Maelfu wapanga foleni kumuaga mhubiri TB Joshua
Mwili wake umekuwa katika kanisa Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos ambapo atazikwa Ijumaa.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Rais Museveni aamuru kukamatwa kwa wanaosambaza uvumi kuwa amefariki

Chanzo cha picha, Getty Images
Raia wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuna haja ya kuwakamata raia wa taifa hilo wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya.
Akizungumza na vyombo vya habari rais huyo ameshutumu wale wanaosambaza habari kwenye mitandao kwamba yeye amefariki.
Amesema kwamba wale wanaohusika na habari kama hizo wanapaswa kusakwa na kukamatwa kwa kuwa wamekuwa wakipotezea watu muda wao.
Alisema: Tatizo jingine ambalo linapaswa kutatutiliwa ambalo sio la kiusalama bali la kijinga ni mitandao ya kijami. Mitandao ya kijami imekuwa ikisema kwamba museveni amefariki. Hivyobasi naitaka idara ya usalama kusuluhisha tatizo hilo.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Nataka wawafuatilie kwa haraka wale wanaozua uvumi kama huo.
Twitter Kumekuwa na uvumi katika siku za hivi karibuni kwamba kiongozi huyo alikuwa amesafirishwa kutoka nchini Uganda na kupelekwa nchini Ujerumani akiwa katika hali mahututi baada ya kuugua maradhi ya tatizo la kupumua linalohusishwa na ugonjwa wa corona.
Hatahivyo akizungumza Rais Museveni alisema kwamba wale wanaozua habari kama hizo wanapaswa kufuatiliwa na vyombo vya usalama ili kukamatwa haraka iwezekanavyo.
Michezo ya Olimpiki kufanyika bila mashabiki

Chanzo cha picha, Getty Images
Watazamaji wamezuiwa kushuhudia michuano ya Olimpiki wakati hali ya dharura ikitangazwa Japan kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.
Waziri wa olimpiki Tamayo Marukawa ametoa tangazo hilo baada ya majadiliano na maafisa na waandaaji Alhamisi jioni.
Hali ya dharura mjini Tokyo itakuwepo wakati wote wa michezo hiyo, kupambana na janga la corona. Waziri Mkuu Yoshihide Suga amewaambia waandishi wa habari kuwa dharura hiyo itaanza kufanya kazi kuanzia tarehe 12 Julai mpaka tarehe 22 mwezi Agosti.
Vilabu vya pombe na migahawa haitaruhusiwa kuuza vinyaji vya kilevi na kuamriwa kufungwa majira ya saa mbili za usiku saa za mji huo. Maambukizi ya virusi vya corona yanaongezeka Tokyo wakati sherehe za ufunguzi wa michezo hiyo zikitarajiwa tarehe 23 mwezi Julai.
Kumekuwa na upinzani mkubwa kuhusu ufanyikaji wa michezo hiyo Japan, ukitaka michuano hiyo iahirishwe au kufutwa kabisa.
''Kwa kuzingatia hali ya aina ya virusi na kutochangia maambukizi kusambaa tena nchi nzima, tunapaswa kuimarisha hatua tunazozichukua dhidi ya ugonjwa huu,'' alisema waziri mkuu.
Kwa kuzingatia hali ilivyo, tutatangaza hali ya dharura Tokyo.'' Saa kadhaa kabla ya uamuzi wa kuwazuia mashabiki, Mkuu wa michuano ya Tokyo ya 2020 Seiko Hashimoto alisema: ''Tunahitaji kutoa ujumbe wenye nguvu na rahisi kueleweka kwa mantiki ya kuzuia kuenea zaidi kwa virusi''.
Tangazo hili limetolewa baada ya mkutano kati ya kamati ya maandalizi, serikali na rais wa kamati ya olimpiki, Thomas Bach, ambaye tayari amewasili Japan.
Michuano ya Olimpiki imepangwa kufanyika jijini Tokyo kati ya tarehe 23 mwezi Julai na 8 mwezi Agosti na michuano ya Olimpiki ya walemavu kati ya tarehe 24 Agosti na tarehe 5 mwezi Septemba.
(Picha)Maelfu wapanga foleni kumuaga mhubiri TB Joshua

