Je mataifa mengine yanaweza kuingilia vita vya Israel – Gaza? Tunajibu maswali yako

Hali kwa watu wa Gaza inazidi kuwa mbaya, huku maji, chakula, nguvu za umeme na dawa vikiwa haba.

Moja kwa moja

  1. Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel yakanusha mapatano ya kusitisha vita kusini mwa Gaza

    th

    Chanzo cha picha, X/Netanyahu

    Israel inaonekana kukanusha ripoti za kusitisha mapigano kusini mwa Gaza, nusu saa baada ya vyanzo vya usalama nchini Misri kuliambia shirika la habari la Reuters kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano yalikuwa yamekubaliwa kuwiana na kufunguliwa tena kwa kivuko cha Rafah.

    Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu inasema: "Kwa sasa hakuna suluhu na misaada ya kibinadamu huko Gaza kwa kuwaruhusu wageni kutoka nje."

    Israel yatangaza kuwahamisha jamii karibu na mpaka wa Lebanon

    Jeshi la Israel limetangaza mpango wa kuzihamisha jamii za kaskazini mwa Israel karibu na mpaka na Lebanon.

    Wakazi wa jamii 28 ambazo ziko ndani ya kilomita 2 (maili 1.24) kutoka mpakani watahamishwa hadi "nyumba za wageni zinazofadhiliwa na serikali", Jeshi la Ulinzi la Israeli lilisema.

    Raia mmoja wa Israel aliuawa katika shambulizi la kombora la Hezbollah kwenye kijiji kimoja karibu na mpaka siku ya Jumapili, kulingana na jeshi la Israel.

    Israel imefanya mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya Lebanon, ikilenga miundombinu ya kijeshi ya kundi la wanamgambo wa Lebanon Hezbollah.Hakuna majeruhi wameripotiwa.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

  2. Habari za hivi punde, Usitishaji mapigano wakubaliwa kusini mwa Gaza - ripoti

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Marekani, Israel na Misri zimekubaliana kusitisha mapigano kusini mwa Gaza ili kuwiana na kufunguliwa tena kwa kivuko cha mpaka cha Rafah, vyanzo viwili vya usalama vya Misri vimeliambia shirika la habari la Reuters.

    Reuters ilisema usitishaji wa mapigano ungeanza saa 06:00 GMT - sasa - huku kukiwa na ripoti za vyombo vya habari kwamba kivuko kinachodhibitiwa na Misri kitafunguliwa tena kwa wakati mmoja.

    Vyanzo viwili vya usalama vya Misri vimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba usitishaji vita kusini mwa Gaza utaendelea kwa saa kadhaa - ingawa hawajaweka wazi kuhusu muda halisi.

    Pia walisema Israel, Misri na Marekani zimekubali Rafah "itafunguliwa hadi 14:00 GMT" Jumatatu kama ufunguzi wa kwanza wa siku moja.

    Walipoulizwa kuthibitishwa, jeshi la Israel na Ubalozi wa Marekani nchini Israel hawakuwa na maoni ya mara moja, Reuters inaongeza.

    Bado hatujaweza kuthibitisha ikiwa kivuko kimefunguliwa.

    Hamas inasema haina taarifa kuhusu usitishaji vita - ripoti

    Mkuu wa ofisi ya vyombo vya habari vya Hamas anasema hawana taarifa kuhusu makubaliano ya kusitisha vita kwa sababu za kibinadamu yaliyokubaliwa kusini mwa Gaza, kulingana na Reuters.

    Salama Marouf ameliambia shirika hilo la habari kwamba hawajapata uthibitisho wowote kutoka upande wa Misri kuhusu nia ya kufungua kivuko cha Rafah kati ya Gaza na Misri.

    Kivuko cha Rafah kinaweza kufunguliwa kwa muda mfupi pekee - Marekani

    Marekani inatarajia kuwa hali katika kivuko cha Rafah kati ya Misri na Gaza "itabaki kuwa shwari na haitabiriki" huku kukiwa na ripoti kwamba kitafunguliwa saa 09:00 kwa saa za huko - karibu sasa.

    Ikitoa ushauri kwa Wamarekani huko Gaza, wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema haijafahamika iwapo watu wataruhusiwa au kwa muda gani kupita kivuko cha kusini.

    "Ikiwa utatathmini kuwa ni salama, unaweza kutaka kusogea karibu na kivuko cha mpaka cha Rafah - kunaweza kuwa na taarifa ndogo sana kama kivuko kikifunguliwa na kinaweza kufunguliwa kwa muda mfupi," inasema.

