Lifshitz Oded, 83, bado wanazuiliwa na Hamas huko Gaza, kulingana na maafisa wa Israeli.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mauaji ya Kibbutz:Jinsi Hamas walivyofanya shambulio lisilofikirika
    • Uchambuzi:Je, uvamizi wa ardhini wa Israel dhidi ya Gaza unaweza kuafikia malengo yake?
    • Historia:Masuala muhimu unayopaswa kujua kuhusu mzozo kati ya Israel na Palestina
    • Kiini cha mzozo:Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
    • Hamas:Lifahamu kundi la wapiganaji wa Palestina lililoivamia Israel kupitia angani, baharini na nchi kavu
    • Mossad:Mbinu ,mikakati na kuwatumia wanawake katika shirika la ujasusi la Israel walipa ufanisi katika operesheni zake
  13. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 24.10.2023