Waombolezaji wamejitokeza kwa wingi kuona mwili wa mhubiri mwenye ushawishi mkubwa wa Nigeria TB Joshua, aliyekufa mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 57.
Mwili wake umekuwa katika kanisa Synagogue, Church of All Nations (SCOAN) huko Lagos ambapo atazikwa Ijumaa.
Ibada za mazishi zilianza na misa ya kuwasha mishumaa siku ya Jumatatu na kulikuwa misa nyingine siku ya jumanneya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho .
TB Joshua alikuwa mmoja wa wainjilisti maarufu nchini Nigeria .Makumi ya maelfu ya watu Walihudhuria misa za kila wiki huko Lagos.
Umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 uliwiana na mlipuko wa vipindi vya "miujiza" vilivyopeperuhwa kwenye runinga ya kitaifa na wachungaji mbali mbali
Kanisa lake lilidai kuponya kila aina ya magonjwa pamoja na VVU / Ukimwi na kuvutia watu kutoka kote ulimwenguni.

Siku ya jumanne Viongozi na watu mbali mbali maarufu walikuwa katika makao makuu ya kanisa la TB Joshua ili kutoa heshima na rambi rambi zao .
Mke wake Evelyne na watoto wake watatu Sarah, Promise and Heart walipata fursa ya kumzungumzia maisha ya TB Joshua.
Kulingana na mke wake Evelyn Joshua, alishuhudiaTB Joshua akikua ‘’kutoka kuwa na kusanyiko la waumini 8 wa kanisa hadi kuwa na kanisa lililojaa umati wa watu na kuwa na wafuasi kote duniani "
‘’Alinifunza kuwa mwanamke niliye leo. Kwa dhahabu kuwa dhahabu lazima ipitie moto. Ninataka tu kukushukuru kwa kuwa baba mwema wa watoto wetu.", alisema mjane Everlyne.


Watoto wake TB Joshua , Sarah, Promise na Heart walimsifu baba yao mpendwa kwa kuwa mtu aliyejitolea kumtumikia Mungu " kwa heshima bila uwoga."
"Aina ya upendo uliotuonesha hatukuwahi kuuona maishani mwetu. Kama kuna mtu yeyote aliyeishi maisha ya kushangaza ni wewe. Baba yangu alikuwa na utu ambao kwa namna ambayo sikuwahi kuelewa kamwe ," alisema binti yake Sarah.
Mchakato wa mazishi ya kumuaga na kumkumbuka TB Joshua ulianza Jumatatu .
Sergio Ramos ajiunga na PSG

Chanzo cha picha, Ramos
Mchezaji wa kimataifa wa soka wa zamani wa Uhispania na nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos amejiunga na timu ya Ufaransa PSG kwa mkataba wa miaka miwili.
"PSG ni mahali ambapo mtu anaweza kuendelea kuendeleza matamanio yake, timu itaendelea kushinda, nitaendelea kushinda katika PSG ," aliandika kwenye Twitter.
Real Madrid ilitangaza Jumanne tarehe 15 Juni kwamba nahodha Sergio Ramos ataondoka kwenye klabu pale mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa mwezi Juni.
Ramos, 35, ameshinda mataji kadhaa katika Real ikiwa ni pamoja na mataji matano ya La Liga titles na manne ya Championi Ligi, tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Sevilla mwaka 2005.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ramos nchi mchezaji wa tatu kusaini mkataba na PSG katika msimu huu baada ya Wamorocco Morocco Achraf Hakimi na Georginio Wijnaldum.
Pia amekaribishwa na klabu ya PSG ambao wametuma ujumbe kwenye mtandao wao rasmi wa Twitter ulioandikwa "Karibu Ramos ".
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Zuma anaweza kuachiliwa huru kwa msamaha katika kipindi cha miezi 4