    Maafisa wanashughulikia "chaguo zinazowezekana za kuondoka" kwa Wamarekani huko Gaza.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

  3. Polisi wa Uganda walitibua njama ya kulipua makanisa - Museveni

      • Author, Wycliffe Muia
      • Nafasi, BBC News
    Rais Yoweri Museveni alisema majeshi ya Uganda yalifanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa ADF

    Chanzo cha picha, Ugandan Presidency/X

    Maelezo ya picha, Rais Yoweri Museveni alisema majeshi ya Uganda yalifanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa ADF

    Polisi wa Uganda walizuia shambulio la bomu dhidi ya makanisa lililofanywa na kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) katikati mwa wilaya ya Butambala, Rais Yoweri Museveni amesema.

    Wanamgambo hao wanaohusishwa na Islamic State siku ya Jumapili walikuwa wakipanga kutega mabomu mawili katika makanisa ya Kibibi, karibu kilomita 50 kutoka mji mkuu Kampala, Bw Museveni aliandika kwenye mtandao wa X, ambao zamani ilijulikana kama Twitter.

    Lakini vifaa hivyo "viliripotiwa kwa polisi na kuhariwa", aliongeza.

    Rais alisema mabomu hayo yalifichwa kama mifumo ya anwani na zawadi kwa wachungaji wa eneo hilo. Ziliripotiwa na wananchi waliokuwa na mashaka alisema.

    Mapema siku hiyo hiyo, Bw Museveni alisema vikosi vya Uganda vilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya ngome nne za ADF katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    "Inaonekana idadi kubwa ya magaidi waliuawa," rais alisema.

    Alionya kwamba ADF wanaotoroka "wanaingia tena Uganda na kujaribu kufanya vitendo vya kigaidi vya kubahatisha".

    Mwezi Juni, wanamgambo wa ADF waliwaua watu 42, wakiwemo wanafunzi 37 katika shule ya upili magharibi mwa Uganda karibu na mpaka na DR Congo.

    Lilikuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya ADF nchini humo.

    Maelezo zaidi:

  4. Daniel Noboa achaguliwa rais wa umri mdogo zaidi nchini Ecuador

    Daniel Noboa

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mfanyabiashara Daniel Noboa

    Mfanyabiashara Daniel Noboa anatarajiwa kuwa rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Ecuador, akiwa na umri wa miaka 35.

    Bw Noboa alishinda uchaguzi wa Jumapili kwa 52.3% ya kura, mbele ya Luisa González 47.7%.

    Alikubali kushindwa na kumpongeza mpinzani wake. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 35, wa chama cha National Democratic Action, ni mtoto wa Álvaro Noboa, ambaye aligombea urais mara tano bila mafanikio.

    Bw Noboa atakuwa na miezi 17 pekee madarakani hadi uchaguzi ujao.

    Atatawala kuanzia mwisho wa Novemba 2023 hadi Mei 2025, kwa sababu uchaguzi wa sasa ulianzishwa mapema wakati Rais anayemaliza muda wake Guillermo Lasso alivunja bunge huku kukiwa na kesi ya kumuondoa madarakani.

    Anaweza kuwania tena muhula wa urais wa 2025-29 ikiwa anataka.

    Bw Noboa ataapishwa kuwa rais tarehe 25 Novemba, siku tano kabla ya kutimiza miaka 36.

    Kufuatia ushindi wake katika duru ya pili ya upigaji kura, Bw Noboa aliwaambia wafuasi wake: "Kesho tunaanza kazi ya Ecuador hii mpya, tunaanza kufanya kazi ya kujenga upya nchi iliyoathiriwa vibaya na ghasia, ufisadi na chuki."

    Ecuador imekumbwa na ongezeko la ghasia za magenge katika miaka ya hivi karibuni na kampeni ya urais ilikumbwa na mauaji ya mwezi Agosti ya mgombea Fernando Villavicencio.

  5. Kilo 11 za dawa inayoshukiwa kuwa Cocaine zapatikana kwenye kiti cha magurudumu

    Mshukiwa huyo anasema aliazimwa kiti hicho cha magurudumu na rafiki yake

    Chanzo cha picha, HONG KONG GOVERNMENT

    Maelezo ya picha, Mshukiwa huyo anasema aliazimwa kiti hicho cha magurudumu na rafiki yake

    Maafisa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong wamepata kilo 11 za dawa inayoshukiwa kuwa ya Cocaine ikiwa imefichwa kwenye kiti cha magurudumu cha umeme.

