Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah

Taarifa kutoka wizara ya afya ya Lebanon zinasema kuwa watu 182 wameuawa na wengine 727 kujeruhiwa, wakiwemo watoto, wanawake na wahudumu wa afya katika mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon yaliyoanza asubuhi ya leo.

Muhtasari

  • Katika picha: Maelfu wakimbia huku Israel ikizidisha mashambulizi Lebanon
  • Tazama: Moshi ukifuka kusini mwa Lebanon baada ya mashambulizi ya Israel
  • Israel inakabiliwa na siku ngumu zijazo, asema Netanyahu
  • Watoto 21 wuawa Lebanon katika mashambulio ya Israel huku idadi ya vifo ikifikia 274
  • Lebanon yasema watu 274 wameuawa katika siku mbaya zaidi ya mzozo baina ya Israel na Hezbollah
  • Viongozi wa Chadema miongoni mwa watu 14 wanaotuhumiwa na polisi Tanzania kwa maandamano yaliyopigwa marufuku
  • Mke wa kiongozi wa upinzani Tanzania Freeman Mbowe na bintie waachiliwa huru
  • Seneta wa Kenya awasilisha hoja ya kupinga tabia ya Naibu wa Rais
  • Tazama: Hali ilivyokuwa katika mji wa Dar es Salaam katika siku ambapo upinzani ulikuwa umepanga maandamano
  • Tazama: Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alivyokamatwa
  • Lebanon yawaonya wakazi wa Kusini kwa ujumbe wa simu kuepuka maeneo ya Hezbollah yanayolengwa
  • Polisi yathibitisha kuwakamata viongozi wa Chadema na wengineo
  • IDF kutekeleza mashambulizi 'makubwa na kwa usahihi' zaidi nchini Lebanon
  • Kwa Picha: Hali ilivyo katika mji wa Dar es Salaam
  • Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akamatwa
  • Polisi watanda Dar es Salaam kuelekea maandamano ya Chadema
  • Sri Lanka yamuapisha rais mpya anayeegemea mrengo wa kushoto
  • Watu sita wafariki dunia baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko Japan
  • Zelensky kuwasilisha 'mpango wa ushindi' kwa Biden, Harris na Trump
  • Kocha wa Arsenal asema sare na Man City ni 'muujiza'
  • Italia: Watu wanne wa familia moja wafariki dunia katika mlipuko wa gesi
  • Trump asema hatagombea tena ikiwa atashindwa katika uchaguzi wa Novemba

Moja kwa moja

Na Asha Juma & Dinah Gahamanyi

  1. Kocha wa Arsenal asema sare na Man City ni 'muujiza'

    Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ni "muujiza" timu yake kukaribia ushindi baada ya kucheza kipindi cha pili na wachezaji 10 katika mechi ya Ligi Kuu England.

    "Ni muujiza tulicheza dakika 56 pale Etihad tukiwa na wachezaji 10," alisema Arteta. "Siamini tulichokifanya."

    Bao la kusawazisha la John Stones wa Manchester City katika dakika ya 98 liliinyima Arsenal ushindi muhimu dhidi ya mabingwa hao watetezi.

    Baada ya winga wao Leandro Trossard kutolewa kwa kadi nyekundu katika muda wa majeruhi wa kipindi cha kwanza, The Gunners walimiliki mpira kwa asilimia 12.5 pekee katika kipindi cha pili.

    Arsenal walikuwa wamebakia na sekunde chache kabla ya kuwa timu ya kwanza ya ugenini kushinda katika uwanja wa Etihad tangu Brentford mwezi Novemba 2022.

    Soma zaidi:

  2. Italia: Watu wanne wa familia moja wafariki dunia katika mlipuko wa gesi

    Watu wanne wa familia moja wakiwemo watoto wawili wamefariki katika mlipuko wa gesi kusini mwa Italia.

    Nyumba yao ya ghorofa mbili katika mji wa Saviano, karibu na Naples, iliporomoka kwa kiasi fulani katika mlipuko huo, na kuwaua ndugu - mvulana na msichana - pamoja na mama na bibi yao.

    Baba na mtoto mchanga walipatikana kutoka kwenye vifusi wakiwa hai, wazima moto wa Italia walisema.

    Bado yuko hospitalini huko Naples akiwa katika hali mbaya, wakati majeraha ya mtoto sio ya kutishia maisha, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Idara ya zimamoto ya Vigili del Fuoco, Italia, iliripoti kwamba wazazi na watoto watatu waliishi kwenye ghorofa moja ya nyumba hiyo, wakati mwanamke mwingine - anayesemekana kuwa bibi - aliishi kwenye ghorofa ya juu.

    "Wazima moto waliwaokoa baba na mtoto mchanga wakiwa hai, na kuwakabidhi chini ya uangalizi wa wafanyikazi wa afya mahali hapo, wakati hawakuweza kufanya chochote kwa watoto wawili, mvulana na msichana, ambao kwa bahati mbaya miili yao ilitolewa wakiwa washafariki dunia," Idara ya zimamoto ilisema katika taarifa.

    Ingawa mamlaka haijathibitisha umri wa watoto hao, vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba walikuwa wa miaka minne na sita.

    Wazima moto waliwapata watoto na baba asubuhi, kisha ikawachukua siku nzima kutafuta kwenye vifusi, na hawakumpata mama huyo hadi saa 16:45.

    Vikosi vya utafutaji na uokoaji, vinavyofanya kazi na mbwa wa kunusa, viliendelea na utafutaji wa bibi huyo hadi usiku, na kutangaza kuwa wamempata na walikuwa wamemaliza shughuli hiyo kufikia saa 01:00.

    Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo hasa cha kuporomoka kwa jengo hilo, lakini nadharia za awali zinaonyesha kuwa nyumba hiyo ilianguka baada ya mlipuko wa gesi.

    Pia unaweza kutazama:

  3. Trump asema hatagombea tena ikiwa atashindwa katika uchaguzi wa Novemba

    Rais wa zamani Donald Trump amesema hatarajii kugombea tena uchaguzi mwaka 2028 iwapo atashindwa katika uchaguzi wa urais wa Marekani utakaofanyika Novemba mwaka huu.

    Trump, mwenye umri wa miaka 78, amekuwa mgombea wa chama cha Republican kwa chaguzi tatu za kitaifa mfululizo na amekijenga upya chama hicho kwa miaka minane iliyopita.

    Katika mahojiano na Sinclair Media Group, aliulizwa kama anaweza kujiona akiwania tena urais iwapo atashindwa na Makamu wa Rais wa chama cha Democratic Kamala Harris.

    "Hapana, sitawania. Nafikiri... itakuwa hivyo," Trump alisema.

    "Sioni hilo hata kidogo." Lakini aliongeza kuwa "natumai, tutakuwa na mafanikio makubwa".

    Sheria za Marekani zinawazuia marais kuhudumu kwa zaidi ya mihula miwili, na hivyo Trump hatarajiwi kugombea mwaka 2028 iwapo atashinda pia.

    Katika siku za nyuma, tajiri huyo mmiliki wa majengo ni mara chache sana amekubali uwezekano wa kushindwa katika uchaguzi, mara nyingi zaidi akiwachochea wafuasi wake kwa hotuba na jumbe za kwenye mitandao ya kijamii akiahidi ushindi katika uchaguzi.

    Lakini hii ni mara ya pili ndani ya siku nne ametaja kuwa pia anaweza kushindwa.

    Soma zaidi:

  4. Ni wakati mwingine tena nakukaribisha katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 23/09/2024