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 jela wiki iliyopita Waziri wa sheria wa Afrika Kusini anasema rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob atastahili kupewa msamaha baada ya miezi ipatayo minne.
Ronald Lamola amesema huu ulikuwa ni muda kujizuia, sio sherehe, na akaahidi kuwa Bw Zuma atachukuliwa kama mfungwa mwingine yeyote yule.
Atatumikia wiki mbili za kifungo chake cha miezi 15katika eneo lililotengwa kulingana na sheria za Covid.
Rais huyo wa zamani alijipeleka mwenyewe polisi Jumatano usiku kuanza kifungo chake kwa kutotekeleza agizo la mahakama.
Alihukumiwa wiki iliyopita baada ya kushindwa kufika mbele ya uchunguzi kuhusiana shutuma za ufisadi.
Bw Zuma alikana kuwa kulikuwa na ufisadi mkubwa na kwamba hakuonesha ushirikiano katka mchakato wa kisheria dhidi yake.
Mshukiwa sugu aliyekiri kuua aachiliwa na mahakama nchini Kenya
Mahakama nchini Kenya imemuachilia huru mshukiwa wa mauaji Philip Onyancha kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha.
Onyancha alikuwa anakabiliwa na kesi juu ya mauaji ya wanawake wawili Catherine Chelangat na Jackline Chepngetich mwaka 2008.
Katika uamuzi wake, Jaji Jessie Lesiit amesema waendesha mashitaka katika kesi hiyo hawakutoa ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani mshukiwa.
Jaji alisema uchunguzi juu ya kesi hiyo ulitaka na ulikuwa "mapungufu ya kuvunja moyo "
Bw Onyancha, ambaye alikana makosa mashitaka mwaka 2014 mahakamani alidai kuwa hakutekeleza uhalifu.
Mshukiwa alikana mashitaka baada ya kufanyiwa vipimo vya kiakilina ripoti kuonyesha kwamba ana uwezo wa kukiri au kukana mashitaka , kufuatilia kesi, na kumpa maagizo wakili wake.
Awali Onyancha, ambaye aliwaambia polisi na vyombo vya habari kwamba alihusika na mauaji, pia alikana kumuua Catherine Chelagat tarehe 22 Novemba 2008.
.Taarifa ya hukumu juu ya kuachiliwa kwa Onyancha ilishirikishwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Kenya.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Pamoja na washitakiwa wenzake Tobias Nyabuhanga Aradi na Douglas Obiero Makori, alikana kumuua mvulana mwenye umri wa miaka 14 Anthony Njirwa Muiruri Aprili 14, 2014 katika kijiji cha Ngando Dagoretti, Nairobi.
Jovenel Moïse: Polisi wawauwa watu wanne baada ya mauaji ya rais wa Haiti

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Jovenel Moïse aliuawa wakati washambuliaji walipovamia nyumba yake katika mji mkuu Port-au-Prince Watu wanne wanaoshukiwa kumuua rais wa Haiti Jovenel Moïse wameuawa katika ufyatuaji risasi uliofanywa na vikosivya usalama, polisi imesema.
Wengine wawili wamekamatwa, huku washukiwa wengine waliosalia wakiaminiwa kuwa wamejificha katika mji mkuu -Port-au-Prince.
"Watauawa au kukamatwa," mkuu wa polisi Leon Charles amesema.
Bw Moïse, aliyekuwa na umri wa miaka 53, aliuawa kwa kupigwa risasi na mke wake alijeruhiwa wakati washambuliaji walipoivamia nyumba yao mapema Jumatano.
Rais aliripotiwa kupigwa risasi nyingi na ofisi yake na chumba chake cha kulala viliporwa na kuharibiwa. Mke wa rais huyoMartine Moïse amesafirishwa kwa ndege hadiFlorida ambako anasemekana kuwa yuko katika hali mahututi lakini thabiti na anapokea matibabu.
"Mamluki wanne waliuawa na wawili wako chini ya udhibiti wetu," Bw Charles alisema katika taarifa aliyoitoa kwenye televisheni siku ya Jumatano. "Polisi wawili waliokuwa wametekwa wamepatikana ."
"Tumewazuia washukiwa njiani walipokuwa wakiondoka kutoka kwenye eneo la uhalifu," aliongeza. "Tangu wakati huo tumekuwa tukikabiliana ."

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Kuna ongezeko la uwepo wa polisi karibu na makazi ambapo polisi waliuawa Aizungumza baada ya mauaji, Waziri mkuu Claude Joseph alitoa wito wa kuwepo kwa utulivu na alitangaza hali ya tahadhari kote nchini.
Hali ya tahadhari, inaruhusu kuzuiwa kwa mikusanyiko na matumizi ya jeshikwa polisi, na utekelezaji zaidi ya mamlaka.
Rais wa Marekani Joe Biden alitoa rambirambi kwa wtau wa Haiti kwa "mauaji ya kutisha ". Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alikitaja kamakitendo "kinachoudhi " na pia akatoa wito wa utulivu.
Euro 2020: Shamrashamra zatawala England ikivunja mwiko wa miaka 55

