Mazungumzo kati ya Iran na Oman; Ripoti kuhusu kuikabidhi Iran njia ya kuingia mlango bahari wa Hormuz kutolewa
Katika matamshi ambayo yanaonekana kumlenga Donald Trump, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema kwamba taarifa ya pamoja kuhusu makubaliano hayo inakamilishwa isipokuwa iwapo baadhi ya wahusika wengine wataingilia kati.
Kulingana na ripoti, makubaliano yaliyopendekezwa yataipa Tehran udhibiti wa meli zinazoingia Ghuba ya Uajemi kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao baadhi ya wataalamu wanasema utakuwa mojawapo ya makubaliano makubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa Iran.
Kuongezeka kwa matumaini kuhusu makubaliano hayo na uwezekano wa kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz kumesababisha bei za hisa kupanda katika masoko ya Marekani na Asia.
Wakati huo huo, Shirika la Propaganda za Kiislamu nchini Iran limetangaza kwamba mikutano ya mitaani nchini Iran itaendelea hadi mwisho wa Safar, na, matokeo yake yatatangazwa baada ya kuidhinishwa na kiongozi mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei.