Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Kenya 2022 : Kwa nini wakulima wanapenda matamanio makubwa ya William Ruto
Mkulima mkubwa - hivyo ndivyo watu wanaozunguka nje ya kituo kidogo cha maduka katika mji wa Kosachei magharibi mwa Kenya wanavyomuelezea Naibu Rais William Ruto, ambaye anawania kiti cha urais katika uchaguzi wa Agosti 9.
Bw Ruto ni mmoja wa wakulima wakubwa wa mahindi nchini Kenya. Shamba lake kubwa, ambalo liko karibu na kituo cha ununuzi, ni ushahidi wa utajiri wake.
Wanawake hununua mboga, ndizi na mayai kutoka shambani na kuviuza katika masoko katika miji ya karibu, huku wanaume wakifanya kazi kama vibarua shambani.
Imewekwa nyuma ya lango jeusi la chuma, inalindwa vikali na polisi.
Bw Ruto anamiliki mashamba makubwa kote nchini na wasiwasi umeibuka kuhusu jinsi alivyopata baadhi ya sehemu hiyo ya utajiri wake.
Mnamo Juni 2013, Mahakama Kuu ilimwamuru kusalimisha shamba la ekari 100 (hekta 40), na kufidia mkulima ambaye alikuwa amemshtaki kwa kunyakua ardhi wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Alikana shutuma dhidi yake.
Katika uchaguzi huo alikuwa ameunga mkono azma ya urais ya Raila Odinga, ambaye sasa ndiye mpinzani wake mkuu - akiakisi miungano ya kisiasa inayobadilika kila mara nchini Kenya huku viongozi wakihesabu namna bora ya kupata mamlaka.
Gazeti la Daily Nation la Kenya linasema Bw Ruto anafurahia ufuasi kama wa madhehebu miongoni mwa wafuasi wake. Lakini kura ya maoni ya hivi majuzi nchini kote - ambayo Bw Ruto amepuuzilia mbali kuwa "iliyotengenezwa" - inaonesha kuwa anamfuata Bw Odinga kwa 37% hadi 43%.
Wakazi wa Kosachei wana matumaini kuwa atashinda, na kuwasaidia wakulima kuongeza mavuno yao na kuifanya Kenya kujitosheleza kwa chakula.
"Ni jirani mwema anayetufundisha kulima. Zamani alipokuwa waziri wa kilimo alitoa ruzuku ya mbolea. Bei ya mbolea kwa sasa ni ya juu kabisa. Ni yeye pekee ndiye anayeelewa masuala ya wakulima. " anasema Mama Sasha muuza mboga.
Shamba la Bw Ruto liko katika kaunti ya Uasin Gishu, ambayo - pamoja na kaunti jirani - huzalisha mahindi mengi ya Kenya.
Ugavi wake kwa bodi ya kitaifa ya nafaka umekuwa na utata kuhusu malipo.
Mnamo 2018, kampuni iliyosajiliwa kwa majina ya mke na mwanawe Bw Ruto ilichunguzwa kuhusu usambazaji wa mahindi ya thamani ya mamilioni ya pesa za Kenya, lakini shirika la kupambana na ufisadi likaifuta.
Majirani wa Bw Ruto huko Kosachei wanamtetea wakisema alilengwa isivyofaa.
Wanakataa kumkosoa, wakimlaumu Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta - ambaye anamuunga mkono Bw Odinga baada ya kutofautiana na naibu wake mapema katika muhula wao wa pili - kwa kushindwa kwa serikali.
Kwao, Bw Ruto ndiye chanzo cha maisha yao na "ushindi kwake utakuwa ushindi kwa kila mtu".
"Ikiwa 'mama mboga' [mchuuzi wa mboga] hana mtaji wa kuanzia, huenda kutafuta mazao kutoka kwa shamba lake ili kuanzisha biashara," Mama Sasha anatuambia huku akionesha baadhi ya kabichi na mboga za asili kutoka kwa shamba la Bw Ruto.
Kibanda chake chenye kuta za udongo kiko mita mbali na shamba la Bw Ruto.
Ameahidi mikopo nafuu kwa wakulima ili kuwasaidia kumudu gharama za uzalishaji na kuwapatia soko tayari kwa mazao yao.
Mkulima wa mahindi, maziwa na kondoo, Edward Barngetuny, ambaye shamba lake la ekari 40 liko katika eneo la Salient kaunti jirani ya Nandi, anasema kuongezeka kwa gharama ya mbolea kumewafanya wakulima kupunguza ekari wanazolima.
"Suala kubwa tunalokabiliana nalo ni ukosefu wa mapato ya chini ya uhakika. Ikiwa soko litadhibitiwa basi mtu anaweza kufanya hesabu na kupanga ipasavyo," baba wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 33 anasema.
Bei ya mahindi inadhibitiwa na mahitaji na nguvu za ugavi na kuifanya isiweze kutabirika.
Kwa sasa, gunia la mahindi linauzwa kwa bei ya juu zaidi lakini baadhi ya wakulima katika eneo la nyumbani kwa Bw Ruto walikuwa tayari wametelekeza zao hilo kwa ajili ya miwa ambayo bei yake inadhibitiwa na serikali.
"Tungependa yeye [Ruto] aondoe ushuru wote wa zana za kilimo. Vifaa vimekuwa ghali sana ilhali tunataka kutengeneza mashine ili kuongeza mavuno," Bw Barngetuny asema.
Anapuuza ruzuku iliyotangazwa hivi majuzi ya unga wa mahindi - ambayo itadumu kwa mwezi ujao - kama njama ya uchaguzi, akisema haitaathiri wakulima wengi kwani mavuno yajayo sio hadi Desemba.