Chanzo cha picha, Getty Images
Kumekuwa na shamrashamra kubwa katika maeneo mbalimbali ya England kufuatia timu ya taifa hilo kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Euro 2020.
England iliwachabanga Denmark 2-1 na kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza na fainali yake ya kwanza ya michuano mikubwa katika miaka 55 iliyopita.
Mara ya mwisho taifa hilo kufuzu fainali katika soka la wanaume ilikuwa mwaka 1966 ilipotwaa kombe la dunia.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson alianza kuongoza sherehe hizo toka jana akiwa na mkewe Carrie, huku video kadhaa zinazosambaa mtandaoni zikionyesha mashabiki wa timu hiyo wakiimba na kutamba kwamba kombe la Euro mwaka huu linaenda ‘nyumbani’ kwa maana ya England.
Huko Newcastle, polisi walilazimika kuwatawanya baadhi ya mashabiki waliokuwa wanakesha usiku kucha kushangilia ushindi huo katika maeneo yaliyo karibu na Central Station. Sifa kubwa ya England ni kuwa na washabiki wengi wanaopenda sana soka na wanafuatilia vilabu vyao na kuunga mkono timu yao ya taifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika majiji ya London, Liverpool, Manchester na Stoke pia shangwe zilikuwa kubwa, mashabiki wakionekana kuvua mashati na wengine wakinywa pombe kama ishara ya furaha yao ya ushindi.
Wengi wamepongeza hatua iliyofikia timu hiyo akiwemo nahodha wa zamani wa England, Wayne Rooney aliyechapisha picha katika mtandao wake wa twitter, akiwa na familia yake kufurahia matokeo ya usiku wa jana.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Goli la Mikkel Damsgaard katika kipidi cha kwanza kidogo litibue sherehe za England lakini shukrani kwa bao la dakika za nyongeza la nahodha Harry Kane likaipeleka England fainali
Baada ya ushindi wa jana gwiji wa zamani wa Arsenal na England Ian Wright, aliandika katika mtandao wake wa twitter ‘See you Sunday’, akimaanisha tukutane Jumapili.
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Rio Ferdinand, nyota wa zamani wa England na klabu ya Manchester United na yeye aliweka video fupi akionekana kuimba na mamia ya mashabiki wa England.
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Kufuatia ushindi huo dhidi ya Denmark, England sasa itakutana na Italia katika mchezo wa fainali utakaopigwa Jumapili hii katika uwanja wa Wembley. Italia ilitinga fainali baada ya kuibwaga Hispania kwa mikwaju ya penati.
Museveni: Waafrika wanaweza kuunganishwa zaidi na Kiswahili

Chanzo cha picha, @KAGUTAMUSEVENI
Rais wa Uganda Yoweri Museveni Uganda amewataka Waafrika kutumia lugha ya kiswahili ili kuwa na umoja barani humo.
Akizungumza katika siku ya Muungano wa Afrika ya upatanishi inayolenga kutathimini mafanikio ya muungano wa Waafrika, Bw Museveni amesema kiswahili ni ‘’lugha ambayo haiegamii upande wowote kiasi kwamba inaweza kutuunganisha, sio lugha ya kabila yoyote ile, na sio lugha ya mtu binafsi".
Katika hotuba hiyo, amesema anasikitushwa na kukosekana kwa mshikamano wa Waafrika.
Kupitia ujumbe wake wa mtandao wa Twitter, rais huyo wa Uganda aliandika : "Waafrika tayari wana mambo mengi ya kufanana au kuhusiana, hakuna sababu ya sisi kutoungana. Ni rahisi kwa Waafrika kuungana kuliko Watu wa Ulaya, lakini la kushangaza hatuchukui mwelekeo huo’’.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Bw Museveni aliendelea kusema kuwa: ‘’wakati wazungu wa Ulaya wanapoamua kukutana, wanaanza kujiuliza tunafaa kuongea lugha gani? Kiitalia?Kiingereza?, Kiholanzi?, kijerumani? Lakini katika Afrika tunaweza kutumia lugha ya kiswahili isiyoegemea upande wowote kutuunganisha , si ya kabila lolote, sio ya mtu yeyote’’.
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Lugha ya kiswahili ni lugha inayotumiwa katika nchi mbali mbali za Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.
Lugha ya Kiswahili ni lugha inayoendelea kukua na kuenea.
Kauli ya 'Chokochoko' ya Rais Samia yaibua mjadala Tanzania
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yusuph Mazimu
- Nafasi, BBC Swahili