    Dawa hiyo yenye thamani ya dola milioni 1.5, ilipatikana wakati mwanamume mwenye umri wa miaka 51 alipokuwa akifanyiwa ukaguzi wa forodha siku ya Jumamosi.

    Mwanamume huyo, ambaye aliwasili kutoka nchi ya kisiwa cha Caribbean ya Sint Maarten kupitia mjini Paris siku ya Jumamosi, amekamatwa.

    Anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha jela iwapo atapatikana na hatia ya kusafirisha dawa hatari za kulevya.

    Kulingana na maafisa wa forodha, mshukiwa alileta kiti cha magurudumu kama moja ya mizigo miwili iliyokaguliwa.

    Uchunguzi zaidi uliamriwa wakati wafanyikazi walipotilia shaka na wakapata ushahidi kwamba mto wa kiti ulikuwa umeshonwa tena.

    Mwanamume huyo, ambaye sio mkazi wa Hong Kong na anayekabiliwa na changamoto ya uhamaji, inasemekana aliwaambia maafisa kuwa yeye ni mkurugenzi wa kampuni ya kukodisha magari na kwamba aliazimwa kiti hicho cha magurudumu na rafiki yake.

    Uchunguzi wa tukio hilo umeanzishwa.

    Maafisa wa forodha walisema katika hatua ya kukabiliana na visa kama hivyo wataimarisha ukaguzi kwa wageni kutoka "maeneo hatarishi" ili kukabiliana na shughuli za kimataifa za usafirishaji wa dawa za kulevya.

    Takriban watu 178 walikamatwa kuhusiana na visa kama hivyo mwaka jana.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Israel 'haina nia ya kuikalia Gaza', asema balozi

    Israel "haina nia ya kuikalia Gaza au kusalia Gaza", balozi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa amesema.

    Akihojiwa kwenye kituo cha Habarii cha CNN, Gilad Erdan alisema kuwa "kwa vile tunapigania uhai wetu... njia pekee ni kuwaangamiza Hamas, hivyo itatubidi kufanya chochote kinachohitajika".

    Alipoulizwa ni nani atawale Ukanda wa Gaza ikiwa Israel itaiondoa Hamas, Bw Erdan alisema Israel "haifikirii kitakachotokea siku moja baada ya vita".

    Kauli ya Bw Erdan inajiri baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuulizwa kwenye kipindi 60 Minutes za CBS kama angeunga mkono uvamizi wa Israel Gaza.

    Biden alijibu kwamba "itakuwa ni makosa kwa Israeli kuikalia Gaza tena", lakini akasema ni "hatua ya lazima" kuwaondoa "wenye msimamo mkali".

    Alipoulizwa kama Hamas inapaswa "kuondolewa kabisa", rais alijibu: "Ndiyo ninafanya." Aliendelea kusema kwamba "kuna haja ya kuwa na mamlaka ya Palestina, kuna haja ya kuwa na mustakabali ya taifa la Palestina".

  7. Hifadhi ya mafuta katika hospitali za Gaza huenda ikaisha baada ya saa 24, UN yaonya

    Watoto wakilia Oktoba 15, 2023 mjini Khan Yunis, Gaza.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watoto wakilia Oktoba 15, 2023 mjini Khan Yunis, Gaza.

    Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hifadi ya mafuta katika hospitali za Gaza inatarajiwa kudumu takriban saa 24 zaidi.

    "Kuzimwa kwa jenereta kungeweka maisha ya maelfu ya wagonjwa hatarini," ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu ilisema kwenye tovuti yake.

    Haya yanajiri baada ya mashirika kadhaa ya misaada kutoa wito wa kufikia Gaza ili kutoa msaada wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na mafuta na maji.

    Usiku wa kuamkia leo, Ghassan Abu Sitta, daktari wa upasuaji kutoka Uingereza na Palestina anayefanya kazi kutoka Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka huko Gaza, alionya kuwa wafanyakazi wa hospitali yake hawana vifaa vya kutosha vya kusaidia watu.

    "Kwa upande wa vifaa vya matibabu, sisi hutumia vifaa vya matibabu vya mwezi au mwezi na nusu kila siku katika dharura hii," aliiambia BBC.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

  8. Hajambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Jumatatu 16.10.2023.