"Ni tu kuwashawishi Wakenya kupiga kura katika chaguzi zijazo," asema.
Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa pia ni mkubwa magharibi mwa Kenya na jamii ya Wakalenjin ambako Bw Ruto anatoka wana kitamu cha kitamaduni kiitwacho "mursik".
Ni maziwa yaliyochachushwa katika kibuyu cha kitamaduni kilichowekwa masizi ya matawi ya miti maalum kwa ajili ya kuhifadhi na ladha.
Nelly Kulei amekuwa katika biashara ya mursik kwa zaidi ya miaka 20 na anasema mwaka huu umekuwa mgumu.
"Tuliathiriwa na uhaba wa maziwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Tuna matumaini kwamba mambo yatabadilika baada ya uchaguzi huu," anasema mama huyo wa watoto watano huku akionesha jinsi mursik inavyotengenezwa.
Jamii ya Wakalenjin ndiyo iliyomtoa rais mkongwe zaidi wa Kenya, marehemu Daniel arap Moi, ambaye alitawala kwa miaka 24.
Katika mji wa Eldoret, kundi la wakazi hukutana mara kwa mara kujadili siasa katika kile kiitwacho "Bunge la Mwananchi",
Mbunge mtarajiwa Dan Langat anazungumza nao kuhusu hitaji la jamii ya Wakalenjin kumuunga mkono kikamilifu Bw Ruto, ambaye amechukua nafasi ya marehemu Bw Moi kama kinara wa jamii hiyo.
"Tuna matumaini kuwa Bw Ruto atachukua kiti cha urais na kurejesha nafasi yetu nchini," anauambia umati.
Eldoret imekua na kuwa mji wa nne kwa ukubwa nchini Kenya. Inajivunia skyscraper mpya, iliyojengwa kwenye eneo lake la vilima.
Jiji linazungumzwa na wafanyabiashara wengi wanaouza mazao ya kilimo.
Lakini pia ni nyumbani kwa makampuni makubwa ya nguo ambayo hutoa ajira kwa maelfu.
Moja wapo, Zaritex, inamilikiwa na Daniel Odhiambo, anayetoka katika jamii ya Waluo, kama Bw Odinga.
Anasema ilhali Eldoret ni mahali penye ghasia wakati wa uchaguzi, hana mpango wa kusafiri kurudi nyumbani Kisumu kwani haogopi kulengwa kwa sababu ya asili yake ya kikabila.
Anasema takriban 50% ya wafanyakazi wake ni wenyeji kutoka jamii ya Wakalenjin na wameishi pamoja vyema.
"Vyombo vya usalama hapa vimejaribu sana kuhubiri amani na tunatumai kuwa itakuwa ya amani," Bw Odhiambo asema huku akimuonesha mfanyakazi jinsi ya kupima kitambaa.
Eldoret pia ina sekta ya nguo za mitumba inayostawi katika Soko la Magharibi.
Nguo za mitumba zimejitokeza katika ilani za wagombea wote wawili wanaoongoza, kila mmoja akitaka kuunga mkono tasnia ya nguo ya ndani na kupunguza utegemezi wa nguo kutoka nje.
Bw Odinga alizua utata kwa kusema kuwa nguo za mitumba zilikuwa zikimilikiwa na watu waliofariki barani Ulaya, lakini baadaye akafafanua kuwa ataunga mkono wafanyabiashara walioziuza hata alipotaka kukuza viwanda vya nguo vya humu nchini.
Tabitha Mumbi, 40, anasema sekta hiyo inatoa riziki kwa mamilioni ya Wakenya.
"Mimi ni zao la mtumba, wazazi wangu walinisomesha hadi ngazi ya diploma na biashara hii na sasa nalipia ada ya shule kwa watoto wangu kwa fedha hizi," anasema.
Yeye na wafanyabiashara wengine hawakutaka kuzungumzia siasa za uchaguzi, lakini walikubali soko lilihitaji kudhibitiwa ili kuhakikisha kwamba ni nguo za mitumba tu za ubora zinazoingizwa nchini.
"Tumekuwa uwanja wa kutupia taka. Baadhi ya nguo tunazopokea ni za ubora duni na sasa imekuwa vigumu kupata faida yoyote," anaeleza Violet Nyambokho mwenye umri wa miaka 50, ambaye ameuza sketi kwa miaka 15.
Maili mbali katika milima ya Iten, inayojulikana kama nyumba ya mabingwa wa kuwachukua wanariadha wengi maarufu nchini, wanariadha wana matumaini kwamba ushindi wa Ruto ungefaidi mchezo huo.
Uwanja wa Kamariny - ambao Bw Ruto aliahidi 2017 utakamilika baada ya miezi sita - bado uko katika ukarabati.
"Kuna ukosefu wa uungwaji mkono kwa wanariadha ambao wanataka kushindana katika mashindano ya mbio. Ndio maana tunaona upendeleo wa mbio za barabarani. Hakuna vifaa vya wanariadha kujifunzia katika mashindano," kocha Peter Bii anasema, akiwalaumu wakandarasi kwa kuchelewa kukamilisha kazi ya uwanja.
Anasema wanariadha wengi wanaokuja Iten kufanya mazoezi kwa sababu ya eneo hilo huishia kuchanganyikiwa kwa sababu ya kukosa kuungwa mkono - na wanataka kuwa na mpangilio bora.
"Bw Ruto atahitaji kusambaratisha Riadha Kenya kwani muundo wake wa sasa umejaa wastaafu ambao hawana ubunifu," asema.
Matamshi ya kocha huyo yanasisitiza matarajio makubwa ambayo wafuasi wa Bw Ruto wanayo - lakini kwanza atahitaji kuwaonesha yeye ni mshindi.