Chanzo cha picha, Twitter
Kauli ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuwataka wananchi kulinda amani na utulivu wa nchi imezua mjadala mkubwa nchini humo.
Akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Morogoro, Rais Samia alisema kuna chokochoko zimeanza kujitokeza na kuwataka wananchi kuzipuuza na kutozipokea.
“Vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, fedha za matibabu wanatoa wapi, nawaomba sana wasiwaingize kwenye huo mkenge kwa sababu pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na watoto, na mama watoto na msijue chakula mtatoa wapi na wala usijue mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani,” alisema Samia bila kueleza kwa undani hizo chokochoko ni zipi.
Ingawa hajaeleza bayana kuhusu chokochoko hizo, baadhi ya wanaharakati na wafuasi wa vyama vya upinzani wanahusisha kauli hiyo na vuguvugu la kudai katiba mpya linaloendelea sasa kupitia mitandao na mikutano ya ndani ya kisiasa hasa ya vyama vya upinzani kikiongozwa na CHADEMA.
‘Kama chokochoko ni kudai Katiba mpya, basi tunataka chokochoko’ aliandika Harry Mwala kwenye mtandao wake wa Twitter
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mwanaharakati Maria Sarungi aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter ‘Kila kukicha tunapewa majina mapya, sisi tunachotaka ni katiba mpya itakayotupa haki kwa wote na kuondoa tabaka linalodhani limejimilikisha nchi’.
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kauli iliyoungwa mkono na Aikande C. Kwayu aliyesema amani inatumika kama kisingizio cha kukwepa kusikiliza maoni ya watu.
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Lakini kauli hiyo ya Rais Samia, imeungwa mkono pia na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa Chama chake tawala cha CCM, wakisema amani na utulivu wa nchi ni jambo la msigi zaidi kuliko matakwa mengine kwa sasa ikiwemo katiba. ‘Tunamuunga mkono Rais wetu wananchi tunataka maendeleo hatuna muda wa kupoteza’ aliandika Vuru Jr.
Ruka X ujumbe, 4Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Huku Malewa_Tz akiwakosoa aliowataja wanaoleta chokochoko kwamba hawawezi kujenga hata hoja.
Ruka X ujumbe, 5Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 5
Licha ya Rais Samia kueleza mbele ya wanahabari msimamo wake kuhusu katiba mpya, akitaka kupewa muda wakati huu akiifungua na kujenga uchumi wa nchi hiyo, kwa majuma kadhaa sasa kumekuwa na wito wa kuhuishwa kwa mchakato wa katiba mpya uliosimama tangu mwaka 2014, huku vyama vingine vya siasa vikieleza kutoshiriki katika chaguzi zozote mpaka kupatikane kwa Katiba hiyo. Kwa sasa nchi hiyo inatumia katiba ya mwaka 1977.
Kiongozi wa wanamgambo DRC akamatwa

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Kuna makundi kadhaa ya wanamgambo yanayoendesha harakati zake katika jimbo la Kivu Kaskazini Polisi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo wamemkamata kiongozi wa wanamgambo wa Mai Mai, Kambale Kabamba.
Alikamatwa katika eneo la Kyona, katika wilaya ya Pakanza katika mji wa Oicha (Beni territory), Kivu Kaskazini.
Polisi wamekuwa wakimsaka juu ya kuhusika kwa mashambulio katika eneo hilo.
Atafikishwa katika mahakama ya kijeshi kuwajibishwa kwa vitendo vyake.
Kuna makundi kadhaa ya wanamgambo katika jimbo la DRC la Kivu Kaskazini.
Botswana yachimba 'moja ya mawe ya almasi kubwa duniani'

Chanzo cha picha, Dr. Mokgweetsi E.K Masisi/Twitter
Maelezo ya picha, Jiwe hili la Almasi limeripotiwa kuwa ni la tatu kwa ukubwa duniani Botswana imefichua jiwekubwa na jeupe la almasi lenye ukubwa wa karati 1,174, liliwa ndio jiwe la pili kwa ukubwa kuchimbuliwa nchini humo mwezi huu.
Almasi hiyo iligunduliwa tarehe 12 Juni na kampuni ya machimbo ya madini ya Canada- Lucara na kuwasilishwa kwenye hifadhi ya taifa ya madini iliyopo katika mji mkuu Gaborone Jumatano.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Naseem Lahri ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Almasi hiyo ni ya tatu kwa ukubwa duniani.
"Hii ni historia kwetu na kwa Botswana pia ," alisema.
Mwezi uliopita, jiwe lililokuwa na uzito wa karati 1,098 -lilionyeshwa kwa Rais Mokgweetsi Masisi, baada ya kampuni ya almasi ya Debswana, kuligundua tarehe 1 Juni.
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi aliushirikisha umma picha za jiwe hilo la thamani :
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo tarehe 08.07.2021
