TB Joshua:Fahamu maneno ya mwisho aliyosema katika mahubiri yake kabla ya kifo

Chanzo cha picha, oTHERS
Jumamosi ijayo ya tarehe 12 Juni mhubiri wa Nigeria Temitope Balogun almaarufu TB Joshua angeadhimiha miaka 58 ya kuzaliwa kwake .
Lakini kwa bahati mbaya aliaga dunia siku ya Jumamosi tarehe 5 Juni wiki moja tu kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa .
Kinachowashangaza wengi ni kwamba TB Joshua alikuwa amesema kuwa hatosherehekea siku yake ya kuzaliwa .
Huu ndio uliokuwa ujumbe wa mwisho wa TB Joshua :
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Katika video iliyowekwa mtandaoni baada ya kutangazwa kwa kifo chake Joshua anaonekana akijiimbia wimbo wa 'Happy birthday'
Kisha alitangaza kwamba mwaka huu hakuwa na nia ya kusherehekea siku hiyo kwasababu hakufurahia yote yaliyokuwa yakitendeka duniani .
Alisema: " Haitakuwa rahisi kwangu kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa,kwasababu watu wengi wanahangaika duniani'
" Huzuni zao na hofu zao zipo nami hivyo basi siku hiyo itakuwa ya sala na kufunga na tusiwasahau wanaohitaji msaada wetu'.
Aliongeza kwamba 'kulikuwa na siku zake nyingi za kusherehekea kuzaliwa kwake
Jinsi watu walivyomuomboleza TB Joshua mtandaoni :

Chanzo cha picha, Twitter
Siku ya Jumamosi tarehe 5 Juni 2021, nabii TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel.
''Kila kitu kina wakati wake - tunapokuja hapa na kuomba na tutarudi nhyumbani baada ya utumwa''.
TB Joshua alikuwa mmoja ya wahubiri maarufu ambapo alijulikana kwa kutabiri matukio yajayo ambayo wengi waliona kama uingiliaji kazi ya Mungu.

Chanzo cha picha, TB JOSHUA MINISTRIES
Mwaka 2014, Muhubiri huyo alikosolewa nchini Nigeria baada ya upande mmoja wa paa la kanisa lake nchini humo kuanguka na kuwaua takriban watu 116.
Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.
TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.
Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo uhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.
TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Marekani ya kusini.
Utata wa TB Joshua
Baadhi ya watu wamekuwa wakimkosoa kutokana na idadi ya miujiza yake anayofanya katika mikutano yake.
Baraza la makanisa ya Pentecostal nchini Nigeria PFN , chini ya mwavuli wa makanisa ya Pentecostal nchini Nigeria hayakubaliani na kanisa la muhubiri huyo wakimtaja TB Joshua kuwa kibaraka.
Christ Okote muhubiri wa kanisa maarufu nchini Nigeria alimshutumu Joshua kwa kuwa 'mganga'
Wakosoaji wake wa Kikristo wanasema kwamba mbinu zinazotumiwa na Joshua haziendani na zile za biblia.
'Miujiza yake ilikuwa ya kweli?'
Lakini mzozo uliokuwa ukimzunguka muhubiri huyo haukuishia hapo, kwasababu wengi pia walimkosoa kuhusu miujiza yake mingi katika mikutano yake.
Mwaka 2017, Chris Okotie, muhubiri Maarufu nchini Nigeria , alimshutumu Joshua kwa kufanya 'uganga'.
Lakini waziri wa zamani wa usafari wa ndege , Femi Fan Kayode ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa TB Joshua alimtaka Okotie kuwacha kumshambulia Joshua na badala yake kuitisha umoja katika kanisa hilo.
Wakosoaji wake wa Kikristo wamekuwa wakisema kwamba mbinu anazotumia TB Joshua haziendani na zile zilizopo katika bíblia.
Baraza la Kanisa la Pentecostal nchini Nigeria halikukubali kanisa la Joshua kuwa chini yake.
Paa la nyumba kuanguka
Mwaka 2014, paa la nyumba moja ya wageni iliopo ndani ya kanisa la SCOAN la muhubiri huyo katika eneo la Ikotun -Egbe mjini Lagos lilianguka .
Idadi ya watu waliofariki kutokana na kuanguka kwa jumba hilo ilifikia 115, ikiwemo raia 84 wa Afrika Kusini kulingana na waziri mmoja wa taifa hilo, Jeff Radebe.
TB Joshua alilaumiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwa jumba hilo.
Alidai kwamba baadhi ya watu walitaka kumuua kupitia tukio hilo.
Wakati huo, rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitembelea kanisa hilo na kuamua kuanzisha uchunguzi kuhusu kile kilichotokea.
Msimamo kuhusu wapenzi wa jinsia moja
YouTube ilisimamisha akaunti ya TB Joshua juu ya madai ya matamshi ya chuki.
Shirika moja la kutetea haki liliwasilisha lalamikoa baada ya kukagua video zisizopungua saba zikimuonesha mhubiri huyo akifanya maombi ya "kuwaponya" watu wa mapenzi ya jinsia moja
Facebook pia iliwahi kuondoa ondoa moja ya machapisho ambayo yanaonesha mwanamke akipigwa kofi wakati TB Joshua akimuombea na kusema anatoa "roho ya pepo".
Akaunti yake ya YouTube ilikuwa na wafuasi milioni 1.8.
TB Joshua ni mmoja wa wainjilisti wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, na wanasiasa wakuu kutoka bara zima ni miongoni mwa wafuasi wake.
Kwanini akaunti yake ilifungwa ?
Shirika la Open Democracy lenye makao yake nchini Uingereza liliwasilisha malalamiko baada ya kukagua video saba zilizochapishwa kwenye idhaa ya YouTube ya TB Joshua Ministries kati ya 2016 na 2020, ambayo inaonysha kuwa mhubiri huyo anafanya maombi "kuponya" watu wa mapenzi ya jinsia moja.
Msemaji wa YouTube aliambia OpenDemocracy kwamba akaunti hiyo ilifungwa kwa sababu sera yake "inakataza maudhui ambayo yanadai kwamba mtu ni mgonjwa wa kiakili, anaugua, au ni duni kwa sababu ya ushirika wao katika kikundi kinacholindwa pamoja na mwelekeo wa kijinsia".
Ujumbe kwenye akaunti ya Facebook ya TB Joshua Ministries uilisema: "Tumekuwa na uhusiano mrefu na wenye mafanikio na YouTube na tunaamini uamuzi huu umefanywa kwa haraka."














