Watu 12 wahukumiwa kwa mashambulio ya mabomu

Chanzo cha picha, PTI
Iliyochapishwa
Mahakama moja nchini India, imewakuta wanaume kumi na mbili na hatia kwa kuhusika katika mashambulizi ya mabomu kwenye treni mjini Mumbai mwaka 2006.
Mtu mmoja hata hivyo aliondolewa mashtaka hayo na kuachiliwa huru.

Chanzo cha picha, AP
Zaidi ya watu mia moja themanini waliuwawa na mamia ya wengine kujeruhiwa wakati mabomu saba yalipolipuka kwenye treni za abiria.
India iliwashutumu wanamgambo wa Kiislamu, kutoka kundi la la Lashkar-e-taiba, lenye makaazi yake nchini Pakistan, kwa kutekeleza mashambulizi hayo madai ambayo Pakistan iliyakanusha.

Chanzo cha picha, AP








