Uchaguzi Kenya 2022:David Mwaure anayegombea urais Kenya ni nani?

David Mwaure

Chanzo cha picha, David Mwaure/FACEBOOK

Maelezo ya picha, David Mwaure mgombea urais Kenya wa chama cha Agano
    • Author, Asha Juma
    • Nafasi, BBC Swahili
  • Iliyochapishwa

David Mwaure Waihiga ni mmoja wa wa wagombea wa urais katika uchaguzi wa Kenya unaofanyoka agosti tarehe 9 mwaka huu . Baada ya kuhudhuria shule ya msingi na ya upili, alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi, ambako alisomea sheria.

Mwaure ni kiongozi wa chama cha Agano kilichoanzishwa mwaka 2006.

Anagombea kiti cha urais kwa mara ya pili baada ya kujitolea kuwania nafasi hiyo mwaka wa 2013 lakini baadaye akaghairi azma yake hiyo na kujiondoa kinyang'anyironi.

David Mwaure Waihiga ambaye amejitokeza kuwania viti mbalimbali vya uchaguzi katika chaguzi zilizopita ni wakili mwandamizi na amehudumu kama wakili kwa muda mrefu akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 35 baada ya kumaliza shahada yake ya Sheria mwaka wa 1981 katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Mwaure pia ana shahada ya uzamili katika uongozi na kwa sasa anasomea Shahada ya Uzamivu katika fani hiyo hiyo.

Bwana Mwaure, sio mgeni katika ulingo wa siasa kwasababu hapo awali aliwania viti tofauti vya uchaguzi katika ngazi ya eneo bunge na kaunti.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Raila Amollo Odinga

Muungano wa Azimio la Umoja

  • Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
  • Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
  • Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
  • Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
  • Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
  • Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
  • Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  • Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
  • Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

William Samoei Ruto

Muungano wa Kenya Kwanza

  • Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
  • Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
  • Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
  • Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
  • Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
  • Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
  • Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
  • Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
  • Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
  • Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC

George Wajackoyah

Chama cha Roots

  • Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
  • Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
  • Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
  • Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
  • Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
  • Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
  • Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
  • Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito

David Mwaure Waihiga

Chama cha Agano

  • David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
  • Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
  • Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
  • Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
  • Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
  • Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
  • Kupambana na ufisadi uliokithiri.
  • kuunda nafasi za ajira.
  • Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

Baadhi ya mapendekezo katika manifesto yake

David Mwaure

Chanzo cha picha, David Mwaure/TWITTER

Maelezo ya picha, David Mwaure ameahidi kukabiliana na ufisadi iwapo atachaguliwa kuwa rais

Chama cha Agano kimebandikwa jina la ''Mabadiliko'', yaani Change kwa Kiingereza, huku manifesto ya chama hicho ikitoa (ahadi) 12.

Nazo ni: Agano kwa katiba, Familia, Wanawake, Vijana, Watu Wanaoishi na Ulemavu, Serikali za Kaunti, Wafanyakazi, Wamiliki wa Biashara, Uchumi, Taasisi za Kidini, Mazingira, pamoja na Agano kwa Jumuiya ya Kimataifa.

Iwapo yeye na mgombea mwenza wake, Ruth Mutua, wataingia mamlakani mnamo Agosti, David Mwaure ameahidi kuongeza mgao wa mapato kwa kaunti hadi 40%, na kuteua 10% ya 40% kwenda moja kwa moja kwa mabaraza ya miji

Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Chagua suala ambalo linakuvutia

Sera za kila chama

  • Azimio La Umoja One Kenya Coalition

  • Roots Party of Kenya

  • Chama cha Agano

  • Kenya Kwanza Alliance

Mwongozo huu ni muhtasari wa sera kuu zinazotolewa na kila chama.

Pata maelezo zaidi kuhusu wagombea urais wa Kenya hapa

End of Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Bw. Mwaure ananuia kuunda jopo kazi kuchunguza uwezekano wa kuvunjwa kwa Kaunti ya Nairobi baada ya uchaguzi huu ili baada ya 2027, gavana wa Nairobi awe anateuliwa na rais baada ya uchaguzi na mjumbe wa moja kwa moja wa baraza la mawaziri.

Katika mpango wake kwa wafanyakazi wa Kenya, ameahidi msamaha wa jumla wa 50% ya PAYE(Kodi ya mapato), pamoja na mazingira mazuri kwa sekta ya kibinafsi, watu binafsi na wengine kuanzisha biashara kwa nia ya kukuza ujasiriamali.

Hali mbaya ya kiuchumi pia iko kwenye manifesto yake, na mpango wa kuhamisha shirika la urejeshaji mali kwa afisi ya rais,kupeleka bajeti kwa mabaraza ya miji tofauti na ofisi ya hazina au bajeti ya Ikulu, na kutafuta wale vigogo waliohusishwa na sakata za rushwa na kuhakikisha wanafuatiliwa kwa mujibu wa sheria.

Wakili huyo ameapa kukabiliana na ufisadi.

"Sisi Agano tunasema ni wakati wa mabadiliko, tunasema ni wakati wa Kenya kuwa na uongozi mpya, tunasema pia Kenya haitakwenda popote tukiwachagua viongozi walewale waliokuwepo miaka nenda, miaka rudi. Ni wakati wa kumaliza laana na vitendo vya ufisadi na kashfa," anasema Mwaure.

Aidha, amesema iwapo atachaguliwa serikali yake italenga kurejesha mali zote zilizoibwa zilizofichwa nje ya nchi na ndani, kushughulikia mdororo wa kiuchumi unaoikabili nchi na kuwa sauti ya wasio na uwezo.

Mwaure pia anakusudia kuunda mfumo wa kisheria utakaohakikisha kuwa ripoti za ukaguzi wa hesabu za sekta ya umma ni ushahidi wa kimsingi katika matumizi mabaya ya ofisi na matumizi mabaya ya fedha.

"Tutahakikisha Ksh. trilioni 15 zilizoibwa na kufichwa nje ya nchi zinarejeshwa Kenya kwa mashauriano na nchi zote husika zilipo fedha hizi," ameahidi Bw Mwaure.

Serikali yake pia ina nia ya kuweka kikomo katika jumla ya malipo ya mkopo kutoka kwa serikali hadi Ksh.1 trilioni.

"Hii itatoa Ksh.350B mara moja kusaidia miradi ya serikali.

Tutaitisha kwa dharura mkutano na wakopeshaji wetu ili kufikia mpango mpya wa ulipaji ili kuhakikisha nchi haiingii katika dhiki ya madeni," alisema Mwaure.

Uchaguzi
Maelezo ya picha, Uchaguzi Kenya

Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma

Uchaguzi