Uchaguzi Tanzania 2020: Kura zaanza kuhesabiwa Tanzania

Raia wa Tanzania hii leo wanashiriki katika shughuli ya uchaguzi mkuu ambapo wanatarajiwa kumchagua rais, wabunge na madiwani

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu, Esther Namuhisa and Asha Juma

  1. Uchaguzi Tanzania 2020:Watanzania wanasema nini kuhusu kuminywa kwa mitandao ya kijamii?

    Maelezo ya video, Uchaguzi Tanzania 2020:Watanzania wanasema nini kuhusu kuminywa kwa mitandao ya kijamii?
  2. Matokeo ya Uchaguzi 2020: Matokeo yameanza kuhesabiwa

    uchaguzi
    uchaguzi
    Maelezo ya picha, Matokeo yameanza kuhesabiwa
    Wananchi wameonekana kusogea karibu ya vituo baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika
    Maelezo ya picha, Wananchi wameonekana kusogea karibu ya vituo baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika
    wanachi
  3. NEC yakanusha uwepo wa kura feki

    kura
  4. Uchaguzi Tanzania 2020:Video ya 'Ushaidi wa kura feki'

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  5. Matokeo Uchaguzi Tanzania 2020:NEC itaanza kupokea matokeo ya uchaguzi kuanzia usiku

    tANZANIA
  6. Uchaguzi Tanzania 2020:Tundu Lissu akipiga kura Singida

    Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu awali akipiga kura ya Uchaguzi Mkuu leo Oktoba 28, 2020, majira ya mchana, katika Kituo cha Ntewa Ikungi, Mkoani Singida.

    Kwa sasa mchakato wa kupiga kura umefikia tamati, na wasimamizi wa vituo pamoja na mawakala wataanza kuhesabu kura hizo.

    Lissu

    Chanzo cha picha, CHADEMA

    Bwana Lissu anapambana vikali na rais wa Tanzania John Magufuli kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

    Lissu

    Chanzo cha picha, CHADEMA

  7. Uchaguzi Tanzania 2020: NEC yakanusha uwepo wa kura feki

    kura

    Tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania, NEC imekanusha shutuma za uwepo wa kura feki.

    Kwa mujibu wa tume, Jaji Semistocles Kaijage amesema taarifa hizo si rasmi na ni za kupuuza.

    Awali kupitiwa mitandao ya kijamii iliripotiwa kukamatwa kwa karatasi za kura ambazo tayari zilikuwa zimeshapigwa katika maeneo ya Kigoma ,Tanga na Kawe.

    Mapema leo aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kawe, bi. Halima Mdee alikamatwa na polisi baada ya kulalamikia uwepo wa masanduku yenye kura feki ambapo baadae aliachiwa.

    Pamoja na hilo, mwenyekikiti wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kupitia mtandao wa Twitter aliandika kuhusu kukamatwa kwa kura ambazo zimeshapigwa katika jimbo lake la uchaguzi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  8. Uchaguzi Tanzania 2020: Matukio katika picha

    tANZANIA

    Zaidi ya watu milioni 29 wamejiandikisha kupiga kura nchini Tanzania.

    Raia wa Tanzania wamechagua rais, wabunge na madiwani na huku matokeo yakitarajiwa kutoka ndani ya wiki moja.

    PICHA
    PICHA

    Watu wakiwa wamepanga foleni kwa ajili ya kupiga kura mapema leo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

    wAPIGA KURA

    Wagombea wa urais walikuwa 15 na wawili kati ya hao ni wanawake.

    KURA
  9. Uchaguzi Tanzania 2020: Tume imethibitisha kuwa kila mwananchi anajua haki yake

    Maelezo ya video, Uchaguzi Tanzania 2020:'Kila Mtanzania anapata haki yake ya kupiga kura'
  10. Uchaguzi Tanzania 2020: Netblocks yathibitisha kuminywa kwa mtandao

    Shirika la Netblocks linalofuatilia usalama na usimamizi wa mtandao limeripoti kuminywa kwa intaneti huku upigaji kura ukiendelea nchini Tanzania.

    Shirika la Netblocks limethibitisha “kuminywa kwa mtandao” kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania, hatua ilioathiri zaidi “mtandao wa Twitter, WhatsApp, Instagram na huduma za Google” ambayo ni majukwaa makubwa ya mawasiliano.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Hata hivyo mtandao wa Facebook umetoa hakikisho kwamba utaendelea kutoa taarifa kwa wapiga kura na kuimarisha juhudi zao katika kukabiliana na taarifa za uongo na muingilio wowote kwenye uchaguzi huo.

    Pia mtandao huo ulisema kuwa watumiaji wataweza kuelimishana na wengine kuhusu taarifa zao za upigaji kura.

    Mamlaka imeonya dhidi ya kusambaza taarifa za uongo na kuongeza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wanaokiuka kanuni za mawasiliano.

    Kuanzia jana hadi leo, watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania wamelalamikia kuminywa kwa mitandao ya Twitter,Instagram na WhatsApp.

  11. Uchaguzi Tanzania 2020: Balozi wa Marekani awatakia kheri Watazania

    Balozi wa Marekani nchini Tanzania , Donald Wright amewatakia kheri watanzania katika zoezi zima la upigaji kura.

    "Kuwapatia uhuru waangalizi na mawakala wa vyama pamoja na mchakato wa kuhesabu kura ulio wazi kutafanya uchaguzi huu kuaminika."

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  12. Uchaguzi Tanzania 2020: Wasiojua kusoma na kuandika wanavyoshiriki kupiga kura

    Zoezi la uchaguzi linaendelea kote nchini Tanzania na raia ambao wametimiza umri wa kupiga kura leo wanatekeleza haki yao.

    Lakini je ikiwa mpiga kura hajui kusoma wala kuandika itakuwaje?

    Tazama mama huyu ambaye ni miongoni mwa kundi hilo.

    Maelezo ya video, Mama asiyejua kusoma wala kuandika apiga kura
  13. Uchaguzi Tanzania 2020: Seif Sharif Hamad ametekeleza haki yake ya kupiga kura

    Seif Sharif Hamad
    Maelezo ya picha, Seif Sharif Hamad

    Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Seif Sharif Hamad amepiga kura yake.

    Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo aliachiwa huru jana baada ya kukamatwa visiwani Zanzibar.

    Maalim Seif anakabiliana na Hussein Mwinyi katika kugombea urais Zanzibar.

  14. Uchaguzi Tanzania 2020: Kijana anayepiga kura kwa mara ya kwanza

    Miongoni mwa wanaoshiriki uchaguzi unaoendelea nchini Tanzania ni kijana Hashim Bakari anayepiga kura kwa mara ya kwanza. Hisia zake zilikuwa zipi wakati anatekeleza haki yake?

    Maelezo ya video, Kijana anayepiga kura kwa mara ya kwanza
  15. Uchaguzi Tanzania 2020: Matukio yanayoendelea katika uchaguzi wa Tanzania

    Raia wa Tanzania leo wanaendelea kuchagua viongozi wao katika ngazi mbalimbali ikiwemo urais.

    Tazama picha zinavyoonesha hali ilivyo katika baadhi ya maeneo.

    Maelezo ya video, Uchaguzi wa unaendelea nchini Tanzania
  16. Uchaguzi Tanzania 2020: Rais Magufuli akipiga kura huko Dodoma

    Magufuli

    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amepiga kura yake katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma.

    Rais Magufuli anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Tundu Lissu, mwanasiasa wa chama cha upinzani cha Chadema.

    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akipiga kura yake

    Chanzo cha picha, CHAMA CHA MAPINDUZI

    Maelezo ya picha, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akipiga kura yake
  17. Uchaguzi Tanzania 2020: Hussein Mwinyi apiga kura yake Zanzibar

    Viongozi mbalimbali wameanza kupiga kura katika uchaguzi unaoendelea Tanzania miongoni mwao akiwa Hussein Mwinyi anayegombea urais Zanzibar kupitia chama cha CCM.

    Hussein Mwinyi anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwaSeif Sharif Hamad wa chama cha ACT Wazalendo.

    Hapo jana Maalim Seif alikamatwa na maafisa wa polisi katika kituo cha kupigia kura cha Garagara hatua ambayo imeshutumiwa vikali na viongozi wa upinzani.

    Hata hivyo aliachiwa huru saa za jioni.

    Maelezo ya video, Hussein Mwinyi apiga kura yake
  18. Uchaguzi Tanzania 2020: Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo ya kupigia kura

    Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo ya kupigia kura
    Maelezo ya picha, Hali ilivyo katika baadhi ya maeneo ya kupigia kura

    Raia nchini Tanzania wameanza kupiga kura kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

    Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa moja majira ya asubuhi tayari kwa zoezi hilo.

    Mwanahabari wa BBC Eagan Salla alitembelea ofisi ya mtendaji wa mtaa wa Kunduchi Mtongani eneo ambalo makarani na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura walikuwa wanachukua vifaa, vituturi, karatasi za kupigia kura pamoja na masanduku ya kuwekea kura baada ya kura kupigwa.

    Hali imekuwa ni harakati za makarani wakiingia na kutoka eneo hilo kuelekea maeneo yao husika wanayosimamia zoezi la uchaguzi.

    Pia katika vituo vya kupigia kura muda wa mapema wakati mwanahabari Eagan Sallah anatembelea watu walikuwa sio wachache wala wengi sana wanaowasili kila mmoja kwa wakati wake wakiendelea kuhakikisha taarifa zao kwenye makaratasi ambayo yamebandikwa kwenye kuta.

  19. Uchaguzi Tanzania 2020: Takwimu za waliojiandikisha kwa daftari la wapiga kura Tanzania

    Wapiga kura wamekuwa wakikagua maelezo kuwahusu kwenye sajili ya wapiga kura vituo vya kupigia kura
    Maelezo ya picha, Wapiga kura wamekuwa wakikagua maelezo kuwahusu kwenye sajili ya wapiga kura vituo vya kupigia kura

    Leo ni siku ambayo Tanzania inapiga kura katika katika uchaguzi Mkuu Mwaka huu wa 2020.

    Zaidi ya wapiga kura milioni 29 waliojiandikisha wanatarajiwa kupiga kura yao leo Jumatano Oktoba 28 katika uchaguzi huo mkuu.

    Tofauti na miaka iliyopita ya uchaguzi nchini Tanzania mwaka huu wagombea wa nafasi za urais wamejitokeza kwa wingi.

    Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania, wagombea 15 wa urais ikiwa ni pamoja na rais John Pombe Magufuli ndio wanaogombea nafasi hiyo.

    Aidha wengine wanaochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Wabunge, Wawakilishi na Madiwani watakaoongoza kwa miaka mitano.

    Siku ya uchaguzi inawadia baada ya kumalizika kwa siku 63 za kampeni.

    Kulingana Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage, wapiga kura milioni 29.188 wamejiandikisha katika Daftari la Kudumu la NEC na 566,352, wamejiandikisha katika Daftari la Kudumu la Tume ya Uchaguzi Zanzubar (ZEC).

  20. Uchaguzi Tanzania 2020: Baada ya kupiga kura, je unajua iwapo kura yako itahesabiwa?

    Maelezo ya video, Baada ya kupiga kura tarehe 28,Je unajua iwapo kura yako itabainika imeharibika?